NAMBA MOJA AJAYE NCHINI
JF-Expert Member
- Oct 29, 2019
- 8,796
- 18,063
Wanabodi habari za mchana. Huu uzi nauandika ili umsaidie kaka yangu Melo!!
Mimi ni mdau wa JF kwa muda mrefu sana nimesoma nyuzi nyingi humu na zimenisaidia sana kama Mtanzania japo imenichukua muda mrefu kujiunga kutokana na changamoto mbalimbali za kimtandao!!
Kuna mdau humu anaitwa THE BOLD AU HABIBU A. ANGA nyuzi zake nyingi zipo kule Jamii Inteligence. Kwa kutumia maarifa niliyoyapata kwa kusoma uzi wake wa ROMAN ABRAMOVIC namshauri MELO afanye usajili upya wa hatimiliki ya JF kwa usajili wa mlolongo mrefu sana wa wamiliki kama kampuni vile. Kama ROMAN ABRAMOVICH alivofanya usajili wa kampuni zake za mafuta na aluminium.
Mlolongo wa wamiliki zaidi ya kampuni kama mia au mia mbili hivi itakusaidia usiwe tageti wa moja kwa moja kwenye mashtaka mbalimbali.
Kwa mfano JF inamilikiwa na Melo Enterprises chini ya umiliki wa ASAS Limited pia Mushi Company ina hisa 25% za JF. Tena SIDO ina asilimia 50 za umiliki wakati huo huo TANAPA inamiliki asilimia 90 za Mushi Company za hisa za JF, wakati The Breed Supply Enterprises inamiliki asilimia 100 za hisa za Melo Enterprises.
Yaani mlolongo wa kampuni ndani ya kampuni kama mia mbili hivi. Jamhuri ikitaka kushtaki itamshitaki nani? Melo au utitiri wa makampuni?
Nawasilisha. Karibuni kwa maboresho kama yapo tumuokoe Melo na kesi kandamizi.