Kwa unayetaka kuanza project mpya na kubwa zingatia Hili utanishukuru baadae

Poqo

Member
Oct 10, 2023
30
90
Unapota kuanzisha mradi mpya na mkubwa,mradi unaomini ukiusimamia vizuri utakutoa basi huna budi kuzingatia jambo Hili la mhimu ambalo wengi Huwa tunalisahau kwenye mipango yetu,jambo lenyewe ni Hili hapa;

Kuzingatia kuwa wewe ni binadamu na unatakiwa kupata mahitaji ya msingi kama chakula,mavazi na malazi pindi mradi unavyoendelea,hivyo kwenye bajeti zako za mradi usisahau kuweka gharama za kukusaidia uishi pindi mradi unaanza mpaka utakapoanza kuzaa matunda.

Usipozingatia Hilo katikati ya mradi utajikuta unatumia fedha ya mradi na kusababisha mradi kufa au kutoleta matunda tarajiwa,na wengi wetu tunakuwa frustrated na kuanguka kabisa na Inatufanya tukate tamaa kabisa.

USHUHUDA: 2015 nilianzisha mradi wa ufugaji wa kuku wa mayai,nilipanga bajeti zangu za mradi mzima mpaka kukamilika,nikakusanya fedha nikaanza mradi,katika bajeti zangu nilisahau kabisa namna nitakavyoishi mpaka mradi utapoanza kuleta matunda, hakika nilianza mradi vizuri lakini nikajikuta natumia fedha ya mradi Kwa ajiri ya mahitaji yangu mhimu, jambo Hili lilifanya mradi kufifia maana baada ya miezi mitatu nilianza kukosa fedha ya dawa na chakula Kwa ajiri ya kuku wangu wa mayai,nilikata tamaa ya mradi wa kuku na kuanza kulaani kuwa mradi wa kuku ni mbaya na haufai.

NINI UFANYE?unapoanzisha mradi mkubwa kama huna fedha za kutosha anzisha mradi mdogo wa kukusaidia uendelee kuishi pindi mradi mkubwa unavyoendelea.
 
I was Thinking about the same thing oneday ni kama uliwaza kama mimi!

Unapotaka kuanzisha mradi mkubwa ambao unaamini utachangia kwa kiasi kikubwa basi ni lazima ujiweke katika nafasi nzuri ya ku-afford basic needs.

ili ufanye mipango yako smart basi lazima uwe na uhakika wa kula, kulipa kodi, mavazi, afya na dharura hii itaondoa stress za maisha na kukufanya u-focus kwenye project yako tu!

Kwa hiyo ni lazima uwe na project nyingine ndogo ambayo inakupa pesa ya kujikimu au akiba ya kutosha, lakini akiba sio nzuri kwa sababu kama project yako kubwa itafail na akiba ikaisha what gonna happen?

Kwahiyo ni vizuri ukawa na project ambayo inaendelea tayari.

Lakini hii kitu ina Disadvantage moja psychologically, wazungu husema ''Give a man assuarence food, shelter, clothes, sex and little entertainment and he will throw away all his ambition, comfort zone is where our dreams die''

So ili hii principle ifanye kazi lazima uwe na discipline kubwa, kwamba you keep working on your project as if you can't afford your basic needs!

Xie xie.
 
Back
Top Bottom