Kwa wana CCM wacha Mungu: Je, mnaamini mmeshinda kihalali na uchaguzi ulikuwa huru na wa haki? Kila mmoja wetu atasimama mbele za kiti cha hukumu

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,131
2,000
Ndugu zangu kuna maisha baada ya maisha haya, na kila mmoja wetu atasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu. Asilimia kubwa ya Watanzania ni wacha Mungu, ndio maana naomba sana tujibu swali hili kutoka kwenye vina vya mioyo yetu.

CCM ina watu wanaomcha Mungu na wengine ni Maaskofu Wachungaji Mashehe na Mapadre. Je, ni kweli CCM ilishinda uchaguzi kwa halali? Je, uchaguzi ulikuwa huru na wa haki? Ni kweli wananchi waliichagua CCM maeneo yote nchini kwa kura nyingi hivyo? Je, vyombo vya dola havikuingilia uchaguzi na kubadilisha matokeo? Je, tume ya uchaguzi ilisimama katikati kama mwamuzi asiyependelea upande wowote?

Je, Mioyo yetu haina hatia kuhusu Uchaguzi huu?

Kumbuka kila mtu atasimama mbele za kiti cha hukumu cha Mungu.
 

Ryaro wa Ryaro1233

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
353
1,000
CCM Kwanza Mungu Baadae.Na wanalitaja Jina la Mungu mara Mbilimbili, tena kwa Kutetemeka. CCM wanasahau Kwa Mungu ni HAKI Kwanza AMANI ni Matunda ya HAKI. Kwa sasa Wanatuimbia Tusimame Kizalendo Kuitetea nchi wanasahau Muda uliopita Kidogo Wametoka Kuwaumiza WAPINZANI wao Na WATANZANIA Kwa Ujumla. Kwa Yaliyotokea Umoja na Mshikamano or UZALENDO ni Ndoto..
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
38,359
2,000
CCM Kwanza Mungu Baadae.Na wanalitaja Jina la Mungu mara Mbilimbili, tena kwa Kutetemeka. CCM wanasahau Kwa Mungu ni HAKI Kwanza AMANI ni Matunda ya HAKI. Kwa sasa Wanatuimbia Tusimame Kizalendo Kuitetea nchi wanasahau Muda uliopita Kidogo Wametoka Kuwaumiza WAPINZANI wao Na WATANZANIA Kwa Ujumla. Kwa Yaliyotokea Umoja na Mshikamano or UZALENDO ni Ndoto..
CCM ni adui wa kila kiumbe hapa duniani
 

Usher-smith MD

JF-Expert Member
Jul 7, 2015
8,390
2,000
Unasema?!
IMG_20201123_103414_860.JPG
 

Anatomist

Senior Member
May 16, 2020
133
250
Uchaguzi umeisha, CCM imeshinda kwa kishindo, Lissu karudi kwa mabwana zake, Mbowe, Sugu, Mdee, Zitto, Lema na wengine wengi watatafuta shughuli zingine za kufanya na sisi tuache malumbano yasiyonatija tuchape kazi.
Ni kweli Kuna mwenzenu alisema ushindi wa CCM ni lazima Mungu atake asitake ushindi ni lazima bahati mbaya amefariki wiki iliyopita.Hii ni picha halisi kuwa CCM kwenu MUNGU siyo chochote!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom