Dream Queen
JF-Expert Member
- Nov 4, 2015
- 8,255
- 18,047
Mwanaume mzima unaogopa chura ati nikaenda kulala kwa mshikaji,Mwaka Jana nilisafiri masika nkaenda kulima bush, basi nkakaa kama wiki mbili, Ile narudi usiku nimechoka balaa nikajitupa kitandani na viatu nkaanza kuota kama nipo mtoni naskia sauti za vyura, ila Ile sauti ikawa kama inatokea kichwani mwangu, dakika Moja nyingi nkakurupuka Kumbe frog yupo chini ya kitanda.
Yaani wenge lote la usingizi likakata nikawa najiuliza kaingilia wapi au ni wa kutumwa, nikagundua alipitia chini ya mlango palipokuwa na uwazi.
Sasa mawazo yakazidi kuwa kama kaingia chura, nyoka atashindwaje, nikatoka nikaenda lala Kwa mshkaji kesho yake nikafanya famigesheni huwezi amini Ili kuwa kama zoo ya wadudu maana walitoka wengine hata siwafahamu.
Huna hata aibu!