Kwa wana JF ambao hawajawahi kukutana

Kwa wana JF ambao hawajawahi kukutana

kadoda11

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Posts
21,453
Reaction score
20,755
2011 inaiishia,mengi yamejadaliwa hapa jf.watu wamajenga marafiki/maadui,wamefurahi,wamenuna,wameshutumiwa,
wamekosolewa,wamekashifiwa,wametukanwa.kwa ujaumla mengi yametendeka hapa jf kwa 2011.sasa wewe ni mwana jf wa umri wa miaka 20,25 hadi 30.vuta picha siku unakutana uso kwa uso na mwana jf
mwenye umri kati ya miaka 45-50,anajitambulisha kwa ID yake anayo tumia hapa jf,unakumbuka kuna siku ktk mjadala flani mlipishana lugha.pasipo ustahimilivu yeye akakutukana mpaka ukaumia rohoni,mbaya zaidi lugha aliyo tumia kukutukana ni lugha za vijiweni tunazotumia vijana wa leo.unaangalia umbile lake na kugundua ni mtu aliye kuzidi umri kwa mbali sana,swali je utakumbushia na kumkanya kwa maneno yake machafu ya siku hiyo au utapotezea.tuendelee......
 
nitakumbushia ktk hali ya utani halafu ntamwambia siyo poa!
 
Nakukosoa siku tukikutana kwenye basi unikanyage. . .
Ungezingatia herufi kubwa ingependeza sana kujua nini kimeanzia wapi na kuishia wapi.
 
Kakuzidi umri na alikutukana kwa lugha za kijiweni!!!!!KUWA NA BUSARA VINGIVEVYO HUTAKUWA NA TOFAUTI NAE MSAMEHE NA MUHIMU ZAIDI MUOMBEE.
 
Kwakuwa sina mpango wa kukutana na member yeyote, hakuna haja ya kueleza msimamo wangu.
 
Nakukosoa siku tukikutana kwenye basi unikanyage. . .
Ungezingatia herufi kubwa ingependeza sana kujua nini kimeanzia wapi na kuishia wapi.
kosa lingine tena.bado hujaisoma thread yangu vzuri.pitia kwa mara ya pili.kwa jinsi unavyo niandama,nadhani unahitaji uwe rafiki yangu.cjui kwanini nawaza hivyo....kuna kusudi.
 
kosa lingine tena.bado hujaisoma thread yangu vzuri.pitia kwa mara ya pili.kwa jinsi unavyo niandama,nadhani unahitaji uwe rafiki yangu.cjui kwanini nawaza hivyo....kuna kusudi.

Haina mvuto, ukweli lazima nikwambie.
 
kwa tuliozoea kukutana....ya JF tunayaacha humuhumu....kinachoendelea ni kula maisha....
 
atakwambia, ntakuua

Nakukosoa siku tukikutana kwenye basi unikanyage. . .
Ungezingatia herufi kubwa ingependeza sana kujua nini kimeanzia wapi na kuishia wapi.
 
kosa lingine tena.bado hujaisoma thread yangu vzuri.pitia kwa mara ya pili.kwa jinsi unavyo niandama,nadhani unahitaji uwe rafiki yangu.cjui kwanini nawaza hivyo....kuna kusudi.
Hitaji?Rafiki?

Nilionao tu nataka kuwapunguza.
 
Back
Top Bottom