Kwanini baadhi ya wanaume hamuwapendi Feminists?

Kwanini baadhi ya wanaume hamuwapendi Feminists?

Status
Not open for further replies.
Feminism; If not monitored...comes wth hints of anger and disrespect to a Man

iwe kauli ama vitendo

ni mada pana kwa kweli
 
Nimesoma Michango ya wadau na hoja zao Mstari kwa kwa Mstari.
Itoshe Kusema Dunia imebadilika sana. Yesu urudi upesi
 
Mimi ni ke mkuu! Andiko lako limenibariki sana na siku zote huwa napenda watu wanaosimamia wanachoamini haijalishi wataonekaje na haijalishi watapingwa na watu wengi kiasi gani!
That's my girl... na kwa sie wanaume tunaposimamia mambo kama haya ndo pale wengine wanatuona uanaume wetu haujakamilika, au tukifanya sehemu kama hizi wengine wanaona tunafanya mauzo ; yaani taabu tupu!
 
James delicious hamshindi utamu baba yako, babako ana tako laini zaidi
Aisee mkuu Andie kwa heshima zote naomba usiingize mambo ya wazazi ktk hili,sometimes mzee wake anajuta kwanini alizaa kiumbe kama hiki.
 
That's my girl... na kwa sie wanaume tunaposimamia mambo kama haya ndo pale wengine wanatuona uanaume wetu haujakamilika, au tukifanya sehemu kama hizi wengine wanaona tunafanya mauzo ; yaani taabu tupu!

Na wanaume kama ninyi mmebaki wachache sana juu ya uso wa hii dunia!

Anyway nimpongeze tu in advance huyo wifi yangu utakayemuoa (kama bado haujaoa) niseme tu kuwa namuonea wivu sana aise na ninamshauri tu asiichezee hii bahati!
 
naona kama kuna mahala humu tunachanganya hadithi na mwisho wa siku kwenda nje ya maada.

Nini maana ya feminist, namna gani hii feminism inakuwa applied na tafsiri inataka nini duniani na Africa?

Ipi nafasi ya mwanamke kwenye familia na jamii.
Ipi nafasi ya mwanaume kwenye jamii na familia.

Mwanamume anapashwa kuwa na majukumu sawa na mwanamme and vice versa kwa mwanamke.?

Nini maana ya ndoa ya mwanamke na mwanaume.
Kwanini wanawake wasioane wenyewe na wanaume wasioane wenyewe?.

Imani zinazungumziaje nafasi ya mwanamke kwenye ndoa na jamii, ukristo, uislamu, upagani, uhindu, ubudha nk?

Maada ni pana sana naona tuko out of phase na kufikia kuparuana...lets be free and discuss without taking wrong anybody its just a discussion and views mwisho wa siku kila mtu anafamilia yake achievement zake na failures zake..
 
Mi naona Ni mfumo mzuri Sana unaomlinda na kumpa Mwanamke mamlaka, Wana haki ya kukosea na kujifunza, wanahaki ya kuwajibishwa pia wakizingua plus hii itatupunguzia mizigo wanaume yale Mambo ya kuhangaika huko uku Jianamke linanenepesha Makalio home unakuta hamna, kila mtu akatafute alete na Kama Mwanaume unaona usawa haupo sawa kwani Ni lazima kuoa mazeee?

Kwanza mi naona ndoa Ni mtego wa mwanamke kubenefit kutoka kwa Mwanaume, huu usawa wa mafeminist utapunguza kelele Home hata kwa wale wamama ambao wanachakalika ndani ya ndoa Kisha wanawalalamikia Waume zao kwamba hawawahudumii, wataacha kulalamika hovyo na wataona pia Ni majukumu yao kupambana na kuhudumia familia pia..
Mi ndo nshaamua Swala la Ndoa mpaka Maulana akipenda, Saizi nazisaka ndalama kwa hasira ili nipate Uhuru wangu wa kuchagua.. Hayo Mapenzi ngoja wakae nayo kwanza na watoto watazaliwa na wengine tu!!! Sina udhaifu Wala Mapungufu maana kama Ni matendo ya ndoa Nimefanya weee hata sijaona faida zaidi ya hasara tu na kutiana nuksi
 
Kwenye maisha kuna mila na tamaduni kwa kila jamii hapa duniani ambazo zinafanya kazi kwa jamii husika...

Waarabu wana mila na desturi zao.
Wahindi wana mila na desturi zao.
Wazungu wana mila na desturi zao.
Wachina na WaAfrica pia..

Zipo pia dini au imani ambazo kuna waliochagua kuzifuata na kufanya sehemu ya maisha yao.
 
Nani alisema wanawake wawe chini na usilete blah blah Mara maandiko ya hadithi za kusadikika hapa,
Swali zuri sana, nataka twende kielimu na si habari za paukwa pakawa na hisia za kihamasa.

Naomba unipe muongozo katika nukta hizi zifuatazo. Naomba uniambie ni wapi turejee ili tupate majibu sahihi nje ya maandiko ?

Pili, hadithi za kusadikika zina sifa gani ? Naomba unithibitishie ya kuwa ni kweli hizo unazo ziita wewe ni hadithi za kusadikika ni kweli ni za kusadikika. Ukishindwa hili, itabidi ukiri hadharani ya kuwa unaandika mambo usiyo kuwa na elimu nayo, na huu ni ujinga usiyo faa kupigiwa mfano.
 
Hii hoja kuna baadhi ya watu wake kwa waume wanairukia pasipo kuielewa. Kabla ya kuwajadili feminist kwa maana wafuasi wa hicho kitu ni vyema tukajadili kitu chenyewe ni nini, ambacho ni feminism.

Feminism wanasema kwa urahisi ni jinsia zote zinahitaji haki sawa na fursa (ambazo zimo kwenye jamii). Itikadi yao ni kuwa maadamu wote ni binadamu basi mwanaume na mwanamke ni sawa. Kwa maana hiyo wanawake wanahitaji haki sawa ndani ya jamii kama mwanaume.

Wanachoshindwa kufahamu ni kwamba mwanaume na mwanamke ni sawa kwa hali ya ukiumbe! Kwa maana wote ni binadamu. Lakini hawa binadamu wana utofauti wa kimaumbile, nguvu, ujasiri, nidhamu za kibailojia, kufikiri n.k na tunaishi kwenye jamii ambayo inatubidi tuwajibike.

Kwa muktadha wa namna huu kwa kutofautiana huku ni lazima kutakuwa na mgawanyo wa majukumu kwenye kuyaendea mambo kuwajibika kwenye jamii. Mambo mengine yanatokana na kanuni na nidhamu za kimaumbile (nature) mfano mwanamke anapenda kupika na majukumu mengine ambayo yanafahamika mwanamke anayoyafanya. Halikadhalika kwa mwanaume.

Feminist wanachokitaka ni usawa lakini usawa wao hawauhitaji kwenye majukumu. Mathalani kwa hapa Tz mwanamke anayedai usawa akiambiwa naye ahudumie familia kwa hali na mali kama mwanaume anavyojitoa kutoka kwenye pato lake hawakubali. Ukienda Uk wanataka walipwe mshahara mmoja na mwanaume wakati kwenye kitengo hicho hicho mwanaume anafanya kazi ya ziada ambayo inamlazimu atumie nguvu za mwili wake pia ukiacha taaluma.

Ni sawa sawa kusema Simba,Chui, Swala, Mbuzi, Duma, Paa wote wapewe majukumu sawa! Jawabu kwa vile wote ni wanyama. Huku ni kujibu kwa kuona na si kwa kutumia akili.

Ukiangalia kote feminists wanapigania ubinafsi na si haki sawa! Wafahamumwanamke na mwanaume si sawa kwa maana ya kimajukumu. Ni vyema wapiganie unyanyasaji wa kijinsia. Ila suala la haki sawalikiwekwa watakaopata madhara makubwa ni wao. Wanapigania kitu ambacho hawafahamu uhalisiya wake.

Moja ya athari hasi ya feminists hawana nidhamu. Si nidhamu ya kuongea ki kauli wala kuandika kimaandishi. Hawajali hisiya za mtu aliye tofauti na mtizamo wao ila wanataka hisiya zao zijaliwe.
 
Kuna wanawake wakuwajibu kwa staha sio haya manungaiyembe mimi hua siyathamini hata punje nayaona kama ****** muozo tu.
Kwa hiyo mtu asipokujibu kwa staha unamshushia mvua ya matusi?
Huoni hapo unakuwa kama yeyebambaye umemwita 'asiye na akili'?
Wote mnakuwa kundi moja tu.
 
Haki neno pana.haki kwa mujibu wa dini au kwa mujibu wa sheria za kidunia au kwa mujibu wa wanaharakati wa haki za wanawake.
 
wanawake tuko juu ndio maana wanaume humu mumetukana mumeshindwa kweli kujiamini na kujibu hoja.
Wanawake mpo juu ya nini ? Na hapo juu nani amewaweka ?

Mimi binafsi sijaona hoja humu, wala haitokuja kutokea, zaidi ya hisia na ujinga mwingi. Naomba unionyeshe hoja zenu humu kama nyinyi mnasema ukweli.

Kujibu hoja au kushindwa hoja kunategemea na nani unaye mjibu, kadhalika nini unajibu ?
 
Mara mkimbilie udhaifu nileteeni hyo kitu ya udhaifu na inahusiana na Nini tungekuwa dhaifu tusimgewazaa na kuwalea, in short mwanaume anayetaka aonekane ana uwalakini flani hivi.
Nimecheka sana, sasa bibie unajifaragua vipi kwa jambo ambalo umeumbiea kwalo mwanamke ? Mwanamke kulea ndiyo jukumu lako. Ndiyo maana nasema hamna hoja sababu hata jukumu lako hulijui na hujui ni upi udhaifu unao zungumziwa hapa, hili ni tatizo lingine.Huku kwetu tutakushauri ya kuwa na uishi katika kauli hii "Tengeneza kiti chako kabla ya kukitia nakshi". Ulitakiwa ujue kwanza nini kinachozungumziwa kabla ya kupinga, huu ni udhaifu mwingine.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom