Hakuna mrembo zaidi ya mke wangu!!!
Mkuu nakushukuru sana kwa comment hii, huu ndio strategy ya kwanza ya kukabilina na janga hili!
Ukiendekeza kufanya mwili unachokitamani utaleta balaa nyumbani kwako na huyo mke unayesema hakuna mzuri kuliko yeye ukamharibia, tena saana tu!
Miili hii Mkuu haitosheki, fikiria umefanya na mke wako mara ngapi, jee umewahi kutosheka? umekula mara ngapi, jee umewahi kutosheka? umetamani vitu vingapi vizuri hapa duniani, umepata vingapi, jee umewahi kutosheka!?
Jibu ni rahisi tuu hujawahi kutosheka, na hutakaa utosheke, MIILI hii haina shukrani Mkuu!
LAZIMA uwe na uwezo wa kuucontrol mwili wako, na sio kila k2 mwili unataka unaupatia, u will be killed unnoticed na ukaaviacha hivyo vizuri unavyofikiri unavipenda sana!
Imagine umeliona dude, HAMMER vehicle! ukalitamani sana na hata kutaka uliendesha siku hiyo hiyo, je utaenda kuvunja kiyoo na kuliendesha kwa sababu unalipenda sana!? jibu sio hata wewe unajua kuna taratibu za kulipata ambazo hazitakufanya ujutie maishani mwako! na utafurahiya milele
Mkuu simama, mpende sana mke wako na fanya chochote kwa ajili yake na kulinda ndoa yenu kwa gharama yoyote ikiwemo kutokutaka kumtendea dhambi kubwa namna hii (kutoka nje ya ndoa) na HICHO ndicho kipimo cha juu cha upendo kwa familia yako!
Watakushauri sana, kama walivyo anza kukushauri uende sijui wapi..... Mkuu hawajui nini maana ya familia, hwajui thamani ya mke, na Kubwa hawajui wanasema nini, Nawasamehe wote! nawe pia wasamehe
Moyo wako unajua ni kipi sahihi cha kufanya kuondolea majuto!
Usiku mwema sana.