Ndejembi Hajaridhishwa na Usimamizi wa Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa Chemba - Dodoma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,908
945
NDEJEMBI HAJARIDHISHWA USIMAMIZI WA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA CHEMBA – DODOMA

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Deo J. Ndejembi (Mb) hajaridhishwa na hali ya usimamizi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa na Ofisi katika halmashauri ya wilaya Chemba Mkoani Dodoma kupitia Mradi wa Kuimarisha Ujifunzaji katika Elimu ya Awali na Msingi (BOOST).

Ndejembi ameona hali hiyo leo tarehe 31 Mei, 2023 wakati akikagua ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa, ofisi mbili na matundu ya vyoo katika Shule ya msingi Soya wilayani Chemba mkoani Dodoma vitakavyogharimu milioni 97.1.

Wakati akikagua miundombinu hiyo, Naibu Waziri Ndejembi amebaini na kujionea matofali yanayotumika katika ujenzi huo kutokidhi viwango ambapo baadhi ya matofali yanayoendelea kutumika katika ujenzi huo ni mabichi na hayakidhi viwango na vigezo vilivyotolewa.

Ndejembi amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Suluhu Hassan Suluhu tayari ametoa bilioni 1.3 katika wilaya Chemba ili kuimarisha miundombinu ya elimu ya awali na msingi kupitia Mradi wa BOOST, kwahiyo lazima wahakikishe fedha hizo zinasimamiwa na kutumika kikamilifu.

Kadhalika, Amemuagiza Afisa Elimu Wilaya Chemba kutoondoka katika kituo chake cha kazi kwa kusafiri nje ya wilaya hadi ujenzi wa madarasa, ofisi na vyoo vinavyojengwa kupitia mradi wa BOOST vikamilike.

Ndejembi amesema Serikali haitawafumbia macho watumishi wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao kikakamilifu ikiwa ni pamoja kufanya kazi kwa mazoea na kushindwa kusimamia fedha nyingi za miradi ya maendeleo inayoendelea kutolewa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Vile vile, Ndejembi ameagiza kazi zote za ujenzi wa Madarasa, Ofisi na Vyoo pamoja na kuweka Madawati kupitia Mradi wa kuimarisha Ujifunzaji katika Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) ziwe zimekamilika ifikapo tarehe 30 Juni 2023.

IMG-20230531-WA0151.jpg
IMG-20230531-WA0148.jpg
IMG-20230531-WA0146.jpg
 
Back
Top Bottom