Hali ya SGR ni mbaya na mradi haujulikani utakamilika lini

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,829
21,460
Kampuni ya Yapi Markezi haina uwezo tena wa kifedha kuendeleza huu mradi na ni wazi kuna mambo yanafichwafichwa sana juu ya nini chanzo na nani yuko nyuma ya hili jambo baya kabisa kuwahi kutokea. Yaani hela za mradi zimeibwa halafu tunakwenda kukopa nyingine kufidia zilizoibwa!.

Mradi huu una mikopo lukuki na yote tulitangaziwa hapa na tunajua fedha zote za kukamilisha mradi huu zilipatikana zote na ili kuweka angalizo kwa watanzania tunawakumbusha kuwa huu ni mkopo na watakaolipa ni watanzania hawa masikini.

Leo mradi umesimama na mkandarasi kaweka wazi kuwa hana fedha!. tunachukulia jambo hili kiwepesi sana na kama ni jambo dogo na hakuna shida yoyote lakini leo nataka niseme kuna WIZI MKUBWA sana umefanyika kwenye huu mradi mpaka mkandarasi kakosa fedha kuendelea na mradi na kazi imesimama. Hii ni kashfa kubwa sana na hatuwezi kukaa kimya hata iweje.

Vyanzo vyetu vinasema MAJIZI hayo yakichukua hela yao "in advance" mara tu mkataba uliposainiwa na ndiyo maana Yapi Markezi wamefika mahali hela waliyotoa rushwa kwa lazima imeleta nakisi kwenye utekelezaji.

Hatuwezi kulitazama hili kirahisi tu na kuona ni jambo la kawaida na sasa tunatafuta nkopo mwingine kama nchi ili kumalizia mradi! Swali ni kuwa nani kaina fedha za mwanzo? Nani yuko nyuma ya hii michezo kiasi kwamba anaogopwa kutajwa na kushughulikiwa mpaka nchi inaingia kwenye mchakato wa kutafuta mkopo mwingine kumalizia mradi? Huyu MWIZI special hivi ni nani mpaka anapewa ulinzi wa hivi?

CAG hivi upo kweli? Yaani huu mradi kinachojufanya usiukague ni kitu gani? Bunge hivi mpo kabisa yaani na haya yanatokea mnaona sawa tu? Mnashindwa nini kutoa azimio la kumtaka CAG akague na kuweka wazi shida iko wapi?

Sisi tunajua nani yuko nyuma ya hasara hii kubwa kwa hili taifa na tunajua nguvu inatumika kumficha na kumlinda lakini watanzania hawa pamoja na ujinga wao na ulofa wao hawapaswi kupitishwa kwenye njia hii na kama vyombo husika hasa wewe CAG hamtachunguza hili basi tutawasaidia ifikapo 1 January 2024 siku ya mkesha wa mwaka mpya! (Siku hii utakuwa ni ukurasa mpya unafunguliwa)

Haiwezekani kuwatia watanzania kwenye shida ya deni jingine kubwa hivi huku tunamjua mtu aliye katikati ya haya madili na tunaogopa kumsema!. Watanzania siyo malofa na wajinga kiasi hicho hata kama wanakaa kimya.

Hatuwezi kukaa wa watu kama Kadogosa pale TRL badala ya kufanya kazi wao wako hapo kwa ajili ya kusaidia watu kuiba fedha za watanzania na wanaogopa kuwasema kwa kuwa wanataka kulinda nafasi zao na vyeo vyao na wengine wameahidiwa ubunge kama Kadogosa. Nyie kama mnawaogopa ni vizuri lakini sisi Kigogo Media hatujawahi kumuogopa mtu na hili linajulikana na tutasema waziwazi ili kila mtu ashinde mechi zake.

Watanzania kuna wizi na kashfa ya kutisha kwenye mradi wa SGR na chanzo cha Yapi Markezi kukwama kuendelea na kazi ni mabilioni ya fedha yamekwapuliwa na wakubwa wakati wa kuwapa tenda sasa hawana hela tena.
 
Kampuni ya Yapi Markezi haina uwezo tena wa kifedha kuendeleza huu mradi na ni wazi kuna mambo yanafichwafichwa sana juu ya nini chanzo na nani yuko nyuma ya hili jambo baya kabisa kuwahi kutokea. Yaani hela za mradi zimeibwa kati wa kuwapa tenda sasa hawana hela tena.
Huyu Professa daraja la Kwanza anasemaje na Waziri wa Ujenzi kabla ya haya mabadiliko ya Waziri kuwa Muheshimiwa Bashungwa anasemaje.
 
Kampuni ya Yapi Markezi haina uwezo tena wa kifedha kuendeleza huu mradi na ni wazi kuna mambo yanafichwafichwa sana juu ya nini chanzo na nani yuko nyuma ya hili jambo baya kabisa kuwahi kutokea. Yaani hela za mradi zimeibwa halafu tunakwenda kukopa nyingine kufidia zilizoibwa!.
wakubwa wakati wa kuwapa tenda sasa hawana hela tena.
Watu wakiwajibishwa na kufilisiwa mali zao kila kitu kitakuwa bayana...wala sio kuogopana ni kawaida ya maccm kuiba na kupenda 10%ndio kunatufikisha hapa tulipo . Kwanza tujiulize mchina amefikia %ngapi na ubora wake wa Kazi upoje??
 
Kampuni ya Yapi Markezi haina uwezo tena wa kifedha kuendeleza huu mradi na ni wazi kuna mambo yanafichwafichwa sana juu ya nini chanzo na nani yuko nyuma ya hili jambo baya kabisa kuwahi kutokea. Yaani hela za mradi zimeibwa halafu tunakwenda kukopa nyingine kufidia zilizoibwa!.
Ncbi ina rais na vyombo vyote vya ulinzi, usalama na figisu za kiuchumi, wana kinga dhidi ya sheria. Halafu unauliza nani yupo nyuma ya kuanguka kwa huo mradi?

Kha!
 
"NANI YUKO NYUMA YA KUFA KWA MRADI WA SGR".

Ni swali zuri sana mkuu 'peno hasegawa'.

Hili swali, kidogo lingefanana na lile ambalo sote tungejiuliza "Ni Nani Alitaka Kuuua Mradi wa Bwawa la Umeme, la Mwalimu Nyerere." Huku ikaonekana watakuwa wamejifunua kiasi kikubwa mno, hadi nyeti zao kuwa nje nje; wakaona siyo neno, wakaachia kwa shingo upande.

Kwa hiyo, ukitaka kupata jibu la maswali yote mawili, sidhani kuwa itakuwa vigumu kwako kupata jibu.

Serikali ya Samia inaendeshwa na genge linalozoa kila kitu. Genge hili halina simile na chochote, na wala halina aibu kufanya chochote linapodhamiria kukifanya.
Mfano mzuri ni wa DP World na IGA yake. Mtu mwenye uadilifu hata kidogo, hawezi kamwe kushiriki katika mpango wa aina ile.

Kwa hiyo hapa kwa SGR, tutalia sana endapo serikali ya huyu mama itaendelea kuwepo madarakani. Huo mradi itakuwa ni aibu kubwa sana kwa taifa letu.

Nikisoma yaliyo andikwa ndani ya mada hii sioni lolote la tofauti na yale mengine yooote tunayolia nayo kila siku chini ya hawa watu; lakini nimevutiwa sana na hilo swali, na nadhani ingekuwa na faida zaidi kujaribu kujibu hilo swali kwa usahihi zaidi, kuliko machozi yote haya uliyomwaga hapa.
 
Ninachojua kwasasa watu wanajenga majumba ya gharama kwa kasi sana. Mtu m'moja ana site 6 maeneo tofauti ya mikoa tofauti na zote zipo active watu wapo kazini wanajenga.

Magari ya bei namba E yamejaa barabarani, bei tunazungumzia Milioni 45+ na kuendelea hazijulikani zimenunuliwa kwa Cash au mkopo. Mfano ni zile Land cruiser 300 series mpya, saa hii zimeanza kujaa barabarani tena kwa wingi sana.

Kwa kifupi watu wanajeuri ya pesa. Na ndicho hiki kitu mlichukia magufuri mkasema ana roho mbaya kwa kuzuia watu wachache wasijineemeshe kimaisha.

So wacha tutafune hela za miradi hadi ziishe.
 
Licha ya 'mapungufu' yake ya kibinadamu, JPM alikuwa mtu kweli kweli wa kusimamia mambo yake.
Mambo hayaendi kwa uzuri, 'HAMKANI SI SHWARI TENA'
Viongozi wetu wasipoamka na kumulika mambo haya, tutazidi kuanikwa 'nyeti' zetu.
 
Mafisadi papa yanamiliki malori. Kamwe hayawezi kuruhusu SGR ikwmilike halafu biashara yao ya malori ife. Never and never ever.

Hamasi hata hapa Tanzania wapo, wao hawarushi mabomu ili kuua watu, bali wanaua kwa kula rushwa na kukwa.misha miradi kama SGR.
 
Nani kakwambia mradi umesimama!?

Mbona hamjiongezi kufatilia zaidi ya kusaka vijarida vya udaku na kuleta hapa

Mradi unaenda vizuri zaidi ya jana
 
Back
Top Bottom