Kwa wana CCM wacha Mungu: Je, mnaamini mmeshinda kihalali na uchaguzi ulikuwa huru na wa haki? Kila mmoja wetu atasimama mbele za kiti cha hukumu

Viti maalum yumo mpaka mwenyekiti wa akina mama chadema
 
Kwahiyo hizi ndii sababu za kuwafanye muibe kura?

Vipi na wabunge?

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
Mkuu hakuna aliyemuibia Kura mwenzake.Chadema hawakujianga kwa uchaguzi.Hata taasis moja ya Kenya ilishatabili kuwa CCM wangeshinda kwa asili Mia 79.6 Sasa hapo ukiweka plus or minus 5 utaona wazi kuwa utabili wao ulikuwa sahihi.
 
Endelea kuamini Mungu kwenye mambo ya siasa uone patashika yake kibinadamu..
 
Kazi ya Magufuli ya miaka mitano ndiyo imesababisha CCM kushinda kama ulivyoona,kujipa stress na mawazo mengi eti wameiba wameiba ni kujipotezea muda tu.

Walichokua wanataka wananchi ndicho walichoona kwa miaka mitano,sasa unadhani kura zisinge ongezeka?

Chadema pia ni kundi la wahuni wachache wenye vinasaba vya kikaskazini wapenda pesa waliotaka kuingia Ikulu kuipiga nchi pesa. Isipokua kwa mapenzi ya vyama ndiyo maana jamii haiwezi kuona hili.

Ukiitaja CCM unaiona nchi nzima,ukiitaja chadema unaionaa Arusha na Kilimanjaro...unategemea kuna nini hapo?

Tumieni akili,na kwa mambo haya ya siasa,binafsi nimeona kuna kitu hapa Tanzania,kuna tatizo kwenye vichwa vya wengi, uwezo wa kufikiri mambo kwa kina ni mdogo sana sana sana kupita kiasi
 
Mimi naamini tumeshinda kihalali na kwa dhati kabisa uchanguzi ulikuwa huru na haki.

Japokuwa kulikuwa na changamoto chache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…