Kwa waliosoma Forodhani shule ya msingi

Kwa waliosoma Forodhani shule ya msingi

Daah! ingawa hii thread ni ya siku nyingi lakini imenikumbusha mambo mengi mazuri those days

Kwa tuliosoma Bunge p/s from 1986 - 1992, sure Moses Sarakikya alikuwa mtata, lakini alikuwa yuko vizuri kwenye somo la English nakumbuka, though
kuna wengine waliokuwa vizuri kichwani kina Harrieth Lumbanga, vipaji vya soka akina Renatus Njohole, kuwataja wachache.

Mwalimu mkuu wakati huo alikuwa Mama Masasi, msaidizi wake Mama Msafiri.

Watoto tuliokuwa tunaishi Magomeni mapipa na Mwembechai ilikuwa tukitoka shule tu, kabla ya kwenda posta mpya kupanda maikarus yetu, tunazama jengo la kitegauchumi pale, kipindi hicho ndio jengo refu kuliko yote, chezea lift sana, bonyeza vitufe mpaka ghorofa ya ngapi sijui, ilimradi siku hiyo upande lift, dah utoto wa enzi zile.

Ni jambo zuri sana kukumbuka mambo ya utotoni.

Big up sana kwa wote waliosoma Bunge wakati huo, Big up JF members kwa kuleta kumbukumbu hizi.

Mwl Masasi na Msafiri wako wapi siku hizi? Nimekumbuka mbali sana
 
Nazikumbuka zote Odeon na New chox...hiyo ya upanga pia nimesahau jina..
back in the days.....mimi huwa nalikumbuka yale majengo ya zamani ya Samora
ilio J M Mall now.....yaani dah...

Ilikuwa raha sana kwenda Drive Inn cinema halafu mnakula chips kuku kwenye gari mnachek movie.

Those good old days!
 
Sijui na ile ice cream yao ya karanga kama bado ipo...[/QUOTE

Boss hapo snow cream walikuwa na ice cream nizipendazo mimi
1.Banana split
2.Pineapple sundae
Mmenikumbusha the good old days

Snow cream imehamia mtaa wa jamhuri ila nahisi ice cream zao si tamu tena kama za enzi hizo, nimekula juzijuzi tu hapa hamna kitu
 
Mwl Masasi na Msafiri wako wapi siku hizi? Nimekumbuka mbali sana

Mkuu Stwita, kwa kweli sina taarifa za hawa Wakuu @ those days.

Nakumbuka walimu kama Mwl. Kisebengo, Mwl. Makwega, Mwl. Gowele, Mwl. Teddy (she was cute though)..to mention a few.

Dah, time flies! We r not getting any younger
 
Mkuu Stwita, kwa kweli sina taarifa za hawa Wakuu @ those days.

Nakumbuka walimu kama Mwl. Kisebengo, Mwl. Makwega, Mwl. Gowele, Mwl. Teddy (she was cute though)..to mention a few.

Dah, time flies! We r not getting any younger

Dah. Kisebengo alifanya niichukie hesabu kwa maneno yake mabaya.
 
Dah. Kisebengo alifanya niichukie hesabu kwa maneno yake mabaya.

Ooh yeah, nakumbuka baadhi yetu ilitulazimu kwenda kusoma tuition ya hesabu home kwake Upanga. Alikuwa mkali aisee.
 
Nimekumbuka yule Mchina wa keko alikuwa anaitwa winipeg kwakuwa alikuwa mchina alikuwa anajiona kama Bruce Lee!

Nimekumbuka kitu very interesting kuna Mwanafunzi nimemtaja kwa jina la Patrick akiishi kigamboni huyu jamaa alikuwa gifted kwani alikuwa anaweza kuandika kwa mikono yote miwili bila ya shida!!!
 
Ipo.

Na wafanyakazi ni wale wale wa zamani ila wamezeeka tu kwa sasa. New comers ni wachache.

Kwi kwi kwi teh teh teh

Wewe hujui chochote kuhusu snow cream!
 
Marahabaa kijana wangu

vijana mliokuwa mkisoma wakati Mwl Fadhili Saiwad akiwa mkuu wa shule mna taarifa kuwa amefariki?


dah ama kweli sote tunapita.. mwlm Saiwadi alikua mwalimu mkuu wangu kabla ya mama Chuma... Niliwahi muona mwaka jana hakua kama mwlm Saiwad niliewahi mfahamu.. Dah Mungu amrehemu kwa kweli..
 
dah ama kweli sote tunapita.. mwlm Saiwadi alikua mwalimu mkuu wangu kabla ya mama Chuma... Niliwahi muona mwaka jana hakua kama mwlm Saiwad niliewahi mfahamu.. Dah Mungu amrehemu kwa kweli..

umemaliza mwaka gani mkuu?
 
Afu mkuu spider una kumbukumbu kweli mtu wangu hongera mi wengine nimewasahau kwa majina ila ww unawakumbuka mpaka ubini wao umetisha sana mkuu ha ha haa

hahahahaha.....ila namtafuta sana bony,mathew mbago,kibacha na george mwarabu bila kumsahau mzee wa kuja na biriani,abdala.
kuna ticha aliwekewa majani ya kuwasha kwenye kiti tukiwa std 5,unakumbuka?
 
Nimesikitika sana kusikia Mwl James Alifariki,nakumbuka tuition za Jumamosi,alikuwa mkali ila alikuwa anapendwa sio kama JJ.
 
Back
Top Bottom