Ushauri wangu ni huu hapa.
1. Usiwaze ngono asilani, hata ukiona tu unakumbuka namna ulivyokuwa unafurahia pindi ufanyapo mapenzi na mkeo, hamisha mawazo haraka sana. Narudia, USIRUHUSU, USIRUHUSU, USIRUHUSU mawazo ya ngono yapite kichwani kwako.
2. Pili usiwe mwaminifu kwa ajili ya mkeo bali kuwa mwaminifu kwa kuwa wewe uko hivyo (Kwa kuwa unaamini katika uaminifu, na kwa kuwa ungependa kumpendeza Mungu wako). Hii maana yake ni kuwa hata kama utahakikisha kuwa mkeo anatoka nje ya ndoa, hii haitakiwi kukufanya wewe utoke nje ya ndoa.
3. Usiangalie movies na picha zinazohamasisha ngono. Na hata uwapo huko mitaani jizuie kadri uwezavyo kutupia macho warembo.
4. Mtegemee M'mungu katika kufanikisha azma yako, kwa sababu binadamu peke yetu tuna udhaifu mwingi sana.
5. Ongezea na hayo aliyosema
watu8 hapo juu.
6. Ukifanya yote hayo hapo juu, kuna wakati inafika asili huchukua mkondo wake na ndipo unapata zile ndoto waingereza wanaita wet dreams.
7. Sidhani kama itasaidia sana lakini si vibaya nikisema kuwa niliwahi ku-survive kwa miaka miwili kwa utaratibu huo hapo juu.
Kila la heri na bravo TEAM FAITHFULNESS.