Kwani kuomba radhi ni udhaifu?

Kwani kuomba radhi ni udhaifu?

Mchokoo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2015
Posts
1,188
Reaction score
1,604
Ndugu zangu Watanzania hakuna binadamu asiyekosea, iwe ni kwa makusudi au bahati mbaya. Kimsingi hilo ndilo hudhihirisha ubinadamu wenyewe. lngawa mara nyingi tunapogundua makosa yetu tunajaribu kutoyakubali kama ni makosa!

Au tukikubali tunaona shida sana kuomba msamaha, tukidhani kuonekana ni dhaifu, kitu ambacho siyo kweli. Kimsingi mtu anayekubali kuwa amemkosea Mungu, au wanadamu wenzake ni nguzo ya shaba katikati ya kizazi cha waoga.

Hivyo basi naisihi serikali katika hili la mkataba wa bandari; ikubali kuomba radhi. Mkifanya hivyo hamtaonekana wadhaifu, bali wakomavu sana.

Msituangushe hata wale tunaowanga mkono tangu Mungu awaweke madarakani. Kwani ukitazama kwa makini sana ni kama hili limekuja kufuta mema yote yaliyofanywa na awamu hii.

Sasa kwa nini iwe hivyo, na kwa faida ya nani?
 
Nimeipenda lugha ya Waziri mkuu,
Pale ndio mwisho wa Mvutano.
DP- World inaenda kuleta mapinduzi ya kimkakati katika Bandari zetu.
Tujiandae kuongeza Mapato na kuwepo kwa uchache wa ajira za kwa watu waliozowea mikiki ya kufuatilia kila kitu kwa mguu na makaratasi mikononi. Hii habari kwisha , mambo yote ni dijitali tuu Wizi wa kjinga kwisha.
Badari itakuwa ni eneo shwari sana ,wataonekana wafanyakazi tuu kwenye control room na madereva wa Crane.
 
Umezunguka mno mkuu,sasa sijui aombe msamaha Kwa lipi? Kuna muda anajifunza kufanya kitu kibabe kama aliyepita maana hatuambiliki kitu
Mkuu To yeye, nimezunguka kivipi?
Kwani makosa siyo kawaida ya wanadamu wote? Na yakitokea tunaombana msamaha, na kurekebisha papotofu.
 
Msamaha unaombwa na mtu mwenye uadilifu na anaetambua wapi alipokosea...Katika maisha ni watu wachache sana wenye kijitambua hivyo usitegemee kuwa kila atake kukosea atakuomba radhi..Issue ya msingi ishi na walimwengu kwa akili mtu wangu!
 
Msamaha pekee bila kuniambia vipi utanitoa utumwani uliponipeleka ni ujinga, bora nisiombwe kabisa huo msamaha.
 
Nimeipenda lugha ya Waziri mkuu,
Pale ndio mwisho wa Mvutano.
DP- World inaenda kuleta mapinduzi ya kimkakati katika Bandari zetu.
Tujiandae kuongeza Mapato na kuwepo kwa uchache wa ajira za kwa watu waliozowea mikiki ya kufuatilia kila kitu kwa mguu na makaratasi mikononi. Hii habari kwisha , mambo yote ni dijitali tuu Wizi wa kjinga kwisha.
Badari itakuwa ni eneo shwari sana ,wataonekana wafanyakazi tuu kwenye control room na madereva wa Crane.
Sio kweli, mfumo wa kodi ndio mbovu nao ni lazima wauridhi au unataka kusema wao watakuja na sheria zao za kodi? Mfano gari lilotengenezwa miaka 10 iliyopita linalipiwa kodi milion 4 je wao watasema likipiwe milioni 2 na bidhaa nyingine imekuwa ni ya kukadiria tu baada ya kuona bidhaa usoni na shida kubwa iko hapo.
 
Msamaha unaombwa na mtu mwenye uadilifu na anaetambua wapi alipokosea...Katika maisha ni watu wachache sana wenye kijitambua hivyo usitegemee kuwa kila atake kukosea atakuomba radhi..Issue ya msingi ishi na walimwengu kwa akili mtu wangu!

Na akili ni pamoja na kuomba msamaha mkuu.
 
Hivyo basi naisihi serikali katika hili la mkataba wa bandari; ikubali kuomba radhi.
Mkifanya hivyo hamtaonekana wadhaifu, bali wakomavu sana.
Mkuu Mchokoo , kwanza nakubaliana na wewe, unapokosea, kuomba radhi sio udhaifu, lakini kwa hili la Bandari, serikali iombe radhi kwa lipi wakati mkataba bado?.

Watanzania wanapaswa kuelimishwa elimu ya mikataba, kilichopitishwa na Bunge ni IGA sio mkataba ni MoU ya makubaliano ya kuingia mkataba, mkataba ni HGA, bado haujaingiwa!.

P
 
Mkuu Pascal, wazaramo wanasema; wasiwasi ndiyo akili zenyewe.
Kwanza sina imani kwa asilimia kubwa na wanasheria wa nchi hii ukiwamo wewe hapo.
Mlisema hivihivi kwenye mikataba mibovu iliyoingiwa huko nyuma, ila bado nchi ni masikini ilihali tuna rasilimali kibao!
 
Sio kweli, mfumo wa kodi ndio mbovu nao ni lazima wauridhi au unataka kusema wao watakuja na sheria zao za kodi? Mfano gari lilotengenezwa miaka 10 iliyopita linalipiwa kodi milion 4 je wao watasema likipiwe milioni 2 na bidhaa nyingine imekuwa ni ya kukadiria tu baada ya kuona bidhaa usoni na shida kubwa iko hapo.
Inaonekana mwarabu ataweka watu wake kwa niaba ya TRA wafanye tathmini ya mzigo na kukadiria kodi kwa kasi ya kimbunga, wakimtumia binti mdogo anayeendesha makontena kwa remote, in Dr. kasheku's voice.
 
Mkuu Mchokoo , kwanza nakubaliana na wewe, unapokosea, kuomba radhi sio udhaifu, lakini kwa hili la Bandari, serikali iombe radhi kwa lipi wakati mkataba bado?.

Watanzania wanapaswa kuelimishwa elimu ya mikataba, kilichopitishwa na Bunge ni IGA sio mkataba ni MoU ya makubaliano ya kuingia mkataba, mkataba ni HGA, bado haujaingiwa!.

P
Hey! Brother P

Katika pita pita zako huku na huko umepata fununu kidogo kujua yatakayojiri ndani ya mkataba baada ya MoU ya makubaliano ya mkataba kufanyiwa uchambuzi...

Swali...
Je huo mkataba utakuwa ni wa kipindi gani haswa?
 
MoU yenye vifungu vya kutufunga, yaani hadi makubaliano yawekewe vifungu vya kuzuia makubaliano kuvunjika.......acha fix mzee.
 
Hey! Brother P

Katika pita pita zako huku na huko umepata fununu kidogo kujua yatakayojiri ndani ya mkataba baada ya MoU ya makubaliano ya mkataba kufanyiwa uchambuzi...

Swali...
Je huo mkataba utakuwa ni wa kipindi gani haswa?
Akijibu anaharibu, asipojibu anavuruga.
Kazi yake ni ngumu!
 
Eti tuombe radhi? ili baadae mje kucheka watoto wangu kama mnavyowacheka watoto wa mchonga meno wa butiama jinsi dingi yao hajawaachia kitu

acha tutengenezee vizazi vyetu maisha nafasi hii ni nadra sana kuipata hatuwezi kuichezea
 
Ndugu zangu Watanzania hakuna binadamu asiyekosea, iwe ni kwa makusudi au bahati mbaya. Kimsingi hilo ndilo hudhihirisha ubinadamu wenyewe. lngawa mara nyingi tunapogundua makosa yetu tunajaribu kutoyakubali kama ni makosa!

Au tukikubali tunaona shida sana kuomba msamaha, tukidhani kuonekana ni dhaifu, kitu ambacho siyo kweli. Kimsingi mtu anayekubali kuwa amemkosea Mungu, au wanadamu wenzake ni nguzo ya shaba katikati ya kizazi cha waoga.

Hivyo basi naisihi serikali katika hili la mkataba wa bandari; ikubali kuomba radhi. Mkifanya hivyo hamtaonekana wadhaifu, bali wakomavu sana.

Msituangushe hata wale tunaowanga mkono tangu Mungu awaweke madarakani. Kwani ukitazama kwa makini sana ni kama hili limekuja kufuta mema yote yaliyofanywa na awamu hii.

Sasa kwa nini iwe hivyo, na kwa faida ya nani?
Wakishaomba radhi mtaanza hoo waachie ngazi ,wanajua wamebugi ila wanapambana kuficha hii aibu ya millennia.
 
Back
Top Bottom