Kwa wana CCM wacha Mungu: Je, mnaamini mmeshinda kihalali na uchaguzi ulikuwa huru na wa haki? Kila mmoja wetu atasimama mbele za kiti cha hukumu

Ndugu zangu kuna maisha baada ya maisha haya, na kila mmoja wetu atasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu. Asilimia kubwa ya Watanzania ni wacha Mungu, ndio maana naomba sana tujibu swali hili kutoka kwenye vina vya mioyo yetu.

CCM ina watu wanaomcha Mungu na wengine ni Maaskofu Wachungaji Mashehe na Mapadre. Je, ni kweli CCM ilishinda uchaguzi kwa halali? Je, uchaguzi ulikuwa huru na wa haki? Ni kweli wananchi waliichagua CCM maeneo yote nchini kwa kura nyingi hivyo? Je, vyombo vya dola havikuingilia uchaguzi na kubadilisha matokeo? Je, tume ya uchaguzi ilisimama katikati kama mwamuzi asiyependelea upande wowote?

Je, Mioyo yetu haina hatia kuhusu Uchaguzi huu?

Kumbuka kila mtu atasimama mbele za kiti cha hukumu cha Mungu.
Uchaguzi umeisha fanya kazi na shughuli za kukuletea maendeleo badala ya kupoteza muda wako.JPM ndiyo rais na serikali ni ya ccm na maendeleo kwa wananchi yanakuja.Chadema hamtawahi kupewa nchi wananchi wamewakataa.
 
Ni kweli Kuna mwenzenu alisema ushindi wa CCM ni lazima Mungu atake asitake ushindi ni lazima bahati mbaya amefariki wiki iliyopita.Hii ni picha halisi kuwa CCM kwenu MUNGU siyo chochote!
Alisema hayo kwa sababu anajua wananchi wanaikubali ccm na sera zake
 
Back
Top Bottom