Kikwetu wanasema kuwa mtoto anaona kila kitu ambacho sisi watu wazima hatuwezi kiviona, mfano mtoto ni rahisi kumuona mchawi na mwanga ndiyo maana mtoto anaweza akastuka akalia sana usijue analilia nini kumbe ameona vitu vya kumuogopesha.So wataalam wanasema kuwa mtoto akifungwa kitu cheusi mkononi ama mguuni hawezi tena kuona vitu vya kutisha, kuna wengine wananawawekea jani utosini.Naomba kuuliza kwa wale wenye watoto.
angalia picha hapo chini.
Mkono wa huyo mtoto amevalishwa kamba nyeusi.
Nimewaona watoto wengi hasa uswahilini huvishwa hiyo kitu.
Ni urembo kwa mtoto au hiyo kitu inamaana gani kwa mtoto?
NB: Pichani ni msanii wa bongo fleva na producer maarufu, Bob Junior akiwa na familia yake.
Hapo ilikuwa katika hafla ya kufuturu. ni hafla ya kiimani zaidi.
Wanga tu! Tena mi nkiona mtoto kavalishwa hayo madude hata awe mzuri vp simbebi wala kumshika ng'o!
Kikwetu wanasema kuwa mtoto anaona kila kitu ambacho sisi watu wazima hatuwezi kiviona, mfano mtoto ni rahisi kumuona mchawi na mwanga ndiyo maana mtoto anaweza akastuka akalia sana usijue analilia nini kumbe ameona vitu vya kumuogopesha.So wataalam wanasema kuwa mtoto akifungwa kitu cheusi mkononi ama mguuni hawezi tena kuona vitu vya kutisha, kuna wengine wananawawekea jani utosini.
Kuna siku moja nilikuwa nasafiri na basi kutokea Tarime kwenda Mwanza, tulipofika Msoma akapanda babu mmoja kwenye basi, hapo hapo mtoto mmoja kama wa miezi 2 akaanza kulia sana.Mama yake alibembeleza sana lakini wapi,basi jamaa mmoja kwenye gari akamwambia kuwa mtoto anatakiwa afungwe kitambaa cheusi mkononi eti kwa kuwa ameona kitu kisicho cha kawaida lakini yule mama akagoma.Tulipofika maeneo ya Lamadi yule mzee akashuka na hapo hapo mtoto akanyamaza,basi kuna mama mmoja akasema kuwa yule babu aliepandia Musoma alikuwa mganga wa kienyeji so ndiyo maana mtoto alilia sana maana kuna vitu unusual ameviona.Kwa hiyo kwa kifupi kufunga kitambaa cheusi ni imani inayoendana na kumlinda mtoto asione mambo ya kutisha
Jamani Imani za watu tusiziingilie kwani kuna vitu vingi tu tunavifanya na watoto wetu wanapona.Hiyo inakutambulisha imani, upeo wa kiakili pamoja na level ya elimu ya hao wazazi wa wenye watoto wa namna hiyo.
Wa kikee wa kiume?Mi wangu hawakuvaa na wapo fit
Nikianza na imani, imani yao haba hasa kwa kuamini Mungu aliyemleta huyo mtoto hapa duniani hana uwezo wa kumkuza na kumlinda. Sasa moja kwa moja wanaamua kuwa na imani kwa miungu ya kisanamu.Kwahiyo mkuu upeo wa hao wazaazi unauelezea vp? wapo katika kundi gani?