Kwanini baadhi ya watanzania wanadharau elimu?

Nkerebhuke

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2021
Posts
796
Reaction score
2,027
Inawezekana kuna kundi kubwa halijua maana ya elimu ndio maana imekuwa ni kawaida sana kuisimanga, kuibagaza na kuishusha elimu. Elimu ni maarifa, elimu ni ujuzi, elimu ni mwanga, elimu ni silaha, elimu ni kio, elimu ni Pesa, elimu ni tiba, elimu ni kila kitu kwenye Maisha ya mwanadamu yoyote katika Dunia yoyote. Leo anatokea mtu anadharau badala ya kutoa maoni namna gani tutaunda na kuboresha elimu yetu.

Watanzania baadhi wanakera sana na bahati mbaya wengine wako bungeni kuibagaza elimu sijui inawezekana tumerogwa. Watu wanakalili wanafikili wasomi wanaweza kufanya miujiza wakihisi pengine msomi ni malaika hapana. Taifa letu lina wasomi wazuri ambao ujuzi wao unatumika vizuri kuliletea maendeleo na ustaarabu taifa, wapo serikalini na sector binafsi.

Inasikitisha sana maana hii laana imewashukia hata wasomi wenyewe kuweza kujidhalau na kushindwa kujiamini, kutetea mawazo, kupigania taaluma za kulinda hadhi na heshima ya utu wao. Hivi leo watu wanaita vyeti makaratasi kwa dhihaka hii ni laana sio bure. Kama kuna changamoto kwenye elimu yetu, tuiboreshe na sio kuibagaza inakera sana tunadhalau elimu huku tukipeleka watoto wetu shule
 
Inasikitisha sana maana hii laana imewashukia hata wasomi wenyewe kuweza kujidhalau na kushindwa kujiamini, kutetea mawazo, kupigania taaluma za kulinda hadhi na heshima ya utu wao.
Sidhani kama unawatendea haki "Wasomi"
 
Mkuu

Elimu yetu ni mbovu na mfumo wake haufai!

Elimu ya sasa haina majibu ya changamoto zilizopo!

Ndio . maana wasomi wamekimbilia kwenye siasa ili wapate fedha nyingi!

Elimu ya kikoloni imekosa majibu na hadhi yake!!

Leo hii HATA ukitumia gharama kubwa kusomeshavhaimsaidii kijana kutatua changamoto za maisha binafsi!!!

Elewa HIVYO!!
 
Am just curious nani anajukumu na future ya elimu yetu, wewe unasema elimu yetu ni mbovu bila kubainisha eneo hata moja ambalo linapaswa kurekebiswa unataka nani afanye hivyo. Kuna vitu vya kudadisi je mazingira ya fit kwa vijana wasomi kuweza kutumia vipaji vyao( environment fit ) hakuna monopoly? Tuongeze au tupunguze nini kwenye mitaala yetu, jamii ya Tanzania inapenda kujifunza
 
Elimu inaongeza life expectancy isipuuzwe..na mara zote wanaoipuuza ni wale walioikosa, chamsingi serikali ionyeshe kuwa education is matter kwa kufanya yafuatayo...
1. Ili mtu kugombea ubunge awe na Shahada ya Pili.
2. Cheo chochote kuanzia ngazi ya kata iwe ni kuanzia Elimu ya masters degree.
3 waitambue Shahada ya Pili kwenye mishahara ya watumishi.
4. Nk
Hizo kelele za kuidharau Elimu zitapotea automatically, mf. huwezi ukawa unapinga ukatili wa kijinzia huku unaidharau Elimu hyo haileti mantik
 
Kwanini imekuwa hivyo Namba moja ajaye? Kwa nini Elimu inayopatikana haitatui changamoto za maisha binafsi?
Imepitwa na wakati!

Nyakati zetu hazihitaji elimu za kukariri principle bali elimu tendaji ile ya field inayozaa kitu cha kuonekana na kutengeneza pesa halisi!!

Elimu hii iliopo ni ya kurithi toka kwa mkoloni yaani kuandaa watumishi wa serikali sasa watumishi wametosha na kuzidi inapaswa ibadilike ghafla na kuwa ya kujitegemea na ubunifu ukitumia nature kutatua changamoto!

Juzi nimeenda seminar ya sayansi ya walimu wa secondary nikaona ujinga uleule unapakwa rangi tu!hakuna cha maana ambacho kitaleta fedha baada ya mtoto kuhitimu yaani tunaandaliwa kufundisha jinsi vijana wajibu maswali ya competence based yaani kujiandaa kwa mitihani badala ya maisha halisi!huo ni ujinga hatari sana!

Niliwaambia haya ni mapokeo hayana majibu kwa vijana kuhusu kujiajiri na kujitegemea wakabaki wananishaangaaa tu eti naenda kinyume na wakufunzi!

Elimu ya sasa ujinga mtupu!

Jua HIVYO!!
 
Hua HIVYO!!
Mwl unawaza kutengeza pesa tu😄 kuwa na Elimu yyte Ile kibinadamu ni zaidi ya pesa
 
Elimu inaongeza life expectancy isipuuzwe..na mara zote wanaoipuuza ni wale walioikosa, chamsingi serikali ionyeshe kuwa education is matter kwa kufanya yafuatayo...
1. Ili mtu kugombea ubunge awe na Shahada ya Pili.
2. Cheo chochote kuanzia ngazi ya kata iwe ni kuanzia Elimu ya masters degree.
3 waitambue Shahada ya Pili kwenye mishahara ya watumishi.
4. Nk
Hizo kelele za kuidharau Elimu zitapotea automatically, mf. huwezi ukawa unapinga ukatili wa kijinzia huku unaidharau Elimu hyo haileti mantik
Na mimi naongezea hapo mamlaka zetu ziangulie hali ya soko inchini ili kuangalia kama kuna monopolistic elements kuwapa fursa vijana wanapobuni bidhaa zao waweze kushindana vizuri.
 
Unasoma miaka kibao bado huwezi kujimudu
Anatokea mtu anakufundisha forex kwa mwezi unajimudu.....hapo shule za kazi gani???
 
Elimu inaongeza life expectancy isipuuzwe..na mara zote wanaoipuuza ni wale walioikosa, chamsingi serikali ionyeshe kuwa education is matter kwa kufanya yafuatayo...
1. Ili mtu kugombea ubunge awe na Shahada ya Pili.
2. Cheo chochote kuanzia ngazi ya kata iwe ni kuanzia Elimu ya masters degree.
3 waitambue Shahada ya Pili kwenye mishahara ya watumishi.
4. Nk
Hizo kelele za kuidharau Elimu zitapotea automatically, mf. huwezi ukawa unapinga ukatili wa kijinzia huku unaidharau Elimu hyo haileti mantik
Elimu ninini? Acheni kuaminisha watu kwamba kukalili theories za watu wengine na kuzilazimisha zikae kichwani mwako ndio elimu sahihi!

Tambua dhana ya elimu ni pana sana tofauti kabisa na sisi hasa waafrica tunavyo ipokea na kuiamini .

Na ndio maana unaweza ukawa umeweza kukalili theories za wazungu hadi level ya PhD lakini problems analysis and solution zikaja kutolewa kwa usahihi na mtu ambaye hana hata certificate ila ni great thinker.

Kwenye elimu kinacho badilisha watu ni ile socialization kutoka kwa watu tofauti na misimamo pamoja mitazamo aliyo ikuta wakati anazaliwa.

Ndio maana mtu anaweza akawa hana elimu hiyo ya darasani lakini kajikita kwenye maswala ya dini na ana socialize na watu tofauti kwa upande huo naye atakuwa na ustaarabu kama ulio nao wewe mwenye PhD na mnaweza mkakaa same meeting na wote mkatoa hoja za msingi kabisa na pengine Ukazidiwa mbali kabisa.
 
Mkuu,elimu yetu rasmi ni mbovu kuliko ile elimu isiyo rasmi ya kupatikana mtaani
 
Elimu ninini? Acheni kuaminisha watu kwamba kukalili theories za watu wengine na kuzilazimisha zikae kichwani mwako ndio elimu sahihi!

Tambua dhana ya elimu ni pana sana tofauti kabisa na sisi hasa waafrica tunavyo ipokea na kuiamini .
Unachojua ww shuleni wanajifunza content tu🚮
Hizo theory zenyewe unajizua kuwa huwa zinahusiana na nn katika maisha ya binadam? Kama huzijui lazima utazidharau tu kwasabu unauelewa mdogo wa Mambo. Hebu
fanya jaribio la kutowapeleka wanao shule kiazi we!
 
Mkuu,elimu yetu rasmi ni mbovu kuliko ile elimu isiyo rasmi ya kupatikana mtaani
Hiyo Elimu isiyo rasimi ndo hyo ambayo imejaa unyanyasaji wa kijinzia, mtoto wa kiume ndo asome mtoto wa kike awe mke wa nyumban,
Elimu ni dawa ya maisha ya binadam mf., tabia za mtoto aliyefika darasa la Saba ukilinganisha na tabia za mtoto aliyefika kidato cha nne ni tofauti kabisa, unaona kabisa huyu mtoto aliyefika kidato cha nne anakitu kichwani
 
Imepitwa na wakati!

Nyakati zetu hazihitaji elimu za kukariri principle bali elimu tendaji ile ya field inayozaa kitu cha kuonekana na kutengeneza pesa halisi!!

Elimu hii iliopo ni ya kurithi toka kwa mkoloni yaani kuandaa watumishi wa serikali sasa watumishi wametosha na kuzidi inapaswa ibadilike ghafla na kuwa ya kujitegemea na ubunifu ukitumia nature kutatua changamoto!

Juzi nimeenda seminar ya sayansi ya walimu wa secondary nikaona ujinga uleule unapakwa rangi tu!hakuna cha maana ambacho kitaleta fedha baada ya mtoto kuhitimu yaani tunaandaliwa kufundisha jinsi vijana wajibu maswali ya competence based yaani kujiandaa kwa mitihani badala ya maisha halisi!huo ni ujinga hatari sana!

Niliwaambia haya ni mapokeo hayana majibu kwa vijana kuhusu kujiajiri na kujitegemea wakabaki wananishaangaaa tu eti naenda kinyume na wakufunzi!

Elimu ya sasa ujinga mtupu!

Hua HIVYO!!
Education is the foundation in which our country is built on. Kwenye elimu kuna vitu vingi vya kuangalia badala ya kuidharau na kuibagaza, wengi tumeweka over emphasize on materialism lakini elimu ni zaidi yaho, Kuna value development, covering culture and the likes. Tusiwape nafasi wasiojua umuhimu wa elimu ni nini ila tujenge hoja za kisayansi kuonesha ni wapi elimu yetu unapaswa kuelekea
 
Unachojua ww shuleni wanajifunza content tu🚮
Hizo theory zenyewe unajizua kuwa huwa zinahusiana na nn katika maisha ya binadam? Kama huzijui lazima utazidharau tu kwasabu unauelewa mdogo wa Mambo. Hebu
fanya jaribio la kutowapeleka wanao shule kiazi we!
Watu Wana masters hawawezi kumudu kulipa Kodi ya chumba cha 50,000 wanakaa kwa wazazi wao.

Mafundi kushona, pikipiki, wachona mahindi wanamudu hivi vyumba.

Shule ya kazi gani?????
Form four tu yatosha mengine ziada
 
Hiyo Elimu isiyo rasimi ndo hyo ambayo imejaa unyanyasaji wa kijinzia, mtoto wa kiume ndo asome mtoto wa kike awe mke wa nyumban,
Elimu ni dawa ya maisha ya binadam mf., tabia za mtoto aliyefika darasa la Saba ukilinganisha na tabia za mtoto aliyefika kidato cha nne ni tofauti kabisa, unaona kabisa huyu mtoto aliyefika kidato cha nne anakitu kichwani
Huelewi informal education wewe
Mdogo wangu wa like nilimpeleka kwa fundi simu konki mahala Fulani....
Kakaa na yule fundi mwaka na miezi kumi...leo dogo ni fundi simu na electronics kibao.
Amepanga anaishi na dada yake ambaye ana degree ya procurement mwaka wa tano hana kazi
 
Back
Top Bottom