Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,194
- 10,929
Kuanzia sasa meli yoyote itakayokatiza bahari nyeusi kuelekea Ukraine itachukuliwa kana kwamba imebeba silaha kwaajili ya Ukraine na inaweza kushambuliwa.
Hatua hiyo ya Urusi imekuja siku mbili tu baada ya kujitoa kwenye mkataba wa usafirishaji wa nafaka uliosimamiwa na Umoja wa mataifa pamoja na Uturuki.
Kama kuoa onyo kwa vyombo hivyo vya bahari,mara tu baada ya kusitisha mkataba huo Urusi ilirusha mabomu mengi kutoka angani kuelekea bandari ya Odessa ambayo ndiyo bahari kuu ya kusafirishia bidhaa za kilimo za Ukraine.
Naye Rais wa Ukraine, Volodomyr Zelensky katika hali ya ukaidi mara lilipotaka tangazo la Urusi kujitoa mkataba huo alisema Ukraine haijali na kwamba tayari imeshaanza mchakato wa kusafirisha bidhaa zake bila kuiangalia Urusi inataka nini.
Yahoo News