Kwanini CCM Iko Matatani?

Kutoka maktaba ya JamiiForums. Hivi CCM hii ya kuchota pesa toka hazina bila idhini ya Bunge, ya kukaa kimya pale miili ya Watanzania inapookotwa ufukweni, ya kukosa sera za kuwavutia wanachama wapya badala yake kutumia rushwa ya pesa na vyeo, ya kudharau katiba, mahakama m, Bunge na sheria za nchi, yenye kuleta hofu na taharuki kila kona nchini ndiyo CCM ambayo Watanzania wanaitaka? Kama ndiyo CCM hii ambayo Watanzania wanaitaka kwanini ihofie katiba mpya ya rasimu ya Warioba na Tume huru ya uchaguzi? Kwanini ihofie uchaguzi huru na wa haki?
 
Well.. swali hili labda linahusu CDM Zaidi sasa kuliko CCM. CCM sasa hivi haiko matatani kwani inaogelea kutegemea upepo wa Magufuli. Ukiangalia sana ni kama CCM haipo. Hofu yangu ni kuwa CCM inaweza kuwa imeganda hadi 2015; itaganduka mwisho wa utawala wa Magufuli na kurudi iliko kwani hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika ndani ya CCM ambayo kama chama unaweza ukasema iko tofauti na ilivyokuwa 2015. Yawezekana pia matatizo ya CCM sasa hivi yamejificha kwa kivuli cha umaarufu wa Rais Magufuli. Bado sijashawishika kama CCM ya sasa ni tofauti na ile ya 2015.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

CCM imekuwa mahututi ikisubiri kifo kwa muda sasa. Hali yake ilidhihilika kuwa mbaya sana kuelekea uchaguzi wa 2015.

Hii inaelezeka vizuri kwa kuangalia nguvu (mabavu ya dola, udanganyifu na fedha) zilizotumika na viongozi wa chama hicho, na zinazoendelea kutumika ku-uminya upinzani na sauti yoyote ile inayoenyesha kuwa CCM na viongozi wake;

1. wameharibu nchi, na wameshindwa kutatatua matatizo ya msingi ya wananchi.
2. wamehishiwa mbinu za kurekebisha na. 1 na hivyo hawafai kushika dola.

Njia pekee ya CCM mahututi kuweza kubaki hai ni kwa kuwekewa mashine za kusukuma siku kwa;

- kuua kabisa chama mbadala chochote,
- kufuta kabisa sauti ya upinzani kutoka katika vyama vya siasa au wananchi wa kawaida,
- kuhakikisha sauti inayosikika ni ile ya Mema tu ya CCM na uongozi wake, hata kama hayana ukweli au mantiki, kupitia radio, luninga, mitandao na magazeti.

Uongozi wa CCM unaoneka kushindwa kutambua kuwa CCM ni mahututi kwa kuwa IMEPITWA NA WAKATI. Haiendani kabisa na nyakati tulizonazo;

1. Inategemea sana mabavu na udanganyifu na sio nguvu ya hoja, uwazi na ukweli, Hivyo - kwa mfano, viongozi wake hawawajibiki na hawahitaji kuwa na mantiki/logic katima maamuzi au matamko yao.

2. Inategemea sana "umbumbumbu" wa wananchi ili kuendelea kushika dola, lakini sasa wananchi wanazidi kuamka na hii inawatisha sana,

3. Haina jinsi ya kupata masuluhisho ya matatizo ya msingi na ziada ya wananchi - piga ua, CCM haina rasimali watu wenye uwezo huu, na mfumo wake wa uendeshaji unategemea sana uongozi wa juu wa chama kuwa na uwezo wa mkubwa kiakili (genious like) ili kufanikiwa. Watasubiri sana kumpata wa namna hii.

4. Haina rasimili watu wa kuifanya iwe ya kisasa (kuondokana na 1, 2 na 3) na haina nia, mipango/utaratibu wa kuipata rasimali hiyo.

- etc.

Kifupi kifo cha CCM hakiepukiki, ni swala la muda tu.
 
Umaarufu wa Magufuli kwenye lipi? Chuki za kutisha, vitisho, visasi, kudharau sheria za nchi, katiba, mahakama, Bunge, kutoa rushwa ya vyeo na pesa ili kuwanunua wachumia tumbo? Huu umaarufu wa Magu umefanya utafiti lini na wapi ili kuhitimisha kwamba ana umaarufu na chanzo cha umaarufu huo ni kipi kati ya haya mambo niliyoyataja!?

Well.. swali hili labda linahusu CDM Zaidi sasa kuliko CCM. CCM sasa hivi haiko matatani kwani inaogelea kutegemea upepo wa Magufuli. Ukiangalia sana ni kama CCM haipo. Hofu yangu ni kuwa CCM inaweza kuwa imeganda hadi 2015; itaganduka mwisho wa utawala wa Magufuli na kurudi iliko kwani hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika ndani ya CCM ambayo kama chama unaweza ukasema iko tofauti na ilivyokuwa 2015. Yawezekana pia matatizo ya CCM sasa hivi yamejificha kwa kivuli cha umaarufu wa Rais Magufuli. Bado sijashawishika kama CCM ya sasa ni tofauti na ile ya 2015.
 
Safi sana BAK,ni suala LA muda tu ...JPM anaonekana kuijenga CCM lakini anatumia matofali ya barafu!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom