dosari
Member
- Oct 7, 2016
- 81
- 84
Sifa ya kiongozi mzuri ni nidhamu kwa wananchi anaowaongoza. Anakuwa mnyenyekevu na anawaambia ukweli wenye vipimo sahihi.
Kiongozi mzuri hupaswa kutambua kuwa watu anaowaongoza wana akili timamu, kwa hiyo hawapaswi kuongopewa.
Inapotokea kiongozi anawaambia wananchi wake jambo ambalo si la kweli, kwa kuwaheshimu, hutakiwa kurudi kwao na kuwaomba radhi.
Kuomba radhi baada ya kuwaambia wananchi jambo ambalo si la kweli, ni uungwana wa kiongozi mzuri.
Suala la dawa za kulevya kwa hatua lilipofikia na jinsi ambavyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alivyolianzisha, anapaswa kuwaomba radhi wakazi wa Dar es Salaam na Watanzania kwa jumla.
KWA NINI AOMBE RADHI?
Jibu ni rahisi. Alipotangaza kwa mara ya kwanza mapambano na kuanza kutaja majina ya watuhumiwa, tuliambiwa ni vita dhidi ya wauza dawa za kulevya.
Tulimpongeza kwa nia yake njema pamoja na ujasiri wake. Niliandika makala nikimtakia heri kwa Mungu aweze kufanikiwa na nilimuomba Mungu amlinde.
Vita dhidi ya dawa za kulevya ni ngumu na hatari sana. Ni zaidi ya vita ya Marekani na Vietnam. Ina changamoto kuliko vita ya Tanzania dhidi ya Iddi Amin Dada. Maana unapigana na vigogo wa ndani wenye kujua siri nyingi za nchi ambao huwajui ila wao wanakujua.
Pamoja na pongezi, nilimshauri aachane na njia ya kutaja majina hadharani, kwani kufanya hivyo alikuwa anawasaidia wahusika wa biashara haramu ya dawa za kulevya ama kutoroka au kupoteza ushahidi. Na bila ushahidi hakuna mashitaka.
Nilieleza kuwa utajaji wa majina kama ambavyo Makonda alivyokuwa anafanya, ulikuwa unatengeneza matokeo ya aina mbili.
Mosi; aliwadhalilisha mno wasiohusika. Maana hata baada ya kuonekana hawahusiki bado si rahisi kusafishika.
Pili; unamtuhumu mtu kuuza unga kisha unampa siku mbili za kujiandaa ndipo ajipeleke mwenyewe polisi. Hii ilikuwa ofa ya kipekee kutoka kwa Serikali kwa watuhumiwa wa dawa za kulevya.
Ni muuza unga gani aliyezubaa kiasi hicho mpaka umpate na ushahidi baada ya kumpa siku mbili za kujiandaa? Unawajua wauza unga au unawasikia?
MATOKEO YAKE
Wote waliotangazwa iliripotiwa hawakukutwa na kitu. Ghafla kesi ikahama kutoka kutuhumiwa kufanya biashara ya dawa za kulevya hadi kutumia.
Wanaotuhumiwa kufanya biashara ya dawa za kulevya, wakapelekwa kwa mkemia mkuu wa Serikali kupimwa kama wanatumia unga au la!.
Watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya, wakafikishwa mahakamani kwa tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya.
Kwa hiyo, vita ikahama kutoka ilipotangazwa mwanzoni kuwa ni mapambano na wauza unga mpaka mapambano na watumiaji. Vita dhidi ya mateja.
Sauti kubwa ambayo Makonda aliitumia kuwaaminisha Watanzania kuwa anapambana na wauza unga, haikupaswa kuishia kwa watajwa kufikishwa mahakamani kwa kutumia unga.
Kesi za dawa za kulevya hazina dhamana, kwa hiyo kama utajaji wa majina ungekuwa umefuata baada ya uchunguzi wa kutosha, angalau asilimia 50 ya waliotajwa wasingeachiwa. Kuachiwa kwao ina maana walitajwa bila ushahidi.
Iwe Makonda alifanya makosa ya kutokujua au makusudi kutangaza majina na kutoa siku mbili kwa watajwa ndipo wajitokeze polisi, anapaswa kuwaomba radhi Watanzania hususan wana Dar es Salaam.
Nguvu iliyotumika kutangaza majina, haikupaswa kuishia kwa namna ambavyo imeisha. Wengi wameachiwa bila hata kufikishwa mahakamani, waliofikishwa mahakamani ni kwa kesi ya kutumia unga na siyo kuuza. Je, muuza unga ni nani?
Mafanikio ya nguvu kubwa iliyotumika ni yapi? Makonda awaombe radhi Watanzania. Kukiri makosa na kuomba radhi ni uungwana.
Matangazo ya televisheni moja kwa moja, msisimko mkubwa uliotokea nchi nzima, gharama yake ni kubwa sana. Hayakupaswa kuisha hivi.
Makonda hakupaswa kuwaona Watanzania ni watu rahisi kiasi hiki, kwamba wanaweza kugeuzwa-geuzwa na iwe sawa tu. Watanzania wa Karne ya 21 siyo wa bei poa kiasi cha namna alivyowafanyia.
Ni lazima aombe radhi kipindi hiki ambacho vita ya dawa za kulevya inaendeshwa kitaalamu na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), chini ya ‘mtu wa kazi’, Rogers Siang’a.
SOMO LA KUTAJA MAJINA
Rais wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Kikwete, katika mwaka wake wa kwanza, alitangaza kiama na wauza unga. Aliomba apewe majina kisha ayatangaze na kuwashughulikia wahusika.
Kweli majina yaliandikwa na JK akawa na majina ya Watanzania waliotajwa kuhusika na biashara haramu ya dawa za kulevya.
Kimya kikafuata. Ahadi ya JK kutaja majina ikapotea. Watu wakahoji: "Mheshimiwa Rais, uliomba majina ya wauza unga na umepewa, sasa mbona huyatangazi kama ulivyoahidi?"
Yupo mfanyabiashara mmoja mkubwa sana hapa nchini (simtaji kwa sasa), alikerwa na ukimya wa JK. Akamfuata Ikulu.
Milango ya JK Ikulu ilikuwa wazi, yule mfanyabiashara alikaribishwa Ikulu, akakutana na JK, akamuuliza: "Mtukufu Rais mbona kimya hutaji majina ya wauza unga? Vijana wetu wanazidi kuharibika mitaani, wengine wanakufa kwa sababu ya wauza unga."
JK: "Siwezi kutaja majina bila kufanya uchunguzi, nijiridhishe kama kweli wote ni wauza unga. Inawezekana wapo wametajwa kwa chuki, wengine wametajwa bahati mbaya."
Mfanyabiashara: "Mheshimiwa Rais ungetaja tu hayo majina uliyopewa. Watanzania wanawajua wauza unga. Ukishataja angalau hii vita itakuwa nyepesi. Wauza unga wameachwa sana."
JK: "Ningetaja majina bila uchunguzi hata wewe usingefurahi."
Mfanyabiashara: "Mimi ningefurahi kabisa, kwa nini nisingefurahi?"
JK akatoa majina ya waliotajwa kuwa wauza unga. Akamwonesha mfanyabiashara huyo. Jina namba moja kwenye orodha ni la huyo mfanyabiashara aliyekuwa akisisitiza majina yatangazwe.
Mfanyabiashara huyo akashituka, akahamaki: "Na mimi nimo? Watanzania wapoje, hata mimi nimetajwa? Huo unga nauuzia wapi?"
JK akamjibu: "Ndiyo maana hatukimbilii kutaja majina bila ushahidi. Tumeshaunda kikosi kazi cha polisi kupambana na dawa za kulevya, majina haya yote wanayo. Wanapeleleza, wanaowabaini wanawakamata. Hata sasa wengine wameshaanza kukamatwa."
Kunzia hapo mfanyabiashara huyo hakuhoji tena majina ya wauza unga kutajwa.
Ndimi Luqman MALOTO