Kwako ndugu yangu Maxence Melo. Ufanyaje ili uepuke kushtakiwa na Jamhuri kisa JF?

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,658
17,751
Wanabodi habari za mchana. Huu uzi nauandika ili umsaidie kaka yangu Melo!!

Mimi ni mdau wa JF kwa muda mrefu sana nimesoma nyuzi nyingi humu na zimenisaidia sana kama Mtanzania japo imenichukua muda mrefu kujiunga kutokana na changamoto mbalimbali za kimtandao!!

Kuna mdau humu anaitwa THE BOLD AU HABIBU A. ANGA nyuzi zake nyingi zipo kule Jamii Inteligence. Kwa kutumia maarifa niliyoyapata kwa kusoma uzi wake wa ROMAN ABRAMOVIC namshauri MELO afanye usajili upya wa hatimiliki ya JF kwa usajili wa mlolongo mrefu sana wa wamiliki kama kampuni vile. Kama ROMAN ABRAMOVICH alivofanya usajili wa kampuni zake za mafuta na aluminium.

Mlolongo wa wamiliki zaidi ya kampuni kama mia au mia mbili hivi itakusaidia usiwe tageti wa moja kwa moja kwenye mashtaka mbalimbali.

Kwa mfano JF inamilikiwa na Melo Enterprises chini ya umiliki wa ASAS Limited pia Mushi Company ina hisa 25% za JF. Tena SIDO ina asilimia 50 za umiliki wakati huo huo TANAPA inamiliki asilimia 90 za Mushi Company za hisa za JF, wakati The Breed Supply Enterprises inamiliki asilimia 100 za hisa za Melo Enterprises.

Yaani mlolongo wa kampuni ndani ya kampuni kama mia mbili hivi. Jamhuri ikitaka kushtaki itamshitaki nani? Melo au utitiri wa makampuni?

Nawasilisha. Karibuni kwa maboresho kama yapo tumuokoe Melo na kesi kandamizi.
 
Changamoto ya JF ipo kwenye DATA PRIVACY. Siyo kwamba JF haiwezi kumilikiwa na wengi zaidi, lakini kumbuka kila mwanahisa ni lazima atakuwa na access ya JF Jikoni.

Na Kwakuwa JF Inawindwa, hao wawindaji ndio watakaonunua HISA JF, THEN

WE'RE DOOMED !
 
Ninamini Maxence Melo alishapata ushauri huo, na alishalitafakari hilo swala na likashindikana kufanyika. Swala hilo wana JamiiForums hatuliungi mkono.

1) Akiuza hisa atapunguza nguvu yake katika kuiendesha JamiiForums (Shareholders watakua na uwezo wa kumpelekesha wanavyotaka kwenye kufanya maamuzi ya kuendesha JF).

2) Shareholders atakao wauzia shares wana uwezo wa kumgeuka, wakaziuza shares zao kwa maadui wa JamiiForums (Serikali au Vibaraka wa serikali).

3) Shareholders wanaweza wakamtoa kwenye Management ya JF kabisa, akabakia kua Director/Shareholder tu na kusubiri mgao wa faida katika kikao cha mwaka cha directors (Kwa kumpigia kura ya kumtoa katika management).

NB Wanaweza kuandika mkataba wa kuepusha hayo yasitokee pindi atakapowauzia shares, ila shareholders baada ya kununua shares za JamiiForums wanaweza kwenda mahakamani na kuomba mkataba wa kabla ya mauzo ya shares ufutwe kwa kigezo unawabana (Unfair Contract Terms).

#Zipo sababu nyingi, haina haja kupoteza muda kukuelewesha zaidi, hizo zinakutosha kutokuunga mkono ushauri wako.
 
Ugomvi uko hapo tu! Wanataka wajue Elli ni nani
wakitaka kujua ELI ni nani basi watawauliza wamiliki zaidi ya mia mbili na sio MELO peke yake!na watajibu tuna uhuru wa kulinda taarifa za wateja wetu na huu ni mtandao huru usiofungamana na upande wowote!!!MELO ATAPATA NGUVU KULIKO SASA HV ANAPAMBANA AKIWA TAGETI PEKE YAKE!!!!
 
Wanabodi habari za mchana. Huu uzi nauandika ili umsaidie kaka yangu Melo!!

Mimi ni mdau wa JF kwa muda mrefu sana nimesoma nyuzi nyingi humu na zimenisaidia sana kama Mtanzania japo imenichukua muda mrefu kujiunga kutokana na changamoto mbalimbali za kimtandao!!

Kuna mdau humu anaitwa THE BOLD AU HABIBU A. ANGA nyuzi zake nyingi zipo kule Jamii Inteligence. Kwa kutumia maarifa niliyoyapata kwa kusoma uzi wake wa ROMAN ABRAMOVIC namshauri MELO afanye usajili upya wa hatimiliki ya JF kwa usajili wa mlolongo mrefu sana wa wamiliki kama kampuni vile. Kama ROMAN ABRAMOVICH alivofanya usajili wa kampuni zake za mafuta na aluminium.

Mlolongo wa wamiliki zaidi ya kampuni kama mia au mia mbili hivi itakusaidia usiwe tageti wa moja kwa moja kwenye mashtaka mbalimbali.

Kwa mfano JF inamilikiwa na Melo Enterprises chini ya umiliki wa ASAS Limited pia Mushi Company ina hisa 25% za JF. Tena SIDO ina asilimia 50 za umiliki wakati huo huo TANAPA inamiliki asilimia 90 za Mushi Company za hisa za JF, wakati The Breed Supply Enterprises inamiliki asilimia 100 za hisa za Melo Enterprises.

Yaani mlolongo wa kampuni ndani ya kampuni kama mia mbili hivi. Jamhuri ikitaka kushtaki itamshitaki nani? Melo au utitiri wa makampuni?

Nawasilisha. Karibuni kwa maboresho kama yapo tumuokoe Melo na kesi kandamizi.

Jambo ambalo hufahamu ni kama usiku wa kiza. JF ile ya mwanzo sio ya sasa hivi, imeshanunuliwa na CHADEMA. Obviously hawawezi kukubali lakini huo ndio ukweli. JF hivi sasa imebadilika sana sio ile ya zamani kwa sababu imelalia upande moja tu wa Chadema na vyama vya upinzani. Wao ni wanufaikaji (Chadema) wa kila kinachoendelea hapa. Wengi utaona hawachangii ki-vile kwa sababu michango mingi inafyekwa hasa inayohusu maendeleo ya Watanzania. Its just a matter of time utaona kitu gani kitatokea. JF itakufa kibudu kama ilivyo Chadema. Chadema ina harufu kubwa ya ukabila na ubinafsi. JF sio huru, Max Melo ameingia kwenye mtego ambao hawezi kujinasua.
 
Ndugu yangu!mbona kuna mabandiko mengi yanahusu serekali na juhudi zake!hata leo jpm kazungumza na alichosema kipo humu tumehabarishwa!ina maana serve ya jf imejaa mabandiko ya kuinanga serekali pekee???kama ingekuwa hivyo wakina kawe Alumni,wakudadavua,faizafoxy,jinga lao,msemakweli na wengine ambao ni makomredi wasinge toa nyuzi zao wala kukomenti humu!!!!!
 
Wazo zuri ila Sidhani kama suala hapa ni nani wa kumshtaki maana hata kama Max atakuwa sio direct target,lazima kuna mtu mmoja au kadhaa watakaosimama mahakamani kwa niaba ya JF!

Wanachokitaka wao sio kumuona Max kasimama mahakamani bali kuona wanachokitaka kutoka JF wanakipata.

Sasa swali ni Je hao watakaoshtakiwa badala ya Max watatimiza matakwa ya washtaki au hawatatimiza?au watajinasua vipi na kesi.
 
wakitaka kujua ELI ni nani basi watawauliza wamiliki zaidi ya mia mbili na sio MELO peke yake!na watajibu tuna uhuru wa kulinda taarifa za wateja wetu na huu ni mtandao huru usiofungamana na upande wowote!!!MELO ATAPATA NGUVU KULIKO SASA HV ANAPAMBANA AKIWA TAGETI PEKE YAKE!!!!
Tatizo ni kwamba hao wamiliki sio wote watakua na mtazamo mmoja, unaweza kukuta mapandikizi humo humo ndani! Si unakumbuka hata baadhi ya Moderators humu ndani walifurushwa?
 
Ndugu yangu!mbona kuna mabandiko mengi yanahusu serekali na juhudi zake!hata leo jpm kazungumza na alichosema kipo humu tumehabarishwa!ina maana serve ya jf imejaa mabandiko ya kuinanga serekali pekee???kama ingekuwa hivyo wakina kawe Alumni,wakudadavua,faizafoxy,jinga lao,msemakweli na wengine ambao ni makomredi wasinge toa nyuzi zao wala kukomenti humu!!!!!

I agree, lakini ninalokwambia ndio hilo kama hukubaliani nalo ni sawa tu. I know what I am talking about. Mimi nipo hapa tangu hii Forum inaanzishwa nafahamu mengi bora niishie hapo.
 
Kila mtu aanzishe kampuni yake, hays mambo ya watu kusubiri kununua hisa kwenye kampuni za wenzao ni kuchoka kifikra.

Kama unaakili zako tafuta idea yako na isimamie, ikuze, lakini sio kuvizia vya wenzako.

Kuna mlokole anatafuta mtu amjengee kanisa, eti yeye ni muhubiri, alafu anataka amiliki 50% ya kanisa,unaweza kuona kuna watu wanadhani wanaakili sana kuliko wenzao humu duniani.

Binafsi nasema tafuta idea yako isimamishe, ikisimama na iendeleze, kama unapesa kawekeze kule DSE.

Vitisho havitaisha kwa JF kwasababu kuna watu humu wanagusa maslahi ya vyama vya siasa, hasa ccm na serikali yao, hivyo vitisho vitakuwepo tu.
 
Hata kama akisimama mtu mmoja atakuwa sio yeye pekee itakuwa makampuni mengi sana ambayo jamhuri haiwezi kuyakamata maramoja na kuyashtaki!!lazima jamhuri imtafute mmiliki mmoja ambae hayupo!!kutakuwa na ugumu kufaili kesi ya JF mahakamani na wa kumkamata kumuweka ndani!!!
 
Wanabodi habari za mchana. Huu uzi nauandika ili umsaidie kaka yangu Melo!!

Mimi ni mdau wa JF kwa muda mrefu sana nimesoma nyuzi nyingi humu na zimenisaidia sana kama Mtanzania japo imenichukua muda mrefu kujiunga kutokana na changamoto mbalimbali za kimtandao!!

Kuna mdau humu anaitwa THE BOLD AU HABIBU A. ANGA nyuzi zake nyingi zipo kule Jamii Inteligence. Kwa kutumia maarifa niliyoyapata kwa kusoma uzi wake wa ROMAN ABRAMOVIC namshauri MELO afanye usajili upya wa hatimiliki ya JF kwa usajili wa mlolongo mrefu sana wa wamiliki kama kampuni vile. Kama ROMAN ABRAMOVICH alivofanya usajili wa kampuni zake za mafuta na aluminium.

Mlolongo wa wamiliki zaidi ya kampuni kama mia au mia mbili hivi itakusaidia usiwe tageti wa moja kwa moja kwenye mashtaka mbalimbali.

Kwa mfano JF inamilikiwa na Melo Enterprises chini ya umiliki wa ASAS Limited pia Mushi Company ina hisa 25% za JF. Tena SIDO ina asilimia 50 za umiliki wakati huo huo TANAPA inamiliki asilimia 90 za Mushi Company za hisa za JF, wakati The Breed Supply Enterprises inamiliki asilimia 100 za hisa za Melo Enterprises.

Yaani mlolongo wa kampuni ndani ya kampuni kama mia mbili hivi. Jamhuri ikitaka kushtaki itamshitaki nani? Melo au utitiri wa makampuni?

Nawasilisha. Karibuni kwa maboresho kama yapo tumuokoe Melo na kesi kandamizi.
Acha kudanganya imejiunga na JF tarehe 29 October 2019 leo ni siku ya 37 tangu ajiunge.
 
Jambo ambalo hufahamu ni kama usiku wa kiza. JF ile ya mwanzo sio ya sasa hivi, imeshanunuliwa na CHADEMA. Obviously hawawezi kukubali lakini huo ndio ukweli. JF hivi sasa imebadilika sana sio ile ya zamani kwa sababu imelalia upande moja tu wa Chadema na vyama vya upinzani. Wao ni wanufaikaji (Chadema) wa kila kinachoendelea hapa. Wengi utaona hawachangii ki-vile kwa sababu michango mingi inafyekwa hasa inayohusu maendeleo ya Watanzania. Its just a matter of time utaona kitu gani kitatokea. JF itakufa kibudu kama ilivyo Chadema. Chadema ina harufu kubwa ya ukabila na ubinafsi. JF sio huru, Max Melo ameingia kwenye mtego ambao hawezi kujinasua.

Anzisheni inayolalia ccm, vyombo vyote vya habari sasa hivi vinamsifia Magufuli na ccm lakini vinalia hali ni ngumu. Kama hili jukwaa ni la cdm ww umefuata nini humu ndani? Mmezoea media zinazowahofia hivyo mnalisha habari za upande mmoja. Humu jf mnakutana na ukweli unawaumiza. Hata mkiifunga jf kwa hila, bado platform ni nyingi za kutoa maoni yetu huru.
 
Nanye GO! hakuna kishoka hapa!!toa mchango wa nn kifanyike ili kumsaidia!!we huoni jamaa anavo hustle mahakamani kila siku?NJOO NA IDEA jf sio siasa pekee za vyama kuna forum mbali mbali !!!!JIKITE KWENYE MADA SIO KUSHAMBULIA!!!WAZO BAYA HUSHINDWA NA WAZO BORA ZAIDI!!!
 
Anzisheni inayolalia ccm, vyombo vyote vya habari sasa hivi vinamsifia Magufuli na ccm lakini vinalia hali ni ngumu. Kama hili jukwaa ni la cdm ww umefuata nini humu ndani? Mmezoea media zinazowahofia hivyo mnalisha habari za upande mmoja. Humu jf mnakutana na ukweli unawaumiza. Hata mkiifunga jf kwa hila, bado platform ni nyingi za kutoa maoni yetu huru.

Mkuu labda hufahamu au kwa makusudi kabisa unataka kupotosha. JF ni sisi tuliyoipigania iwe hewani na sio kwa kulalia upande wowote ule. Ask Max, wewe unadandia treni wakati imeondoka? Endeleeni kumdanganya Max na kumtumia laana yenu haitaondoka milele.
 
BREED wewe ni Jasusi mmeona mmeshindwa kupata privacy mlizotaka ili nianze kuwateka wahusika unakuja na wazo la KUIBINAGSISHA JF koma.
Hata kama akisimama mtu mmoja atakuwa sio yeye pekee itakuwa makampuni mengi sana ambayo jamhuri haiwezi kuyakamata maramoja na kuyashtaki!!lazima jamhuri imtafute mmiliki mmoja ambae hayupo!!kutakuwa na ugumu kufaili kesi ya JF mahakamani na wa kumkamata kumuweka ndani!!!
 
Wadau Juzi tu hapa!MELO alienda kupokea Tuzo kule kwa trumph sasa ni bora akawasiliana na kile chama cha waandishi duniani wakamshauri namna ya kufanya ili afanye mchakato wa umiliki ambao ni salama sana kwake kiuchumi na kiusalama!!!
 
Back
Top Bottom