Kwa wazazi: hii kitu inamsaidia nini mtoto?

Ni kweli mkuu hii ipo sana tu . Nakumbuka wakati flani mama mmoja mwanae aliugua basi alipomfikisha kituo cha afya dr akaiona hiyo kamba nyeusi akamwambia mzazi arudi tu nyumbani kwani mtoto tayari ana dawa haitaji dawa nyingine. Ilibidi mama yule amvue mwanae hiyo kamba na ndipo alipopatiwa matibabu. Wazazi inapasa tubadilike hii kitu haina nguvu


Naomba namba ya simu ya huyo DR. kwa kweli anastahili sifa sana. Hizi imani zingine hizi, yaani mtoto anazaliwa basi mzazi tayari unatokwa na povu kuwa mtoto atakuwa shetani ama jini hivyo lazima avalishwe kitanzi cha mkononi.
 
Naomba namba ya simu ya huyo DR. kwa kweli anastahili sifa sana. Hizi imani zingine hizi, yaani mtoto anazaliwa basi mzazi tayari unatokwa na povu kuwa mtoto atakuwa shetani ama jini hivyo lazima avalishwe kitanzi cha mkononi.
Hahahahaha baadhi ya wazazi bwana we acha tu, waniita hii saa yaani wana imani za ajabu sana. Ni siku nyingi mkuu hata namba yake sina, mpe tu hongera kwa imani.
 
Naomba kuuliza kwa wale wenye watoto.
angalia picha hapo chini.
Mkono wa huyo mtoto amevalishwa kamba nyeusi.
Nimewaona watoto wengi hasa uswahilini huvishwa hiyo kitu.
Ni urembo kwa mtoto au hiyo kitu inamaana gani kwa mtoto?
NB: Pichani ni msanii wa bongo fleva na producer maarufu, Bob Junior akiwa na familia yake.
Hapo ilikuwa katika hafla ya kufuturu. ni hafla ya kiimani zaidi.
attachment.php

Ni ujinga wa kutokukujiamini sisi waafrika na kuamini sina tulivyokaririshwa!hapo msaada utoke wapi??alafu hayo yanaonekana sana uswahilini tu.
 
Hahahahaha baadhi ya wazazi bwana we acha tu, waniita hii saa yaani wana imani za ajabu sana. Ni siku nyingi mkuu hata namba yake sina, mpe tu hongera kwa imani.


Haya nimekusikia ila nawe pia unastahili hongera kwa kutoa point iliyoenda shule. I like wise women, keep it up.
 
Haya mambo ya uswahilini sana ambapo kila kukicha story za uchawi zinasikika.
Unalala na nguo unaamka uchi. Unalala kitandani unaamka sakafuni.
Sayansi kitaa

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hiyo tabia ipo sana Tanga. Kuna shemeji yetu mmoja alikuja na mtoto wake akiwa amemfunga kitambaa cheusi mkononi na kiunoni, tulivikata na kuvichoma tulimwambia akirudi tanga ndipo amfunge tena. Sijajua ni kwanini japo hata yeye alidai hajui ila mama yake ndiye anayejua.
 
Sisi tulio kulia uswazwi tumekutana na hivyo vitu na bado watu wengi bado wana practise sana! hicho kikamba cheusi kwenye mkono wa mtoto wa Bob Junior kinaendana sana na imani, hailezeki kuwa ni imani ya nini maana yeye mwenyewe na mkewe ndio wanajua zaidi, mimi nilisha muuliza mdada mmoja ambaye alikuwa amemfunga mwanayea akasema kinacho fungwa kwenye kikamba cheusi kwenye mkono wa mtoto ni kitovu chake ambacho hukatika siku kadhaa mara baada ya kuzaliwa.

akasema kuwa wanaamini kuwa mtoto akifungwa kitovu chake huwa haoti ndoto mbaya wala kulia lia usiku, na wanapenda kufunga kwa kamba nyeusi kwa sababu kamba nyeusi inaicha uchafu tofauti na kutumia kamba nyeupe ambayo huonyesha uchafu kirahisi.

hizi zote ni imani tu ambazo hazielezeki kirahisi, ni sawa na wale wanao vaa shanga shingoni halafu wanaziita culture.
 
Naomba kuuliza kwa wale wenye watoto.
angalia picha hapo chini.
Mkono wa huyo mtoto amevalishwa kamba nyeusi.
Nimewaona watoto wengi hasa uswahilini huvishwa hiyo kitu.
Ni urembo kwa mtoto au hiyo kitu inamaana gani kwa mtoto?
NB: Pichani ni msanii wa bongo fleva na producer maarufu, Bob Junior akiwa na familia yake.
Hapo ilikuwa katika hafla ya kufuturu. ni hafla ya kiimani zaidi.
attachment.php

Hiyo ni hirizi
 
Usaidia mtoto kuacha kushtuka,mashetani hiyo inaitwa mvuje

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Woote mnaosema hapo mliishavaa,sasa mgeuliza wazee walikuwa na maana gani.

Na utakuta hapa wengine kwa waganga wa kienyeji ndio kwao.
Hivi hapa nani hajawahi kwenda kwa mganga wa kienyeji na kwanini asiende Hospital.

Mle kwenye kitambaa kunakuwa kunafungwa Mvuje,na ule mvuje humsaidia mtoto asiweze kustukastuka na pia kukumbwa na mapepo ya njiani.Mbali na yote pia huwa na dua mbalimbali.
Na inaonekana upeo wa watu kwenye maandiko hata ya vitabu hapa ni mdogo sana.Haya mambo yapo tangu wakati wa mitume wote.

Unajua wengine tukifika mjini ndio tunaona kila kitu,ila tukianza kuumwa tu haoo vijijini.


Mie nipo Tofauti na nyie,kwamba naamini baathi ya mambo huwa ni sahihi na sio kila kitu kubeza.
Hapa mkulizwa faida ya Shanga kiunoni kwa mwanamke wooote mtajibu kwa jibu moja tu linalofana na moja kwa moja kwenye Ngono,maana ndio our first impression in mind.Wakati in deep kuna vitu vingi ndani yake.

neno hilo,ukitaka meza usipoweza tafuna.

kwenye shanga umenena. Watu wanajidanganya eti urembo hawajui nyuma ya pazia kuna nini
 
nahisi ni uchafu alaf huwa naogopa ati!

Kama huamini uchawi au ushirikina kwa nini uogope?

Labda useme wewe pia ni muumini wake, ila hu- practice wazi tu

Vinginevyo hamna sababu ya kuogopa
 
Tuachane na imani za kijinga karne ya 21. Hivi mtoto wa mwezi 1,2,3 ana akili ya kutambua vitu vibaya kwa kuona na huo uwezo wa kuona hivyo vitu kisayansi inaelezeka? Mimi nina watoto 4 wa mwisho ana 3 yrs na sijawahi funga hicho kitambaa. Mtoto kulia ni kawaida na inasababishwa na vitu vingi lakini zaidi ni kuumwa tumbo, masikio, joto n.k
 
Back
Top Bottom