Kwanini baadhi ya makanisa yanaweka mabango kuwaasa waumini wavae kwa heshima wakati kinachoangaliwa ni roho na sio mavazi?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,034
Huku ni kukosa mafunzo sahihi ya sheria ya mavazi kwa viongozi wetu wa makanisa ndio maana wanalazimika kuweka matangazo juu ya mavazi, sisi wakristo inajulikana wazi kwamba kinachoangaliwa ni roho sio mavazi, kuna haja ipi ya kuweka haya mabandiko ? uliona wapi misikitini wanaweka matangazo ya aina hiyo ?

Nijuavyo kinachoangaliwa ni roho na sio mavazi, haya makatazo yalishapitwa na muda ni mambo ya agano la kale lililokataza kula wanyama kama mbwa na nguruwe, kunywa pombe, kuvaa mavazi yanyositiri, kukataza kuchonga nywele na ndevu, n.k.


1701683485953.png
 
Kama Mungu yupo kila mahali, anaona na kusikia kila kitu, kwanini watu wanaenda kusali kwenye jengo maalum tu.

Dini ni siasa, ukiingia, zingatia vigezo na masharti.
 
Aliekuambia inaangaliwa roho sio mwili ni nani?
Mwili wako ni hekalu (nyumba) ya Roho mtakatifu

Kwahyo Roho mtakatifu anakaa ndan yetu kwa maana hiyo basi inatakiwa tuwe wa saf maana Mungu ni mtakatifu na neno Lake linasema Mungu anapendezwa na watakatifu walioko duniani.

Sigara pombe matukano mambo yasyofaa yanamwondoa Roho mtakatifu ndan yako kwakua hayo ni uchafu
TUNZA SANA MWILI WAKO TAMBUA MWILI WAKO NI HEKALU
 
Hapo lanisani wanatakiwa wavae nguo za heshima, wakitoka hapo wanao uhuru wa kuvaa vyovyote hata vipensi kama wakipenda na hakuna wa kuzuia.
Kila eneo lina taratibu zake.
kuna hii fasheni imejizolea umaarufu makanisani kuvaa magauni / sketi zinachoresha makalio, mapaja na hips, haya ni mavazi ya heshima ?


Photo by MOCU KCMC MWENGE MWEKA IAA TUMA on August 12, 2023. May be an image of 1 person and d...jpg
 
kuna hii fasheni imejizolea umaarufu makanisani kuvaa magauni / sjeti zinachoresha makalio, mapaja na hips, haya ni mavazi ya heshima ?

View attachment 2832956
Hiyo nguo haina tatizo. Hata akiingia kanisa lolote hakuna atakae mshangaa wala kumrudisha.
Makanisani wapo wanaume wanaojitambua sio wale wengine kule hata akiona kidole anadinda, maana muda wote wanawaza ngono.
 
Huko ni kukosa mafunzo sahihi ya sheria ya mavazi ndio maana wanalazimika kuweka matangazo juu ya mavazi, sisi wakristo inajulikana wazi kwamba kinachoangaliwa ni roho sio mavazi, kuna haja ipi ya kuweka haya mabandgo, uliona wapi misikitini wanaweka matangazo ya aina hiyo?

Nijuavyo kinachoangaliwa ni roho na sio mavazi, haya makatazo yalishapitwa na muda ni mambo ya agano la kale lililokataza kula wanyama kama mbwa na nguruwe, kunywa pombe, kuvaa mavazi yanyositiri, kukataza kuchonga nywele na ndevu, n.k.


Yaani wanawake waje na mavazi ya kutamanisha wanaume - kama yale ya kulalia, mgongo wazi, maziwa nje nje, vimini, hiyo Amri ya 9 ya Mungu haitavunjwa kweli?
 
Back
Top Bottom