Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,823
- 12,278
Wote tunafahamu mwaka jana Rais Samia alipata mkopo wa civid-19 wa takribani Shilingi trilioni 1.5, fedha ambazo zimetumika kujenga vyumba vya madarasa na Hospitali.
Watanzania tukaaminishwa kuwa sasa changamoto ya madarasa na madawati imekuwa historia. Cha kushangaza kumeibuka tena wimbi la watendaji wa kata kuanza kuchangisha fedha za kujenga vyumba vya madarasa katika wilaya nyingi.
Je, wilaya hizo hazikupeleka mahitaji yao ya kutosha kukumilisha ujenzi huo? Na kama ni hivyo je watendaji wa wilaya hizo hawastahili kuadhibiwa kwa kuhujumu mradi huu?
Hii sasa ni kero, wananchi tumechoshwa na michango kila kukicha!