sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,033
Hapo zamani nilishuhudia kwa macho yangu makanisa yalikuwa na tabia za ajabu kuwavisha kanga wanawake waliokuja wamevaa sketi zilizobana kwa mbali, waliovaa suruali hata ziwe pana walifukuzwa kabisa kurudi nyumbani.
Tunashukuru kadri muda umeenda makanisa yamejitambua, Leo hii wanawake wanaruhusiwa hata kuvaa suruali, gauni zinazowachoresha ili wapendeze, gauni zenye uwazi wa kupitisha hewa vifuani na mgongoni, n.k.
Kero kubwa ipo kwa makanisa kujitungia sheria za kukataza vimini na vipensi, huu ni ubaguzi !! Wadada wavae wanavyotaka, makanisa yasiingilie.
Sheria za agano la kale zilishapitwa na wakati,
-sheria za aina ya mavazi na makatazo ya kuchonga nywele zilishapitwa na wakati leo hii karibu kila mkristo anachonga nywele
- sheria za vyakula zilishapitwa na wakati kuna uhuru wa kula kitimoto.
- Sheria za kukataza kusuka nywele zilishapitwa na wakati leo hii makanisani ruksa kuvaa mawigi, kusuka rasta, weaving, n.k.