Wito Kwa wana JamiiForums kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,
Huu ni wito tuu kwa wana jf kuhusu ukosoaji wa Rais wa nchi, Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli, ufanyike kwa staha kwa kutanguliza mbele uzalendo, na maslahi ya taifa mbele, ukiwemo utaifa. Kuitanguliza mbele Tanzania kwanza ndipo rais Magufuli afuatie.

Rais Magufuli nae ni binadamu na sio malaika, hivyo, kama binadamu ni haki yake kukosea, kwasababu no one is perfect, the only perfect being is God!, hivyo Magufuli kama Magufuli kuna mahali anakosea au amefanya ndivyo sivyo, tupaseme sio kwa kubeza au kukejeli, bali kufanyike kwa heshima, kwa lugha ya staha na unyenyekevu kwa lengo la kumuonyesha makosa yake, kisha tuweke na ushauri wa the right thing to do, hivyo ukosoaji kwa rais, ufanyike constructively kwa nia njema ya kujenga na sio kubomoa, yaani tufanye "a constructive criticism" in good faith kwaa nia ya kumsaidia rais wetu kuwa rais bora zaidi na kulisaidia taifa kusonga mbele na sio kurudi nyuma kwa sababu kwa mujibu wa katiba yetu, rais hawezi kukosea ndio maana hawezi kushitakiwa.

Rais ana sehemu mbili, rais ni taasisi ya presidential institution hivyo rais kama taasisi hawezi kufanya kosa lolote ni perfect being kila kauli yake ni sheria, inafuatiwa na utekelezaji tuu, lakini hiyo institution inashikiliwa na kuongozwa mtu apmbaye ni binadamu tuu kama sisi anayeitwa John Pombe Joseph Magufuli, huyu ni binadamu wa kawaida kama sisi wengine wote, he is a human anaweza kukosea. Katika kumkosoa rais, tumkosoe kwa heshima in such a way tusije kujikuta tunakosa uzalendo, badala ya kumkosoa, tumamuaibisha na kujikuta tunajiabisha sisi kama taifa.

Nakiri kupandisha uzi huu kutokana na mchango wa mwana jf huyu
Mkuu Pasco Mtu anayekupa taarifa ya ambayo haiko sahihi utamuitaje?

Ukaguzi maalumu uliofanywa na ofisi ya CAG katika kipindi cha mwaka wa fedha 2010/11 na 2011/12 umebaini kuwa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, bungeni Novemba 2013 kuwa fedha hizo zilitumika kwa miradi ya ujenzi wa barabara, haikuwa sahihi.

Ufisadi wa kutisha waibuliwa
Rais wa nchi ndio kioo cha taifa, ni kama baba wa familia, anahitaji kuheshimiwa.

Hata ikitokea baba mwenye nyumba au baba nyumbani amekosea jambo fulani, anakosolewa kwa heshima kiutu uzima kwa kutumia lugha ya heshima na staha na sio lugha za dharau, kebehi, machukizo au matukano! .

Hata akidanganya haitwi muongo anaitwa hayuko sahihi sana, au ameshauriwa vibaya kwa sababu rais wa nchi hawezi kudanganya, wala hawezi kusema uongo!.

Hata akichelewa kwenye shughuli haambiwi kachelewa maana mkubwa hachelewi bali anakuwa bado hajawasili kutokana na kutingwa na shughuli muhimu, na asipotokea kabisa ni kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu!.

Simaanishi rais Magufuli yeye ni malaika hivyo hawezi kukosea au kufanya makosa, no!, rais Magufuli naye ni binaadamu tuu kama sisi binaadamu wengine wote, na siku zote sisi binaadamu ni viumbe dhaifu, hivyo rais Magufuli naye ana madhaifu yake ikiwemo kuonekana kama ni mtu wa kupenda kusifiwpa kupindukia, anapoongea kuna wakati anaonekana kama ni msema chochote na katika kufanya maamuzi, kuna wakati anaonekana kama anatenda badhi yap maamuzi kwa haraka na baadhi ya maamuzi yake, kuonekana kama ni maamuzi ya uamuzi wa haraka hivyo kukosa tafakuri ya kina ila kwa vile yeye ndie kiongozi wetu Mkuu, kuna mambo ambayo hatupaswi kuyasema hivyo yalivyo, hata kama ni kweli, hata kama ni kweli sometimes anaweza kusema kitu ambacho sio sahihi, hatupaswi kusema rais ni muongo bali rais hakuwa sahihi sana au alikuwa hajashauriwa vizuri au alikuwa ana joke tuu, au anazungumza kwa utani tuu, yaani rais anatania au rais ameteleza tuu ulimi!.

Mfano rais alipohimiza kufyatua tuu watoto kisa atasomesha bure. Tamko hili lilikwenda kinyume cha uzazi wa mpango, hapa rais kiukweli aliropoka na kuteleza ulimi, lakini haiwezi kusemwa kuwa rais karopoka, bali rais alikuwa anatania tuu watani zake, wazaramo!. Siku alipotamka hivyo, hata mimi nilishitushwa na tamko lile ( Rais Kusitisha Uzazi wa Mpango Kwa"Fyatueni Watoto wa Kutosha",Ni Yake au ni ya Wale Wazee wa..?!.)
Lakini baada ya siku mbili tatu, Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu aliibuka na kulitolea ufafanuzi wa kina tamko lile kuwa lilikuwa sii kweli bali rais alikuwa akiwatania tuu watani zake Wazaramo!.

Mfano kwenye hoja ya udikiteta, ni kweli rais Magufuli ni kama dikiteta fulani hivi, ila ni dikiteta Mzalendo. Hivyo ndivyo alivyo, tangu akiwa Waziri, he is a no nonsense man, hataki ujinga na hawezi kuvumilia uzembe, na sio kwamba anajifanyisha, ila pia, kwa Tanzania hapa tulipofika, seriously tulihitaji sana mtu mwenye sifa, silika na haiba za udikiteta ndio anaweza kuinyoosha hii nchi ilivyopinda kupindukia hadi kufanywa ni shamba la bibi!. Siku nyingi tumekuwa tukmlaumu JK kwa u pole wake hadi kumuita "dhaifu" hivyo tumekuwa tukisali kumuomba Mungu atupe kiongozi imara, shupavu, thabiti, ambaye sio mtu wa mchezo mchezo, na kweli hatimaye Mungu akaisikia sala yetu ametupatia Magufuli ambaye ni dikiteta kweli ila sio dikteta mbaya kama Hitler, huyu ni dikiteta mzuri " a benevolent dictator", hivyo badala ya watu kuulaumu huu udikiteta wa rais Magufuli, tunapashwa kumshukuru Mungu kutupatia Magufuli.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Watu walipoitwa Vila.za, hatukunyamaza, tulitoa ushauri humu.
Wito kwa Baba Jesca: Watendee Haki Kina Jesca Wote Ili Nao Wapate Bahati Kama Jesca!.

Hata alipozungumzia mishahara ya peponi, pia tulitoa ushauri humu
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote

Hata majumbani mwetu hasa majumba ya Kiafrika na Kiswahili, baba ambaye ni mkuu na kichwa cha nyumba, kuna mara kibao anakosea hasa sisi mababa wa Kiafrika tunaofuata mila zetu za kiasili za Kiafrika na mambo yetu yalee ya Uafrika wetu, na pia sio malaika hivyo tuna madhaifu mengi tuu ambayo wamama huyajua huyaona, huyavumilia lakini hawayasemi hadharani.

Kuna namna ya ukosoaji wa heshima na staha wenye lengo la kujenga, a constructive criticism ambao hufanywa in good faith na kuna ukoasoaji wa mbaya wa udhalilishaji wenye lengo la kubomoa, kubagaza, kudunisha na kumshusha mtu kwa kumvunjia heshima ambao hufanywa in bad faith, ridiculously au kumdhalilisha, mkosolewa kwa nia ya kumjengea chuki, achukiwe, kumshushia hadhi na heshima ili aonekane ni mtu wa hovyo, etc huu sio ukosoaji mzuri hata kama ni kweli amekosea, yaani japo is the truth but the motive behind is ill motive.

Simaanishi sasa ndio wote kazi yetu iwe ni moja tuu, kumhusu rais wetu, iwe ni kumuimbia tuu nyimbo za sifa na mapambio, no !, tumkosoe rais Magufuli kwa heshima na kwa kutumia lugha ta staha kwa nia njema kabisa kwa lengo la kumrekebisha na kumsaidia na sio kumdhalilisha.

Tanzania ni yetu sote, sio Tanzania ya Magufuli pekee, na japo CCM ndio chama tawala, haimaanishi Tanzania ni ya CCM, Tanzania sio ya CCM pekee, ni Tanzania ya wote, hivyo we all have a role to play and a responsibility of duty of care kujenga nchi yetu kwa kutanguliza uzalendo na kuweka mbele maslahi ya taifa kwa kujenga na sio kuibomoa na kumjenga rais wetu na sio kumbomoa regardless tunampenda, hatupendi, tulimchagua, hatukumchagua, kama wazalendo wa nchi hii ni lazima kuijenga nchi yetu na kumsaidia rais wetu as a responsibility and a duty of care, kama inavyotokea kuwepo kwa mtoto mwenye ulemavu katika familia, hakuna anayependa ulemavu, lakini imetokea, lazima tumpende and we have a duty of care kumsupport, kumsaidia na kupenda kwa dhati, vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa rais Magufuli, ndie rais wetu wa sasa na hivi alivyo ndivyo alivyo, tumkubali, sio lazima tumpende lakini tunawajibu wa kumpa kila aina ya ushirikiano ili aweze kulitawala vyema taifa letu.

Kuna watu katika kumbonda rais Magufuli, kila siku kazi yao wao ni kuponda tuu, hata akifanya mazuri vipi, wao wataponda tuu, kubeza, kukosoa kila kitu na kumbomoa tuu, na katika kuponda huku, sometimes hujikuta wanaponda over and obove na kuliaibisha taifa letu, na wengine humsifia Nyerere, yaani kumtumia wasifu wa Nyerere as a reference, ila kiukweli ukimwangalia rais Magufuli kwa jicho la karibu, yuko kama Nyerere kwa karibu kila kitu
Magufuli Kama Nyerere:Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni Kazi Tuu, Ila Pia,Sio Kama Nyerere!.

Katika kujenga nchi the motive iwe ni kujenga kila kitu ikiwemo kujenga watu akiwemo rais anahitaji kuendelea kujengwa na sio kubomolewa tuu.

Japo nafahamu katika kujenga, kuna sehemu inaweza ikakubidi ubomoe kwanza ndipo ujenge, ubomoaji huo hufanyika kwa makini sana ili usibomoe kusiko husika na kila ubomoaji huo ukifanyika hufuatiwa na ujenzi papo kwa papo! .

Nitapenda kuiona jf ya hivyo, wale waashi mahiri wa jf ambao kazi yao ni kubomoa tuu, wapewe jukumu la kujenga pia sio kila siku wao ni kubomoa tuu, mwisho watapewa sifa ya kuitwa wabomoaji tuu ili hali tuna wajenzi imara na mahiri humu tena waliopitia kozi za uanagenzi kwa wale mahiri kabisa.

Wana jf tuwe wakweli kumhusu rais Magufuli toka ndani ya nafsi zetu sio kwa kuvaa miwani yenye kuona upande mmoja tuu wa mabaya tuu, mapungufu tuu na makosa pekee, bali kama kuna mema pia tuyaone, kama kuna mazuri pia tuyaangazie na kuyasema as encouragement kwa rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Rejea kuhusu ukosoaji. Zifuatazo hapa chini ni baadhi tuu za mada zangu za ukosoaji.

Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria! .
JF Modes, Magufuli ni Rais Wetu, Asiabudiwe, Asiogopwe, Bali Aheshimiwe!.
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki Haki za Binaadamu?!..
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyo
te
Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia!. Akishika Chama, Watakoma

Magufuli, "Kama Unaona Kazi ya Urais ni Ngumu Kwako, Jiuzulu! ".

Je inawezekana huu ndio mwisho wa utumbuaji wa papara na kukurupuka?! Mkuu kutumbuliwa soon!
 
Habari hii ilichapishwa kwenye gazeti la RAI miaka michache iliyopita ikisomeka...

Huyu Ndiye Pombe Magufuli:

- Wasema nyumba 8,000 kauza kwa mkono wake mwenyewe
- Apuuza maonyo ya wataalamu- Mafaili ya Sundi na Musa aliyabeba kwapani

ALIYEKUWA Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, katika Serikali ya awamu ya tatu, aliteka madaraka na kuwa mwenyekiti wa zoezi la kuuza nyumba za serikali ambazo hadi sasa, zimeshauzwa 8,288 imefahamika.

Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya ‘fujo’ katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri kinyume na matakwa.

Ni chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli, aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.

Habari hizo zinaeleza kwamba awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu. Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari mfanyakazi wa Serikali.

Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi miwili akaacha kazi.

“Kwa upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake Sundi,” vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba hizo.

Habari hizo zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba hiyo.

“Ndipo Magufuli aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote, mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili,” chanzo hicho cha habari kinaeleza.

Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa Serikali.

Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.

Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

Hadi Machi mwaka huu, wajumbe hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha, Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A. Bukuku.

Hata hivyo, sheria haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

Mtendaji Mkuu wa TBA Togolayi Makumba Kimweri, alipoulizwa kupitia kwa Katibu Muhtasi wake, alimwambia mwandishi wa Rai aandike maswali kisha asubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi.

Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda wa saa moja, mwandishi alipokwenda kuuliza akaambiwa kwamba Kimweri tayari alikwishaondoka ofisini kupitia mlango wa nyuma na asingeweza kurudi ofisini.

Lakini baadhi ya wafanyakazi wa TBA wameiambia Rai kwamba kinachoandikwa kwenye magazeti kuhusu ushiriki wa Magufuli kuuza nyumba za Serikali ni kidogo mno kuliko hali halisi.

Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa, waziri Magufuli alishinikiza mtoto wa dada yake anayeitwa James Doto Mgosha auziwe nyumba za serikali kwa kumtengenezea ajira ya muda mfupi katika TANROADS.

Tofauti na Musa, Doto ameuziwa nyumba hiyo kwa jina la mtu mwingine lakini anaishi katika nyumba hiyo, namba 64 iliyopo Kinondoni Flats.

Habari kutoka TBA zinaonyesha jina la mtu mwingine (tunalihifadhi) kuwa ndiye aliyeuziwa nyumba hiyo mtu huyo alipata kupitia utaratibu wa Magufuli kupeleka jina lake kwenye wakala wa majengo na kulazimisha apewe nyumba.

Alipoulizwa kwa njia ya simu, Doto alisema suala la ajira na nyumba waulizwe waliomwajiri na kumpa nyumba. Akakata simu.

Mfanyakazi mwingine alieleza Rai kwamba msichana mwingine (jina tunalihifadhi) akiwa na miezi minne tu kazini alipelekwa na Magufuli katika Wakala wa Majengo akilazimisha auziwe nyumba hata kabla ya kuthibitishwa kazini. Nyumba hiyo iko Block A, Ocean Road.

Hata hivyo, habari hizo zinaeleza kwamba msichana huyo ambaye hadi sasa anaishi na wazazi wake, ameipangisha nyumba hiyo kwa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na analipwa kwa dola za kimarekani.

“Kuuza nyumba za serikali sawa, lakini kweli katika mtindo huu? Sisi tunaoshiriki kuzikagua na kuziratibu tukiomba hatupati, lakini wengine wanaingia serikalini miezi miwili wanapata nyumba. Na wengine hata si wafanyakazi, wanapata, hii si sahihi, alilalamika mfanyakazi mmoja aliyeandikia Rai kwa njia ya barua pepe.

Hadi Machi mwaka huu Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) walishauza nyumba 8,288 ambazo hata hivyo zilitakiwa kuuzwa kwa watumishi wa serikali.

Katika mauzo hayo, Serikali ilitarajia kupata jumla ya shilingi 60,016,556,439.00. Hata hivyo hadi sasa Serikali imepata shilingi 22,684,108,115.08.

Kwa sasa, Serikali imebakiwa na nyumba 1,098 zinazosimamiwa na TBA. Kati ya hizo, nyumba 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa Serikali, nyumba 675 kama tied quarters, nyumba 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 ni kama karakana na bohari.

SALVA RWEYEMAMU
RAI
 
Posted 10/3/2015
Ufisadi wa kutisha waibuliwa

magufuli_clip.jpg

Waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli akikagua ujenzi wa kituo cha Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (BRT) Morocco jijini Dar es Salaam siku za hivi karibuni. Picha na Maktaba
By Ibrahim Yamola, Mwananchi
In Summary
Ukaguzi maalumu uliofanywa na ofisi ya CAG katika kipindi cha mwaka wa fedha 2010/11 na 2011/12 umebaini kuwa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, bungeni Novemba 2013 kuwa fedha hizo zilitumika kwa miradi ya ujenzi wa barabara, haikuwa sahihi.

ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
Dar es Salaam. Machungu ya Watanzania yakiwa hayajapoa kutokana na kashfa ya Sh306 bilioni kutoka katika Akaunti ya Tegeta Escrow, ufisadi mwingine wa zaidi ya Sh252 bilioni umeibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad ndani ya wizara ya ujenzi.

Ukaguzi maalumu uliofanywa na ofisi ya CAG katika kipindi cha mwaka wa fedha 2010/11 na 2011/12 umebaini kuwa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, bungeni Novemba 2013 kuwa fedha hizo zilitumika kwa miradi ya ujenzi wa barabara, haikuwa sahihi.

Kutokana na ufisadi huo, habari zilizolifikia Mwananchi zinasema CAG amependekeza hatua stahiki zichukuliwe kwa wahusika wa wizara ya ujenzi na wakala wa barabara ili kuleta imani na uwazi katika bajeti kwa jamii na wahisani.

“Wizara (ya ujenzi) ililidanganya Bunge kuwa kuna ujenzi wa barabara hizo wakati wakijua kwamba walikusudia kulipa madeni ya wakandarasi na washauri wa ujenzi wa barabara...mpango mkakati wa wakala wa barabara wa mwaka wa fedha 2011/12 pamoja na manunuzi ulioidhinishwa havikuonyesha utekelezaji wa mradi huo,” chanzo cha habari kilikariri ripoti ya CAG.

Matumizi hayo yasiyo sahihi yaliibuliwa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) Novemba 22, 2013 baada ya kutilia shaka kiasi hicho cha fedha na ofisi ya CAG kuagizwa kufanya ukaguzi.

Katika kikao hicho ambacho wizara ya ujenzi iliwakilishwa na Katibu Mkuu wake wa wakati huo, Balozi Herbert Mrango alihojiwa na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa CAG mwaka 2011/12.

Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo Sh348.1 bilioni zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililokuwa limetajwa kuwa ni la mradi maalumu hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni.

“Ni vizuri leo (ilikuwa Novemba 22 mwaka 2013) uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. Tunajua kwamba fedha hizi zilipunguzwa Sh95 bilioni na kupelekwa Wizara ya Uchukuzi, zilibakia Sh252.975 bilioni katika kifungu hicho lakini kuna bilioni 100 zimetumika visivyo,” alisema Zitto.

Alisema katika majumuisho ya bajeti wizara hiyo, Dk Magufuli na Dk Harrison Makyembe aliyekuwa Naibu waziri wa wakati huo aliyekuwa Waziri wa Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi walitoa maelezo yasiyo ya kweli bungeni kuhusu fedha hizo.

Zitto alikariri maneno yaliyorekodiwa kwenye Hansard ya Bunge yaliyosemwa na viongozi hao watatu.

“Tunaomba fedha Sh252 bilioni kwa ajili ya kuanzia kazi za ujenzi wa barabara.”

“Fedha hizi zitachangia miradi ya wafadhili,” haya yalikuwa maneno ya Dk Makyembe ambaye sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati akifafanua majumuisho.

“Hizi ni fedha kwa ajili ya Counterpart fund,” alimkariri Lukuvi ambaye sasa ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakati akichangia hotuba ya wizara hiyo.

Chanzo cha habari kimeeleza kuwa ripoti ya CAG imeeleza kuwa, “Katika kikao cha kuanza ukaguzi huo Aprili 3, mwaka jana uongozi wa wizara ulithibitisha kwamba hakukuwa na barabara mpya bali walifanya hivyo baada ya kuona madeni yamekuwa makubwa kiasi cha Sh420 bilioni kama yalivyokuwa kwenye hesabu za wakala wa barabara za mwaka wa fedha 2010/11.”

Katika ukaguzi huo imebainishwa kuwa Sh3 bilioni hazikujulikana matumizi yake.

Taarifa zaidi zinasema baada ya wizara kupeleka fedha kwa wakala wa barabara, fedha hizo zilifanyiwa mchakato wa kuzigawa upya lakini nyaraka halisi zilizotumika kugawa fedha hizo hazikuwasilishwa kwa ukaguzi.

“Hata hivyo, kati ya Sh175.3 bilioni zilizopitia kwenye akaunti ya maendeleo ya wakala wa barabara, kiasi cha Sh3,048,365,229 hakikuweza kupatiwa maelezo jinsi kilivyotumika.

“Pia, kati ya malipo ya Sh77.7 bilioni yaliyofanyika kwa wakandarasi au washauri wa barabara moja kwa moja kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Novemba 30, mwaka 2011 kupitia barua ya kumbukumbu namba GA.65/263/01/VOL.XI Gavana Mkuu wa BoT, alikanusha kulipa asilimia 30 ya fedha hizo Sh30.6 bilioni.

“Gavana wa BoT amekanusha kulipa Sh30.6 bilioni kwa kampuni ya M/S Strabag Internationl Gmbn na M/S China-Engineering Corporation Co, kati ya Sh77.7 ambacho kilipelekwa BoT kwa ajili ya malipo kwa wakandarasi au washauri mbalimbali,” alifafanua zaidi mtoa habari hizi na kuongeza:

“Ukaguzi maalumu umeshindwa kuthibitisha malipo yenye jumla ya Sh47.1 bilioni sawa na asilimia 61 kama yalilipwa kwa walengwa waliokusudiwa kwa sababu Gavana wa BoT amesema kuwa kisheria hatakiwi kutoa taarifa za wateja.”

Pia, habari za ndani kutoka ofisi ya CAG zinadai kuwa, Sh13.4 bilioni za ujenzi wa barabara za mikoa zilitumika kulipia barabara binafsi na za halmashauri za wilaya ambazo hutengewa fedha kupitia mfuko wa barabara kinyume na makusudio yaliyopitishwa na Bunge.

“Pia, nimebaini kwamba baadhi ya miradi haikuwamo kwenye kasma zilizopitishwa na Bunge kwenye makisio ya mwaka wa fedha 2010/11 na miradi mingine ilitengewa fedha kidogo lakini wakala wa barabara alitumia fedha nyingi kulipia miradi hiyo bila kuonyesha jinsi alivyozipata,” chanzo cha habari kimekariri ripoti ya CAG.

Katika ukaguzi huo, ufisadi mwingine wa Sh36.6 bilioni ambazo ni malipo ambayo hayakutolewa taarifa kwenye ripoti za washauri au wakandarasi, jambo linaweza kuwapo kwa uwezekano mkubwa wa wakandarasi kuidai Serikali zaidi ya mara moja na kuitia Serikali hasara.

Mtoa habari wetu alisema kuwa Sh6.2 bilioni zilitumika kuwalipa wakandarasi ambao hawakuonyeshwa katika orodha ya madeni yaliyowasilishwa bungeni pamoja na malipo ya Sh6.6 bilioni yaliyokwishalipwa yaliombewa tena.

“Madeni hayo yalikuwa yamelipwa na wakala wa barabara katika mikoa husika. Hali hii inaashiria kwamba kwa hati ya madai moja kuna uwezekano wa mkandarasi kulipwa mara mbili au zaidi.

Katika mapendekezo ya jumla, chanzo chetu kimesema ofisi ya CAG imeishauri Serikali kusimamisha kuingia mikataba mipya ya ujenzi wa barabara na ilipe madeni ya wakandarasi yaliyopo kwa sasa ili kuepuka ukuaji wa deni hilo kwa siku za baadaye na kuwa mzigo kwa Taifa na wananchi.

“Serikali ihakikishe inaheshimu mikataba iliyowekwa kati yake na wakandarasi ili kuepuka malipo yenye riba na kushtakiwa na wakandarasi kutokana na kuvunja masharti yaliyowekwa kwenye mikataba,” kilifafanua chanzo chetu na kuongeza:

“Zabuni za ujenzi wa barabara mpya ziendane na fedha zilizotengwa katika mwaka wa fedha husika kama itakavyokuwa imeainishwa katika mpango wa manunuzi wa mwaka huo.”

Ukaguzi huo maalumu uliohusisha miradi 46 ya ujenzi wa barabara kuu na barabara za mikoa ambazo wakandarasi na washauri wa ujenzi wa barabara walitoa huduma kwa wakala wa barabara.

“Mbali na miradi hii 46, miradi yote ya wakala wa barabara ilikuwa imezalisha madeni ya jumla ya Sh420 bilioni kama yalivyo kwenye hesabu za wizara kufikia mwaka wa fedha 2010/11,” kilieleza chanzo chetu.

Sakata hili limeibuka wakati lile la uchotwaji wa fedha za Akautni ya Tegeta Escrow halijapoa na hadi sasa limesababisha Rais Jakaya Kikwete kufanya mabadiliko madogo ya baraza lake la mawaziri kufuatia kumfukuza kazi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka huku Profesa Sospeter Muhongo alitangaza kuachia wadhifa wa Waziri wa Nishati na Madini.

Mbali na hao, pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alitangaza kujiuzuru huku Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akimsimamisha kazi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi kupisha uchunguzi wa sakata hilo.

Katika mlolongo wa hatua za kinidhamu kuchukuliwa, baadhi ya watumishi wa umma wamefikishwa mahakamani na wengine mbele ya Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
 
Wanabodi,
Huu ni wito tuu kwa wana jf kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli, ufanyike constructively kwa nia njema ya kujenga na sio kubomoa tuu, yaani tufanye "a constructive criticism" kama kuna mahali amekosea, au amefanya ndivyo sivyo, tupaseme kwa lugha ya heshima na staha, kisha tuweke na ushauri wa the right thing to do, hivyo ukosoaji huu utakuwa unamsaidia rais wetu na kuisaidia nchi yetu.

Nakiri kupandisha uzi huu kutokana na mchango wa mwana jf huyu

Rais wa nchi ni kama baba wa familia, anahitaji kuheshimiwa.

Hata akikosea anakosolewa kwa heshima fulani.

Hata akidanganya haitwi muongo.

Hata akichelewa kwenye shughuli haambiwi kachelewa maana mkubwa hachelewi bali anakuwa hajafika.

Simaanishi Magufuli ni malaika au hawezi kufanya makosa, Magufuli naye ni binaadamu tuu kama binaadamu wengine na siku zote binaadamu ni viumbe dhaifu, hivyo Magufuli naye ana madhaifu yake ikiwemo kupenda misifa, kuropoka na kufanya maamuzi ya papara na kukurupuka ila kwa vile ndie kiongozi Mkuu wetu kuna mambo ambayo hatupaswi kuyasema ikiwemo kumuita rais ni muongo hata kama ni kweli ni muongo.

Hata majumbani mwetu baba ambaye ni kichwa cha nyumba, ana madhaifu mengi ambayo mama huyajua lakini hayasemi hadharani.

Kuna namna ya ukosoaji wa heshima wenye lengo la kujenga, a constructive criticism ambao hufanywa in good faith na kuna ukoasoaji wa udhalilishaji ambao hufanywa in bad faith, ridiculously kumdhalilisha, kumjengea chuki, achukiwe, kumshushia heshima etc ambayo japo is the truth but the motive behind is ill motive.

Simaanishi sasa ndio wote kazi yetu iwe ni kumuimbia nyimbo za sifa na mapambio, no tumkosoe kwa heshima na kwa nia njema kabisa kwa lengo la kumrekebisha na kumsaidia na sio kumdhalilisha.

Tanzania ni yetu sote, sio Tanzania ya Magufuli pekee, we all have a role to play and a responsibility of duty of care kujenga na sio kubomoa.

Katika kujenga nchi the motive iwe ni kujenga kila kitu ikiwemo kujenga watu akiwemo rais anahitaji kuendelea kujengwa na sio kubomolewa tuu.

Japo nafahamu katika kujenga, kuna sehemu itakubidi ubomoe ndipo ujenge, ubomoaji huo hufanyika kwa makini sana ili usibomoe kusiko husika na kila ubomoaji huo ukifanyika hufuatiwa na ujenzi papo kwa papo! .

Nitapenda kuiona jf ya hivyo, wale waashi mahiri wa jf ambao kazi yao ni kubomoa tuu, wapewe jukumu la kujenga pia sio kila siku wao ni kubomoa tuu, mwisho watapewa sifa ya kuitwa wabomoaji tuu ili hali tuna wajenzi imara na mahiri humu tena waliopitia kozi za uanagenzi kwa wale mahiri kabisa.

Mungu Ibariki Tanzania.

Pasco.

Pasco acha vitu vya ajabu. Afrika iko hivi kwa msimamo km wako. Mfalme yuko uchi wa mnyama watu wanashangilia eti kavaa nguo nzuri haijawahi kuonekana. Upuuzi huo umepitwa na wakati. Baba anambaka mwanaye wa kumzaa inasemwa amemgusa hajambaka. Hii hapana. Mwizi ni mwizi, dikiteita ni dikiteita, mtakatifu ni mtakatifu, mbakaji ni mbakaji.
 
Hizi ni ripoti za CAG, CAG huwa haandiki uongo na anachoandika ndani ya ripoti zake ni baada ya uchunguzi wa kina unaofanywa na wakaguzi wa mahesabu. Hawezi mtu akaidharau katiba ya nchi pamoja na kuwa aliahidi kuilinda na kuheshimu katika hiyo halafu akaheshimiwa. Hata jina la dikteta uchwara chanzo chake ni dharau aliyoionyesha kwa wapinzani na katiba ya nchi.

BAK naona Pascoe amekuweka pagumu Leo .

Anyway vizuri kuona watu na magaZeti yaliyoleta habari hii kipindi hicho.

Ingawa haya magazeti wakati mwingine Si yakuaminika kivile.
 
Akosolewe kwa heshima? Soma hapa kwanza,aliingizwa madarakani kwa kura za wizi,hatAki demokrasia ifanye kazi,Zanzibar anazidisha matatizo kwa kumshauri rais was huko asimpe hela za matibabu waziri mkuu mstaafu wakati IPO kisheria,analazimisha mrisho gambo aendelee kutuletea matatizo na anajua sisi wana arusha tulimchagu lema kuwa mwaKilishi wetu hapo INA maana anatudharau sisi tuliomchagua lema,amekosa washauri wazuri na angekuwa nao angekuwa best president
 
Habari hii ilichapishwa kwenye gazeti la RAI miaka michache iliyopita ikisomeka...

Huyu Ndiye Pombe Magufuli:

- Wasema nyumba 8,000 kauza kwa mkono wake mwenyewe
- Apuuza maonyo ya wataalamu- Mafaili ya Sundi na Musa aliyabeba kwapani

ALIYEKUWA Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, katika Serikali ya awamu ya tatu, aliteka madaraka na kuwa mwenyekiti wa zoezi la kuuza nyumba za serikali ambazo hadi sasa, zimeshauzwa 8,288 imefahamika.

Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya ‘fujo’ katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri kinyume na matakwa.

Ni chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli, aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.

Habari hizo zinaeleza kwamba awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu. Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari mfanyakazi wa Serikali.

Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi miwili akaacha kazi.

“Kwa upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake Sundi,” vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba hizo.

Habari hizo zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba hiyo.

“Ndipo Magufuli aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote, mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili,” chanzo hicho cha habari kinaeleza.

Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa Serikali.

Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.

Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

Hadi Machi mwaka huu, wajumbe hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha, Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A. Bukuku.

Hata hivyo, sheria haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

Mtendaji Mkuu wa TBA Togolayi Makumba Kimweri, alipoulizwa kupitia kwa Katibu Muhtasi wake, alimwambia mwandishi wa Rai aandike maswali kisha asubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi.

Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda wa saa moja, mwandishi alipokwenda kuuliza akaambiwa kwamba Kimweri tayari alikwishaondoka ofisini kupitia mlango wa nyuma na asingeweza kurudi ofisini.

Lakini baadhi ya wafanyakazi wa TBA wameiambia Rai kwamba kinachoandikwa kwenye magazeti kuhusu ushiriki wa Magufuli kuuza nyumba za Serikali ni kidogo mno kuliko hali halisi.

Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa, waziri Magufuli alishinikiza mtoto wa dada yake anayeitwa James Doto Mgosha auziwe nyumba za serikali kwa kumtengenezea ajira ya muda mfupi katika TANROADS.

Tofauti na Musa, Doto ameuziwa nyumba hiyo kwa jina la mtu mwingine lakini anaishi katika nyumba hiyo, namba 64 iliyopo Kinondoni Flats.

Habari kutoka TBA zinaonyesha jina la mtu mwingine (tunalihifadhi) kuwa ndiye aliyeuziwa nyumba hiyo mtu huyo alipata kupitia utaratibu wa Magufuli kupeleka jina lake kwenye wakala wa majengo na kulazimisha apewe nyumba.

Alipoulizwa kwa njia ya simu, Doto alisema suala la ajira na nyumba waulizwe waliomwajiri na kumpa nyumba. Akakata simu.

Mfanyakazi mwingine alieleza Rai kwamba msichana mwingine (jina tunalihifadhi) akiwa na miezi minne tu kazini alipelekwa na Magufuli katika Wakala wa Majengo akilazimisha auziwe nyumba hata kabla ya kuthibitishwa kazini. Nyumba hiyo iko Block A, Ocean Road.

Hata hivyo, habari hizo zinaeleza kwamba msichana huyo ambaye hadi sasa anaishi na wazazi wake, ameipangisha nyumba hiyo kwa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na analipwa kwa dola za kimarekani.

“Kuuza nyumba za serikali sawa, lakini kweli katika mtindo huu? Sisi tunaoshiriki kuzikagua na kuziratibu tukiomba hatupati, lakini wengine wanaingia serikalini miezi miwili wanapata nyumba. Na wengine hata si wafanyakazi, wanapata, hii si sahihi, alilalamika mfanyakazi mmoja aliyeandikia Rai kwa njia ya barua pepe.

Hadi Machi mwaka huu Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) walishauza nyumba 8,288 ambazo hata hivyo zilitakiwa kuuzwa kwa watumishi wa serikali.

Katika mauzo hayo, Serikali ilitarajia kupata jumla ya shilingi 60,016,556,439.00. Hata hivyo hadi sasa Serikali imepata shilingi 22,684,108,115.08.

Kwa sasa, Serikali imebakiwa na nyumba 1,098 zinazosimamiwa na TBA. Kati ya hizo, nyumba 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa Serikali, nyumba 675 kama tied quarters, nyumba 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 ni kama karakana na bohari.

SALVA RWEYEMAMU
RAI
Mkuu BAK habari ndeefu ila imenikumbusha kwamba iliandikwa na Salva Rweyemamu
 
Kenda kununua uozo wa boti kwa shilingi bilioni 8 pesa za walipa kodi. Boti limefanya kazi siku chache tu na sasa liko juu ya mawe.

Lugumi kazuia ripoti ya ufisadi huu isijadiliwe Bungeni kwa sababu anazozijua yeye.

Zaidi ya bilioni 15 za wahanga wa tetemeko kazikumbatia kwa wiki ya saba sasa bila sababu yoyote ile ya msingi, hata kwenda kuwafariji hataki.

Pamoja na yote haya bado eti aheshimiwe!

Akosolewe kwa heshima? Soma hapa kwanza,aliingizwa madarakani kwa kura za wizi,hatAki demokrasia ifanye kazi,Zanzibar anazidisha matatizo kwa kumshauri rais was huko asimpe hela za matibabu waziri mkuu mstaafu wakati IPO kisheria,analazimisha mrisho gambo aendelee kutuletea matatizo na anajua sisi wana arusha tulimchagu lema kuwa mwaKilishi wetu hapo INA maana anatudharau sisi tuliomchagua lema,amekosa washauri wazuri na angekuwa nao angekuwa best president
 
Wewe Pasco ndio labda hujajua kua rais ni malaika, tena malaika alie karibu na Mungu.

Kuna mambo mengi anayoyatamka yanayothibitisha kua yeye ni malaika, ni mteule toka mbinguni malaha pa juu palipoinuka na palipotukuka aliekuja duniani kushughulikia matatizo ya binadamu.

Kitendo cha kuita binadamu wenzake mashetani na kusisitiza kua amechaguliwa kushughulikia mashetani kinadhihirisha wazi kua yeye ni Malaika.

Nakuomba usimkosee rais wetu heshima kwa kusema kua yeye sio malaika. Rais wetu ni malaika wa cheo cha juu kabisa .
 
Hizi ni ripoti za CAG, CAG huwa haandiki uongo na anachoandika ndani ya ripoti zake ni baada ya uchunguzi wa kina unaofanywa na wakaguzi wa mahesabu. Hawezi mtu akaidharau katiba ya nchi pamoja na kuwa aliahidi kuilinda na kuheshimu katika hiyo halafu akaheshimiwa. Hata jina la dikteta uchwara chanzo chake ni dharau aliyoionyesha kwa wapinzani na katiba ya nchi.
Kwa hiyo yeye mwenyewe ni jipu kubwa tu?
 
Thanks a million.

Komenti yako imejaa uzalendo, hekima na busara.

Mwenye kutaka kujifunza ulichokiandika ataelimika vizuri lakini mwenye kudhani anaelewa na kuanza kupinga komenti yako hii, huyo kama ulivyosema atakuwa mshusha heshima na mjenga chuki ili Rais achukiwe bila sababu ya msingi.

Kwa mtu anayefahamu vizuri mazingira na siasa za Tanzania ataelewa kuwa Tanzania itakuwa na Rais Magufuli mpaka 2025 labda tu Mwenyezi Mungu ampende zaidi kabla ya muda huo.

Kutaka kujenga chuki hakuwezi kumfanya Rais Magufuli aachie kiti na mbaya zaidi, hata akiamua kutofanya kazi za manufaa kwa taifa, hakuna uwanja ulio wazi na mpana wa kumwajibisha kisheria zaidi ya kusubiri mpaka muda wake utakapomalizika kikatiba lakini vile vile hata Katiba katika Ibara ya 46(1-3) inazuia kumshitaki kwa sababu ya ''madudu'' aliyoyafanya wakati akiwa Rais wa Tanzania.

Hata akifanya ‘’madudu’’ na kuondoka, sioni retrospective legislation ikipata nafasi katika uwanja wa siasa za Tanzania.
 
Magufuli si malaika ! ni binadamu kama wengine ! Anawaza,analala,anakula nk kama wengine tu ! Cha msingi tujaribu kumsoma kiongozi wetu kuwa nini ilikuwa dhamira yake kwenye jambo fulani ! Rais anaweza akawa na dhamira fulani njema juu ya jambo fulani lkn akateleza tu ktk namna kuliwasilisha kwa wahusika,Rais ni binadamu kama wengine tu jamani,Cha msingi ni sisi kujiongeza kwa kumuelewa rais wetu anataka nini na nini dhamira yake juu ya jambo fulani tutaishi kwa amani sana.
 
Pasco wapo watakaokuelewa lakini wengine ndio kazi yao hiyo kupinga tu. Wao jema litafanywa na Chadema tu .....hao wamekopi wanachofanya propagandist wa CCM ambao pia daima hawaoni upinzani kuja na wazo jema. Hivi ndio siasa zetu zilivyojengwa na tunaaminishana siasa ziko hivyo. Siasa uchwara zenye msingi wa mafisadi.
 
Maneno mazito mazito sijui kuropoka,kukurupuka hayatatusaidia/hayatamsaidia hata kidogo ! Tukosoe kwa hekima na uzuri wake rais huwa anasoma haya mambo vizuri ! Yeye anatuongoza lkn sisi tunamuongoza yy pia kwa kumkosoa kwa hekima na kumpa namna bora ya kutekeleza kazi zake badala ya kulaumu tu.
 
Thanks a million.

Kwa mtu anayefahamu vizuri mazingira na siasa za Tanzania ataelewa kuwa Tanzania itakuwa na Rais Magufuli mpaka 2025 labda tu Mwenyezi Mungu ampende zaidi kabla ya muda huo.
Sikujua kuwa "alichaguliwa" kwa miaka kumi.

Kutaka kujenga chuki hakuwezi kumfanya Rais Magufuli aachie kiti na mbaya zaidi, hata akiamua kutofanya kazi za manufaa kwa taifa, hakuna uwanja ulio wazi na mpana wa kumwajibisha kisheria zaidi ya kusubiri mpaka muda wake utakapomalizika kikatiba lakini vile vile hata Katiba katika Ibara ya 46(1-3) inazuia kumshitaki kwa sababu ya ''madudu'' aliyoyafanya wakati akiwa Rais wa Tanzania.
Na madudu aliyofanya wakati akiwa waziri ndiyo vipi?
Hata akifanya ‘’madudu’’ na kuondoka, sioni retrospective legislation ikipata nafasi katika uwanja wa siasa za Tanzania.
You mean rectroactive? Shida ni Tanzania kujidanganya kuwa tunafuata utawala wa sheria. Rule of law is not selective, you prosecute some crimes but overlook the others
 
Back
Top Bottom