Kwa Thomas - Kimara bucha

Kwa Thomas - Kimara bucha

Raimundo

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2009
Posts
13,415
Reaction score
12,622
Kituo cha Mabasi yaendayo haraka (RBT) kinachojulikana kama Kimara - Bucha kimepewa jina la kwa Thomas, nilimuuliza jamaa yangu mmoja juu ya kwa nini wanapaita Kwa Thomas, akasema unatakiwa kuwa mwenyeji wa Dar kumfahamu huyu jamaa.

Kuna story kwamba huyu Thomas alikuwa tajiri siku za nyuma na amekuja kufirisika baada ya kuhusishwa na Mabomu yaliyolipua Ubalozi wa Marekani hapa TZ.

Nilimbishia kwa kumuuliza chanzo cha habari yake lakini hakunipa jibu mwafaka nikaona niulizie humu JF. Mwenye hizi taarifa kwa ufasaha asaidie jamani.
 
we mgeni dar? Inasemekana Ni kweli alihusishwa sababu alichonga kasha(bila kujua!)lililobeba bomu. Lakini pia inasemekana swalatano walikataa pale kuitwa bucha sababu bucha inayoitwa/tamkwa pale ni bucha kubwa na maarufu ya kitimoto. Ni bora akumbukwe Thomas Lyimo kuliko kitimoto!
 
sasa wewe unaelewesha alafu unambishie wakati unajua wewe umekuja dar mwaka jana utajifunzaje,acha ubishi usio na faida utakosa kueleweshwa mambo ya msingi ,kaka hii ndio dar na hiyo story ni kweli ila huyo jamaa hajafirisika na hatofirisika anaishi kwenye ikulu yake hukohuko kimara
 
[/COLOR]sasa wewe unaelewesha alafu unambishie wakati unajua wewe umekuja dar mwaka jana utajifunzaje,acha ubishi usio na faida utakosa kueleweshwa mambo ya msingi ,kaka hii ndio dar na hiyo story ni kweli ila huyo jamaa hajafirisika na hatofirisika anaishi kwenye ikulu yake hukohuko kimara

Unajua kuna style ya kumbishia mtu afunguke zaidi, lakini jamaa naye alikuwa anaonekana kama amesimuliwa, of course alinionyesha hadi duka la jamaa la spare za magari pale Kimara Korogwe lakini stori ilikuwa ina-hang.
 
KWA MATHIAS-KIMARA BUCHA.

Huyu Jamaa alikuwa tycoon kubwa la kichaga,ambaye alikuwa anahusika na biashara nyingi sanaa,Hakufilisiwa kwa issue ya Bomu Ubalozi wa marekani ingawa alihusika katika kujenga yale matanki ambayo mitungi ya gesi pamoja na milipuko ilijazwa ndani.Kuna Jamaa mmoja anafanya biashara Matumbi pale,ndio aliyetafuta hile mitungi ya gesi na kuwadirect kwa fundi mzuri ambaye anaweza kutengeneza matanki mazuri ambayo watabebea maji,basi MATHIAS ndiye aliyechaguliwa,Hata Gereji yake imekaa katika ukuta ambao hakuna mtu anayejua kinachoendelea ndani.
 
Kweli mji una wenyeji. Poa aisee, lakini jamaa wanasema alikuwa na hela mbaya (ya ukweli na amefirisika).
 
we mgeni dar? Inasemekana Ni kweli alihusishwa sababu alichonga kasha(bila kujua!)lililobeba bomu. Lakini pia inasemekana swalatano walikataa pale kuitwa bucha sababu bucha inayoitwa/tamkwa pale ni bucha kubwa na maarufu ya kitimoto. Ni bora akumbukwe Thomas Lyimo kuliko kitimoto!

Kwenye RED, Bucha inayotamkwa pale siyo Noah wala mbuzi katoliki bali ni kuwa pale kulikuwa na ajali nyingi sana watu wakichinjwa ni kama vile pale Chang'ombe panavyoitwa machinjioni. Hivyo si busara kuita jina hilo la kimzaha (lakini mzaha wa hatari) ndo maana waka - opt for Thomas kwani jamaa ana gereji kubwa pale, ambayo naona kama kawakodisha wachina kwa sasa.

Kuna hadithi kuwa ajali hizo zilikuwa zinasababishwa na matambiko ya huyo jamaa, ingawa ukweli ni kuwa tatizo lilikuwa ule mteremko mkali lkn binadamu wakazusha kama kawaida yao.
 
Garage yake ilihusika na kutengeneza mlipuko wa 1998 Ubalozi wa Marekani lakin uchunguzi ukaja kuonesha hawakuwa accomplice alilipwa vzur akafanikiwa kufungua na kampuni yake ya Maziwa Tommy Diary ikaja kufa amebaki na biashara yake ya awali ( Garage ).

Kuhusu majina ya vituo sio big deal sana hata pale Korogwe hapaitwi Korogwe panaitwa Resort, Rombo wamepaita Kibo so sijui km kuna internal politics.
 
Huyu jamaa alikuwa anafanya biashara nyingi ila nilizokuwa nazifaham ilikuwa dairy na garage pale bucha.

Alikuwa anatusaidia kuchonga uwanja wetu wa mpira pale Kimara Baruti P/S.

Alikuwa anatuchukua kwa ajili ya kufanya matangazo ya maziwa yake huku tunafanya jogging.
 
KWA MATHIAS-KIMARA BUCHA.

Huyu Jamaa alikuwa tycoon kubwa la kichaga,ambaye alikuwa anahusika na biashara nyingi sanaa,Hakufilisiwa kwa issue ya Bomu Ubalozi wa marekani ingawa alihusika katika kujenga yale matanki ambayo mitungi ya gesi pamoja na milipuko ilijazwa ndani.Kuna Jamaa mmoja anafanya biashara Matumbi pale,ndio aliyetafuta hile mitungi ya gesi na kuwadirect kwa fundi mzuri ambaye anaweza kutengeneza matanki mazuri ambayo watabebea maji,basi MATHIAS ndiye aliyechaguliwa,Hata Gereji yake imekaa katika ukuta ambao hakuna mtu anayejua kinachoendelea ndani.

Kwa Mathias tena.......hiyo si Kibaha mkuu
 
Unataka kujua kwamba Thomas alifilisika kweli ama unataka kujua kwamba kituo cha Kimara Bucha kimebadilishwa jina!
 
Unataka kujua kwamba Thomas alifilisika kweli ama unataka kujua kwamba kituo cha Kimara Bucha kimebadilishwa jina!

Nilitaka kujua kwa nini jina la Kwa Thomas, ana umuhimu/umaarufu gani wa jina lake kutumika kwenye kituo.
 
Nilitaka kujua kwa nini jina la Kwa Mathias, ana umuhimu/umaarufu gani wa jina lake kutumika kwenye kituo.

Sijui kwa kweli maana nakumbuka sehemu nyingi sana zenye majina ya kibaguzi ilihali waliobatiza maeneo hayo wakiwa tofauti sana na ukoloni, Mfano Uhindini,na Uzunguni Mbeya, afadhali hata mzee Mwakangale alipata shavu kukumbukwa kwenye uwanja wa nane nane pale RRM Uyole
 
Gongo la Mboto.........huyu Mboto alikuwa anauza gongo "first class" mpaka akapewa jina la mtaa!
 
Gongo la Mboto.........huyu Mboto alikuwa anauza gongo "first class" mpaka akapewa jina la mtaa!

Kuna story nyingi kama ya bwana Mussa Hassan wa Msasani ambaye baada ya jina lake kuwa gumu ikabidi lifupishwe Msa'asan. Wwngine wananiambia kuna watu fulani walikuwa wanaishi somewhere Kinondoni ambapo kulikuwa na kutokuelewana fulani kwa namna ya kulogana, sasa mtu mmoja ambaye alikuwa ni mwoga sana wa ulozi kila mwanae akilia alikuwa anambembeleza kwa kumwambia Mwana Nyamala(nyamaza) Lile eneo leo ni Mwananyamala....
 
Back
Top Bottom