Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,674
- 218,183
Kodi ya Majengo imelipwa ndani ya nchi hii kwa miaka na miaka , kwa kipindi kirefu ililipwa kwenye Halmashauri na kuwa mapato ya Halmashauri husika ili kusaidia miradi mbali mbali , mimi mwenyewe nina nyumba 2 kwenye halmashauri ya Temeke , nafahamu ninachoandika , Jina langu linafahamika vema kabisa na Halmashauri hiyo kama wenye nyumba wengine wanavyofahamika , huku kila jengo au nyumba ikirasimishwa kwa kupewa namba Maalum na kubandikwa Ukutani ili kila mtu aone .
Baada ya uchaguzi Mkuu wa 2015 ccm kuangushwa kwa kunyang'anywa halmashauri kubwa kubwa , ikiwemo Halmashauri ya Jiji la DSM , yenye majengo mengi na yenye kulipiwa pesa nyingi , kwa roho yake Mbaya , Rais wa wakati huo Magufuli akaamua kuzinyang'anya kodi ya majengo halmashauri kwa vile sasa zilikuwa chini ya Chadema , na kuamuru wenye majengo wote nikiwemo mimi kulipia kodi hiyo kupitia TRA , rekodi zote zipo na wenye nyumba wote wapo na wanatambulika na tayari walishawekwa kwenye mfumo wa malipo ( japo baada ya uchafuzi wa 2020 kodi hii imerejeshwa tena halmashauri maana chadema hawapo tena ), sasa kuwalipisha watu wasiohusika huku wahusika wanaopaswa kulipa kodi wapo na wanafahamika ni wizi wa kishamba sana uliolenga kutunisha mfuko wa serikali kwa NJIA YA HARAMU .
Kama walipaji walishakuwa kwenye mfumo na wanafahamika , huku kila nyumba mpya inayojengwa ujenzi wake hufanywa baada ya vibali vya halmashauri , kwanini Serikali imeamua kupora pesa za raia wasiohusika ?
Itaendelea ....