Biashara ya Korean Dramas. Jinsi Korea inavyouza Maudhui Yake Duniani

Krikichino

JF-Expert Member
Oct 5, 2019
651
1,098
Habari zenu wakuu.

Kuna swali nilikuwa najiuliza mara kwa mara hasa nikiona CD za Kikorea zinauzwa kama nyanya mtaani. Nikawa najiuliza hivi wakorea wanapata vipi faida kwenye series zao? Maana wanatoa vitu vikali alafu wanaofaidi ni watu wengine kabisa, kitu ambacho sio kibaya ila nikapatwa na hari ya kujua jinsi wakorea wanavyopata mipunga.

Ikabidi nianze kufanya uchunguzi ya jinsi ambavyo soko la series huko Korea linafanya kazi na jinsi ambavyo watayarishaji wa series hizo kama SBS, MBC na KBS wanapata faida.

Sasa kibongo bongo taasisi iliyofanya watanzania tuanze kufuatilia Korean Dramas ni ITV baada ya kuanza kuonesha series kama JEWEL IN THE PALACE (2007), JUMONG (2010), KINGDOM OF THE WIND, GREAT QUEEN SEONDOK, IRIS (2014) na nyinginezo.

Of course kuna matangazo yanakuwepo kwenye series, product placement na, streaming ndio zinafanya series za kikorea zipate faida lakini kuna njia moja ambayo ilinigusa zaidi nayo ni DRAMA EXPORTATION.

Kwenye Drama Exportation ndio sehemu wakorea wanapiga mipunga sana ambapo kuna vituo vya TV kutokea nchi nyingine za Asia kama China, Taiwan, HongKong, Philipines na Thailand huwa wananunua copy rights za kuonesha korean dramas kwenye nchi zao.

Fuji TV kwa mfano ilinunua copyrights ya kuonesha series ya Jumong nchini Japan.
Sasa kulingana na senior marketing manager wa MBC bwana Haewon Chin mwaka 2006 anasema Korean dramas zinauzwa kuanzia USD 1,000 kwa episode moja na kwa zile dramas zilizofanya vizuri kama "JUMONG" au "MAN FROM ANOTHER STAR" zinaweza zikauzwa mpaka dollar 20,000 PER EPISODE.

Bei hiyo inatokana na nchi. Kwa nchi kama Hongkong na Taiwan ambazo uchumi wake ni mkubwa vituo vya TV vinatozwa bei kubwa ukilinganisha na nchi kama Tanzania ambayo ina uwezo mdogo kiuchumi.

Sasa tuchukulie drama kama VAGABOND ambayo ilikuwa ni Hit duniani kote na ilikuwa na episode 20 hivyo, kama episode moja kwa wastani iliuzwa kwa USD 5,000 maana yake ni kwamba bei ya Vagabond kwa ujumla iliuzwa kwa dollar 100,000. Hiyo ni kwa kituo kimoja tukumbuke series inauzwa kwa zaidi vituo 20.

Na hapa tunaongelea Vagabond iliyouzwa kwenye zaidi ya vituo vya TV 30 duniani kote maana yake ni kwamba SBS ilipata faida kubwa sana kwenye mauzo pekee na hapo hujaweka faida ya Ads na Streaming kama vyanzo vingine vya mapato.

Sasa unaweza ukajiuliza mbona
bei ni kubwa sana?

Lakini in reality tukumbuke kuwa hizi drama haziuzwi kwa watu binafsi ni makampuni makubwa kutoka nchi kubwa ndio yananunua sana hizi series hivyo si kitu cha kushangaza kukuta kituo cha TV kutumia USD 100,000 kununua korean drama ili kuvutia watazamaji.

Pia ukilinganisha Korea na nchi nyingine bado TV series za Korea hazina bei kubwa.

Mfano Japan episode moja huanzia USD 20,000 na kuendelea na ndio maana vituo kama Channel 3 kutokea Thailand kutokea Vietnam vimejikita zaidi kuonesha Korean dramas kwa sababu bei zake zinaeleweka

Poleni kwa uzi mrefu ila ni hayo tu kwa leo.
jdu6jojo51z0l0in_1597146458.jpg
MBC-daejeon.jpg
6b69cd37554ef90dfa90ff548ca3c3ab.jpg

Poleni kwa uzi mrefu ila ni hayo tu kwa leo. View attachment 1770372View attachment 1770373View attachment 1770374View attachment 1770375

Gud for them kama wanapiga pesa, ila personally I don’t like watching their shits
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom