Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

daebak, muda huu ndio nimemaliza kuingalia hii drama episode mbili za wiki hii (mpira wa ulaya nimeusamehe kwa siku ya leo). zimebaki episode 4 ili hii drama imalizike na sijajua kama kutakuwepo na uwezekano wa seson 2 japokuwa ningelipenda uwepo muendelezo wake kwa sababu nahisi stori ndio kwanza inachangamka, binafsi nimezoea episode 16 zenye kubeba wastani wa dakika 70 - 90 kupitia tvN tofauti na hiki kituko wanachotufanyia SBS cha kutuonuyesha lisali moja lilisilotimia kwa kila episode kana kwamba hii drama imebeba episode 20.

jessica lee ni mwanadada ambaye ana uwezo wa kusurvive kwenye hali yoyote ya hatari haijalishi anapambana na simba akiwa peke yake ndani ya chumba kisichokuwa na mlango, harakati zake kama lobbyist za kuhakikisha kampuni yake inajiweka ukaribu na wenye nguvu kubwa za kuwaongoza walalahoi zinanikumbusha drama ya lobbyist ambapo alikuwemo mwanadada lobbyist anayekwenda kwa jina la Maria ambaye na yeye hakuona tabu kuutumia mwili wake kama chambo kwa lengo la kuu la kumteka mteja wake kifikra na kimaamuzi.

Ameshinda dili la kusupply ndege za kijeshi lakini bado anainyemelea tenda ya mafuta ambayo waziri mkuu amemwambia raisi tayari anaye partner hivyo basi haitokuwa jambo rahisi kumuingiza jessica lee kwenye project ya mafuta.

je huyo partner aliyemlenga waziri mkuu ni nani?
nina wasiwasi huenda partner akawa ni Edward Park na kampuni yake ya dynamic ambayo pia ni kampuni pinzani, hivyo basi kuna uwezekano waziri mkuu naye ana upande wake anaoshirikiana nao kama ilivyo kwa bwana Yun aliyejiweka karibu na jessica.

halafu kuna issue ya slush fund: hii serikali yote hakuna aliyemsafi kuanzia raisi mwenyewe hadi muajiriwa anayesafisha choo cha raisi wote ni baba mmoja na mma mmoja. Nje ya drama serikali kama hizi zimejaa zaidi ndani ya bara letu la afrika ndio maana vita ya ufisadi na uwajibikaji inaendelea kuwa ni ngumu haijalishi teknolojia ya sasa imepevuka na sababu kubwa ni kukosekana kwa uwazi hususani juu ya matumizi ya serikali, mara nyingi mafisadi na madikteta hujificha kwenye mwamvuli wa kuwapambania wananchi ili wapate stahiki zao na wakati huo huo kwenye nafsi zao wakiongozwa zaidi na ubaya wa kutamani kupora kila kilicho mbele yao.

inaonekana dhahiri secretary Yun ndiye engine kuu ya muheshimiwa raisi kwenye mission zote chafu zinazomuhusu muheshimiwa aliyejificha kwenye kivuli cha utakatifu, kinachokwenda kutokezea baadae ni watatu hao kusalitiana hapo mbeleni kama itatokezea kuvuja kwa siri ya kuwepo kwa mlolongo wa rushwa kwenye dili la kununua ndege za kivita.

mpaka sasa mtu pekee mwenye uhakika wa kusurvive kwenye hili pambano licha ya kuwa naye ni mchafu wa matendo na si mwengine ni waziri mkuu kwa sababu ana ushahidi mwingi sana unaomuhusu muheshimiwa raisi pamoja na waziri wa ulinzi (tukumbuke mwanzoni drama waziri wa ulinzi alihongwa rushwa tofauti na bi jessica ikiwemo rushwa ya ngono na picha zilimfikia muheshimiwa raisi)

heshima kwake bwana judge kwa kuchelewesha kesi licha ya kupokea oda ya kuimaliza kesi ile kutoka chief justice ambaye alikwisha pokea amri kutoka kwa muhimili mchafu (jessica na crew yake)

kama raisi ndiye bingwa wa kupokea rushwa kutoka kwa matajiri unadhani rushwa hii itaweza kuondoshwa kwa mikono yake hususani kwa kuwatishia vyanzo hivi vya chini vya utumishi vinavyoendelea kupokea mshahara wa chini baada ya makato na kodi?

rushwa haiwezi kuondolewa kwa rushwa.
ufisadi hauwezi kuondolewa na mfumo fisadi.
ni sawa na mtengenezaji pombe kuweka tangazo la kukataza ummah uliopotea kunywa pombe.


dah! kadri ninavyomuona my love from joseon hwang bo ra moyo wangu unakatika vipande vipande kama samaki. Wengine wanajileta kwangu nakuniambia kwa nini usinipende mimi daemusin matokeo yake nabaki kuwajibu.


kama wewe kama wewe upendwe nini ?
siwaumbo si wa nywele si wa ghuyuni,
mbele zero nyuma hakujulikani
baraka ya wanja, kujipakaza machoni
kwenye visura wewe huko hisabuni
Zunguka bongo waone kila mahala
figure zao za kupigiwa mfano
sio zumbukuku na shepu ya penseli
hivyo unadhani kwa yakini watakiwa kwa uzuri gani hasa wa kujizuzua

sibasi tu sibasi tu sibasi tu


View attachment 1246653

next: my country drama ndipo nilale.
sitaki niamke kesho nikiwa na fikra za kuangalia korean drama haijalishi ni kwa nusu saa.
Hii drama kila sehemu inasifiwa.
Screenshot_20191028-145656.png
 
Hata maelezo sijasoma maana sio zangu hizi
upcoming drama: VIP
Release Date:
October 28, 2019 (kesho)
Runtime: Monday & Tuesday
Episodes: 16

Na Jung-Sun (Jang Na-Ra) works for a team that deals with VIP customers of a department store. She is married to Park Sung-Joon (Lee Sang-Yoon), who works on the same team. The couple faces an unexpected case, which causes their lives to fall apart.

dondoo fupi kupitia press conference iliofanyika siku mbili zilizopita​

PD (producing director) Lee Jung Rim amezungumza kwa ufupi :
ni stori inayojaribu kuangaza maisha ya kila siku wanayoyapitia wanandoa ikiwemo furaha, huzuni, dhiki yanaunganishwa na siri zilizofichwa ndani ya nafsi zao. kuna mambo mengi ya kushangaza mutakayoyashuhudia kwa kila episode ya drama hii. Kwa mara ya kwanza muandishi alipokuwa akifanya uchunguzi wake alishindwa au hakufikiria kudesign timu itakayohusika kuwahudumia wateja maalumu (VIP), mara nyingi tumezoea kushuhudia marketing team ndiyo inayohusika na shughuli zote za kuuza au kuwahudumia wateja, lakini kiupande wetu tuliona itakuwa ni jambo zuri zaidi kiubunifu kama tutaswitch (kubadilika kifikra) kutoka marketing team hadi kutengeneza department store itakayohusika na utoaji huduma kwa wateja maalumu (VIP).


Jang Nara
mahusiano yake ya ndoa pamoja na mume wake yalianza kubadilika baada ya kupokea ujumbe wa kushangaza na kutia khofu ndani yake unaomuhusu mume wake. Tulipokuwa tunaigiza hii drama haijawahi kutokezea hata mara moja muigizaji mwenzangu ambaye ni Lee Sang Yoon kunifanyia jambo lolote baya ambalo lingenipelekea nisijisikie kuwa na furaha na amani ndani ya kiwiliwili changu (uncomfortable). Nimeamua kushiirki ndani ya drama hii kwa lengo la kuonyesha pande zote mbili kwa usahihi zinazomuhusu na jung sun.

Lee Sang Yoon

baada ya kukaa sote kwa pamoja waigizaji na kujadili the acting style (sijapata neno sahihi la kiswahili) itakayotumika kupitia drama hii nimegundua mambo mengi sana yenye kufanana kati yetu, ni jambo la faraja sana kufanya kazi na kundi la watu munaoelewana kimtazamo.
View attachment 1246318

baada ya miezi takribani minne kupita hatimaye kituo cha SBS wanarudisha tena drama kwa siku ya jumatatu na jumanne.

nina miezi miwili na nusu sijaangalia drama za jumatatu na jumanne hivyo basi huenda hii ikanirudisha tena kwenye ulimwengu wa blue monday,
jang nara pamoja na lee sang yoon ni waigizaji wenye nguvu sana kwenye huu ulimwengu wa sanaa nchini korea ila nguvu pekee ya muigizaji bila ya kuwepo mazingira bora ya kikazi yanayoambatana na good scripting hayawezi kuifanya drama iwe na mafanikio hata kwa njia ya miujiza.

Natumai stori yake itakuwa ni moto zaidi ya mgahawa wa camellia a.k.a dongbaek

View attachment 1246319
 
Kuna series inaitwa kill me,heal me ni noma ni ya 2019 inahusu jamaa mmoja ambaye ana tatizo la kuingiliwa na nafsi mbaya asipopata dawa ya kutoingiliwa na nafsi anageuka kuwa katili na anafanya mambo mabaya baada ya tu nafsi kutoka anarudi kuwa normal na hali yake ya kawaida ya kuwa mpole na anapoteza kumbukumbu ya kitu gani alichofanya.kuna wakati anashangaa anavamiwa na watu anapigwa bila kujua kwanini watu wanampiga kumbe anashindwa kujua aliingiliwa na nafsi ilisababisha kuwapiga hao watu kwa kutumia mwili wake
Kill Me, Heal Me

Hii Drama niliitazama kipindi fulani hivi na niliipenda kiukweli na kinachonivutia zaidi ni jinsi ambavyo walivyojaribu kutuonesha kwa jinsi gani huu ugonjwa wa Multiple Personalities ama Dissociative Identity Disorder (DID) ulivyo na unavyoweza kumuathiri binadamu pale ambapo anapojaribu kuyakabili mawazo mabaya ya zamani hususani kipindi cha utoto akilini mwake hatimaye kupelekea kuzalishwa kwa nafsi nyingine.

Wikipedia
Dissociative identity disorder (DID), previously known as multiple personality disorder (MPD), is a mental illness characterized by at least two distinct and relatively enduring personality states. This is accompanied by memory gaps beyond what would be explained by ordinary forgetfulness.


Unaweza usiamini lakini hili tatizo ni la ajabu sana na ni ngumu sana kulitibia ama kumrudisha mgonjwa katika hali yake ya kawaida aliyokuwa nayo kabla ya kuupata huu ugonjwa.

Katika Kill Me, Heal Me nakumbuka matatizo aliyoyapata Cha Do-Hyun (Ji Sung) wakati wa utoto ndiyo yalipelekea kuzalishwa kwa nafsi nyingine kadhaa ndani yake na kila nafsi ilikuja na jina lake, tabia zake, faida na hasara zake.

Kuna wakati nafsi moja wapo inapochukua 'usukani' na kuuendesha mwili unaweza ukafanya mambo makubwa sana yenye faida lukuki kitu ambacho kwa nafsi ya kawaida ya muhusika asingeweza kufanya mambo makubwa kama hayo. Hebu pata picha mtu ana huu ugonjwa wa DID alafu ndani yake ana nafsi mojawapo yenye tabia za Bill Gates hahaha! Just Kidding!

Hii Project ya Kill Me, Heal Me ilikuwa ichezwe na Lee Sung-Ki kama muhusika mkuu ama Cha Do-Hyun lakini haikuwezekana kutokana na 'Ubize' kwenye Projects nyingine na hatimaye ikachukuliwa na Ji Sung. Ila Ji Sung ameicheza vizuri hii Character kiukweli ama wengine mliopata kuitazama hii Drama sijui mnaonaje? Je Le Sung-Ki angeongeza kitu cha ziada zaidi kuliko Ji Sung?
 
Nina wiki mbilii zimesalia kabla ya kuanza kuwa busy kwahiyo Huu muda wacha niutumie vizuri, najua nikishaanza kuwa busy huenda kwa wiki nikatazama ep. 3 - 5.
Ila kwa kawaida Episode 2 -4 huwa zinanitosha.
Lakini tangu Oktoba imeanza kwa siku ni Episode 5-7.
Huu 'Ubize' nao umeanza kushika kasi kama 'Upepo wa Kisulisuli'.

Umepelekea mpaka wengine tumejipa 'Suspension' ya kilazima ya kutotazama Drama hata hiyo Episode moja inakubidi upige mahesabu ya kaupenyo ka muda kwa kutumia zana kama Scientific Calculator bila kusahau Four Figure.
 
VAGABOND Hii Kitu, Korean Entertainment Ahsante. Stori Tamu Inasisimua Kila Scene Haipiti Bure,
Ina Mtiririko Mzuri Hakuna Nguo Za Ndani Wazi Mule Ndani Wala Mwili Wazi, Hakuna Viungo Vya Wakike Wazi Mule Ndani Na Bado Inakufanya Uhitaji Kuingilia Kila Inapotoka.

Wametengeneza Kitu Kiutamaduni Wao Na Bado Kinavutia.

Tanzania Yangu Tunakosea Wapi!?!
"Tanzania Yangu Tunakosea Wapi?"

Hilo ni swali pengine 'Gumu' sana na labda itahitajika kuwakusanya Maprofesa kama 700 hivi wafanye Discussion ili watupe jibu la pamoja la swali hilo.

Ila kiukweli inafurahisha sana na inatia hamasa kutazama kitu cha kiasili kutoka mahali fulani ambacho ndiyo utamaduni wao wa kiasili na si ule wa kuletwa na 'Upepo wa Kisulisuli'.
 
Nahitaji mnitajie season kali kuzidi six flying dragon
Mzitoe
Greet queen, empress ki na flower in prison.
Sawa, Hebu jaribu hii inayoitwa; Cruel Palace: War Of Flowers.

Hiyo ni Historical na humo ndani kuna vita kali sana 'Mjengoni' kati ya wanawake wa Mfalme Injo wa Joseon. Hiyo vita kali nadhani ndiyo imepelekea kwa Drama hiyo kupewa jina hilo.

Vita hiyo kali inaongozwa na Royal Concubine Soyong Jo ambaye anatumia kila jitihada ili kumuweka mwanaye katika kiti cha Ufalme. Sasa, ili kufanya hivyo inambidi amsafishie njia na hapo sasa analazimika kufanya mauaji kwa wale wote anaowahisi ni kikwazo kwa mwanaye kukifikia kiti hicho cha Ufalme.

Itafute.
 
Once again MB zangu zimepotea

Hii Golden garden ilitakiwa iwe na episode 16 tu zikizidi sana 20 sio mpaka 60 huko wakati hata haina mwanga mzuri,story mbovu

When the camellia blooms ipo slow inafaa muda ambao upo eneo lisilo na network porin huko umeboreka weee halafu movie unayo hio hio moja.

Empress KI nzuri ila ilifaa ipunguzwe episode basi tu enzi hizo ilikua mwendo wa episode nyingi
 
Once again MB zangu zimepotea

Hii Golden garden ilitakiwa iwe na episode 16 tu zikizidi sana 20 sio mpaka 60 huko wakati hata haina mwanga mzuri,story mbovu

When the camellia blooms ipo slow inafaa muda ambao upo eneo lisilo na network porin huko umeboreka weee halafu movie unayo hio hio moja.

Empress KI nzuri ila ilifaa ipunguzwe episode basi tu enzi hizo ilikua mwendo wa episode nyingi
Miye namisi drama zenye Episode nyingi.

Wivu ndo unanisumbua au Nina fikra zenye makengeza why hiyo Drama ya Empress Ki karibia kila mtu anaisifu, halafu miye naiona kama Historical Drama mbovu kuliko zote nilizowahi kuziona. SIJUI.
 
Back
Top Bottom