Kwani Morogoro kuna tatizo gani?

Kwani Morogoro kuna tatizo gani?

Serikali na vyama vya siasa huundwa na watu ambao hawana tofauti na mimi na wewe. Wana tamaa zao, Wana njaa zao, familia zao zina njaa. Wakipata fursa ya kupiga pesa zisizo na mlinzi watapiga. Hata ubadilishe kila bendera inapopandishwa na kushushwa, bado watapiga tu.
 
Sijui kuna tatizo gani katika Mkoa huo. Imekuwa ni kawaida kiongozi akienda ni lazima alalamikie matatizo ya matumizi ya fedha za Umma. Ameenda Rais, ameenda Waziri Mkuu, ameenda Jafo na hivi sasa kapita Katibu Mkuu wa CCM.

Wote kwa namna tofauti na kuhusiana na mambo tofauti tofauti wanalalamikia au kuibua matumizi mabaya ya fedha au usimamizi mbaya wa fedha. Kuna watu hadi waliondolewa lakini inaonekana kama Moro - Mji Kasoro Bahari - unaonekana kuwashinda au kushindwa!

Kuna tatizo gani Morogoro? Labda hata mikoa mingine hali iko hivyo lakini kutajwa kwa Morogoro mara kwa mara ni lazima kuwafanye watu wajiulize "kunani'?
Napapenda Morogoro,ukitumbuliwa unachagua tu njia ya kwenda kwenu,unachagua kwenda njia ya Dodoma,Iringa au kuelekea Dar,yoyote utakayochagua unafika kiulani,naona hii ndio inawafanya wabadhirifu wa fedha za serikali wasiwe na hofu...
 
Usituletee tena habari za huyo vuvuzela Bashiru Ally. Yeye akipita sehemu ni kupiga tu makelele na hanaga data siku zote.
Duh!
Umenikumbusha enzi zile Dr anashusha data za UFISADI hadi serikali inatetemeka.
Siku hizi hakuna mwenye data.
CCM hawana data.
CHADEMA ndo kabisaaa tangu wakatazwe na Lowasa 2015 kuusema UFISADI ndo wakafuta hadi nyimbo zao zoote na hata kelele tu hawapigi.
 
Tatizo ni ccm mkuu. Hao wafujaji wote ni wafuasi watiifu wa ccm. Ccm ni kama ukoo wa panya. Wakitoboa kabati lenye mishkaki hawaachi kitu.
Unachotuambia ni kuwa masharti ya ajira za utumishi serikalini ni kuwa wanachama wa CCM tu?
 
Unachotuambia ni kuwa masharti ya ajira za utumishi serikalini ni kuwa wanachama wa CCM tu?
Kwani hilo ni la kuuliza mkuu. Ushahidi umewekwa humu mara nyingi tu kuwa nafasi za ajira zinatolewa kwa wanachama wa ccm. Hasa watendaji wa Halmashauri. Hata mikopo ya wanafunzi inatolewa kwa kigezo cha kuwa mwana ccm siku hizi.
 
Hivi suala la katibi mkuu wa CCM kutembea na msafara linakaaje?

Maana jana tumesimamishwa sana foleni kwenye round about fulani hapa moro(siifahamu jina). Kuja kusikia eti katibu mkuu wa CCM anapita.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakubwa ni wengi , nimesikia mabalozi wa nyumba 10 wanapewa vitambulisho na wnaruhusiwa kuingia na kuhoji popote! Wakishaspewa vitambulisho,wanapewa maagizo muhimu ya nsmns ya kuisimamia S/ Kijiji, H/W nk. Hili ni sahihi kwa vile Serikali iliyo madarakani ni ya CCM. Itakapoingia ya Chadema kikatiba nao wataunda Serikali na wapange namna ya kuisimamia.
 
Kwani hilo ni la kuuliza mkuu. Ushahidi umewekwa humu mara nyingi tu kuwa nafasi za ajira zinatolewa kwa wanachama wa ccm. Hasa watendaji wa Halmashauri. Hata mikopo ya wanafunzi inatolewa kwa kigezo cha kuwa mwana ccm siku hizi.
Tusikubali hilo na tuache dhania. Haya tuarifiane nafasi za ajira hazitoki CCM, zinatoka utumishi ni hizo hapo tuzichangamkie. Usichanganye ajira na teuzi!!
 
Tusikubali hilo na tuache dhania. Haya tuarifiane nafasi za ajira hazitoki CCM, zinatoka utumishi ni hizo hapo tuzichangamkie. Usichanganye ajira na teuzi!!
Nina uhakika na nilichoandika. Ajira zinatolewa kwa upendeleo. Nimeshuhudia watendaji wakipewa ajira kwa kigezo cha kuwa wanaccm Wilayani Ulanga. Na siyo Wilaya hiyo tu. Zipo nyingi.

Kazopata kazozenga hio ni roho inawasumbua wana Moro
 
Sijui kuna tatizo gani katika Mkoa huo. Imekuwa ni kawaida kiongozi akienda ni lazima alalamikie matatizo ya matumizi ya fedha za Umma. Ameenda Rais, ameenda Waziri Mkuu, ameenda Jafo na hivi sasa kapita Katibu Mkuu wa CCM.

Wote kwa namna tofauti na kuhusiana na mambo tofauti tofauti wanalalamikia au kuibua matumizi mabaya ya fedha au usimamizi mbaya wa fedha. Kuna watu hadi waliondolewa lakini inaonekana kama Moro - Mji Kasoro Bahari - unaonekana kuwashinda au kushindwa!

Kuna tatizo gani Morogoro? Labda hata mikoa mingine hali iko hivyo lakini kutajwa kwa Morogoro mara kwa mara ni lazima kuwafanye watu wajiulize "kunani'?

Tatizo Mh. Raisi akisema hakuna kupinga na hao woote ni makasuku na kwa utawala huu tegemea hata ukienda wewe lazima useme kama hao wengine. Msubirie polepole pia atasema kama mkiti.
 
Kwani mikoa mingine wanateuliwa na mamlaka tofauti? Au hujaelewa swali Bi Akili finyu???

Sent using Jamii Forums mobile app
Mamlaka ya uteuzi Ni tatizo kubwa. Mikoa mingi tu Ni tatizo. Rais mwenyewe analalamika Kila uchao. Mfano anamlalamikia Makonda Mara nyingi. Wengi pia haturidhishwi na utendaji na hata style yake. Lakini bado yupo.na anadunda.
 
Back
Top Bottom