ERoni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2013
- 52,564
- 119,621
Poleni na majukumu wazee watarajiwa.
Kuna nyakati mtu unakaa na kuyatafakari maisha, ni juzi tu tulikuwa vijana, tunaenda huku na kule maisha safi. Leo hii tupo kwenye umri ambao tayari ni wazee, can you imagine?
Sasa tuwekane sawa namna ya kuishi ili kuufikia uzee wa umri, huenda kuna baadhi yetu hawataki kuzeeka(kufika 80s au 90s).
●Namna gani mtu ujilinde kwenye vyakula? Wote tunajua watu wanavyokula siku hizi.
●Vipi kuhusu miendeno ya kila siku, kuna mambo ya kubadilisha?.
● Wale tunaopenda dogodogo, tuache kabisa au tupunguze?
●Vipi kuhusu kujilinda kiuchumi, wengi wetu hata hatujajipata vizuri, bado nanga inapaa, tufanyeje ili uzee wetu uwe angalau unaeleweka. Mambo ya kufikiri kusaidiwa na watoto yameisha mda sana, nini cha kufanya?
●Wengine bado tunaendelea kutafuta watoto, je tuendelee au kuna namna umri huu sasa hizo mambo tuwaachie walioko 20s, 30s na early 40s? Unastaafu na first born yupo class seven, is it worth it?
Mambo ni mengi sana ila mimi nawatakia mianzo mizuri ya utu uzima na uzee wenu!
