Kwa Thomas - Kimara bucha

Kwa Thomas - Kimara bucha

Jamaa yupo na kile chuo cha ualimu Ebonite yeye ndio mmiliki
 
Mkuu, mpe tu heshima yake. Sema wazi tu kuwa yeye ni Form IV kielimu
Ni kweli yeye ni Form IV, na yawezekana ameisha-upgrade zaidi, nilitaka kuonyesha kuwa lolote lawezeka. pamoja na fedha zake yeye hakubweteka aliendeleza shule. Enzni hizo ukiongea naye anampaka mshikaji wake mmoja wa maeneo hayohayo ambaye aliibuka na alikuwa na mabasi ya kwenda mikoani lkn akafilisika eti kutokana na shule ndogo
 
Garage yake ilihusika na kutengeneza mlipuko wa 1998 Ubalozi wa Marekani lakin uchunguzi ukaja kuonesha hawakuwa accomplice alilipwa vzur akafanikiwa kufungua na kampuni yake ya Maziwa Tommy Diary ikaja kufa amebaki na biashara yake ya awali ( Garage ). Kuhusu majina ya vituo sio big deal sana hata pale Korogwe hapaitwi Korogwe panaitwa Resort, Rombo wamepaita Kibo so sijui km kuna internal politics.

Mkuu Mossad007 kama kumbukumbu zangu hazinipotei, huyu Jamaa Thomasi kilichompa ukwasi ni ile Biashara ya Maziwa na naona hapo umekosea uliposema kuwa alianza hii Biashara baada ya kulipwa fidia kwa issue ya U.S Embassy Bombing, hii Biashara aliianza kabla ya 1998, na moja wapo ya Asset zake zilizobaki za ukumbusho wa vibanda vyake vya maziwa vilivyotapakaa kila kona ya Dar ni lile Banda pale Round About ya Kariakoo upande wa kushoto ukiwa unatokea Kamata.
 
any way tuanzie pale mwisho wa wazee chalinze hadi kariakoo

Mkuu hakuna kinachonisikitisha kama kile kituo cha Tip Top kilipobadilishwa jina na kuitwa Bakharesa yaani ni ujinga usio na maana kabisa isitoshe huyo Bakharesa amepakuta pale pakiwa na jina hilo hilo,na nashindwa kuelewa walitumia vigezo gani kubadili majina ya hivi vituo ambavyo vinabeba kumbukumbu na maana kubwa sana kwa Wakazi wa Manzese na Dar nzima,au ndio mambo ya mlungura yametembea.
 
wakuu polen maisha aliyonayo n maombi ya wanabucha
hivi ndivyo vilivyompa umaskni
katika utajiri wake mlioona alitakiwa kutembea na dadake yuko kulia opp na garage yake wanauza matofali

wakabahatika kuzaa mtotn anaitwa deni
hivi sasa denis n bwabwa na kama unakale kamchezo hana kazi yuko pale kwa

dadake ndiealiemfilisi alipoamua kuokoka na hii ni baada ya kupata stroke c siri akuna mwana bucha aliependezwa na hli,,,toka aokoke huyu mama thomas alikwenda mrama mpaka kesho maana ndie alikuwa akimfanya ndondocha wak


la pili
kupitia utajiri wake alifanikiwa kuua wengi kwa ajali pale bucha
hali hii ilifanya wanamaombi kutembea huku wanasali toka baruti to knrogwe na kurudi wiki nzima na n ucku na moja ya maombi kama vifo hvi anahuska mungu akammalize kabsa ndipo wiki inayofata akapata ajali akiwa na kimada kwenye cruiser yake akakimbizwa uk st thomas hospt

aliporud alianza kufunga vibanda vyamaziwa hapa jijin kimoja badaya kiingne


akiwa anaendelea kufunga
msaidiz wake aitwae said ambae ndie alikuwa anamsaidia kila tenda ya bodi maana alikuwa mzuri kuongea huyu akiwa pale wale wazungu walioktxa wakimfadhli thomas machine wakampa dili atafte sehemu anzishe watamletea kila kitu hapa ndipo umaskini ulimpomjia chumban kwak

yuko na ofici nyuma ya lion hotel akahamisha watu wote waliokuwa wakienda kutengenezewa bod

mbaya wazungu wakamletea hadi wazungu wakumsaidia ndipo akachukua vichwa vyote pale bucha vilivyokuwa vikitengeneza mabodi na kuhamia kwake cnza mpaka leo
 
Mkuu bucha inayotajwa ni ya noah aka kitimoto. Ilikua opposite kabisa na lile jengo la garage la thomas lyimo.mwenye bucha aliweka bango lake karibu na barabara likiwa limechorwa ngurue mweupe na maandishi 'pork butcher'. Bucha na bango vilibomolewa wakati zinajengwa barabara mbili. Miaka ya nyuma kituo kilikua baruti na korogwe tu. Pale palikua kushuka kwa kuomba msaada tu.watu walikua wakisema msaada bucha.fika pale uliza wenyeji pale maeneo ya wafalme bar watakuambia.mi mdau maeneo hayo toka 1984
Kwenye RED, Bucha inayotamkwa pale siyo Noah wala mbuzi katoliki bali ni kuwa pale kulikuwa na ajali nyingi sana watu wakichinjwa ni kama vile pale Chang'ombe panavyoitwa machinjioni. Hivyo si busara kuita jina hilo la kimzaha (lakini mzaha wa hatari) ndo maana waka - opt for Thomas kwani jamaa ana gereji kubwa pale, ambayo naona kama kawakodisha wachina kwa sasa.

Kuna hadithi kuwa ajali hizo zilikuwa zinasababishwa na matambiko ya huyo jamaa, ingawa ukweli ni kuwa tatizo lilikuwa ule mteremko mkali lkn binadamu wakazusha kama kawaida yao.
 
Pale pia kulikuwa na Baa maarufu ya John Ngogo (Marhum) RUAHA GALLAXY!
yeah! Wakiwa na Ruaha Discoteque enzi hizo! Wafalme bar ipo chini kidogo ya ruaha galax kama unaenda mjini,wafalme kalikua kabaa kadogo lakini maarufu kwa kutengeneza kitimoto.
 
Aiseeee mngejua mnatupa ufajamu tiokuja na mbio za mwenge hebu endeleenj basi
 
Mkuu bucha inayotajwa ni ya noah aka kitimoto. Ilikua opposite kabisa na lile jengo la garage la thomas lyimo.mwenye bucha aliweka bango lake karibu na barabara likiwa limechorwa ngurue mweupe na maandishi 'pork butcher'. Bucha na bango vilibomolewa wakati zinajengwa barabara mbili. Miaka ya nyuma kituo kilikua baruti na korogwe tu. Pale palikua kushuka kwa kuomba msaada tu.watu walikua wakisema msaada bucha.fika pale uliza wenyeji pale maeneo ya wafalme bar watakuambia.mi mdau maeneo hayo toka 1984

Labda zote mbili zimechangia kwani ukipita maeneo ya Veterinary Temeke kuna kituo chaitwa kwa fundi umeme, simulizi zilizopo zasema kuwa kuna jamaa alitaka kuiba nyaya za umeme kwenye nguzo akanasa akafia pale pale ndo watu kwa utani wakapaita kwa fundi umeme, lakini siku hizi pia pale kuna bango la jamaa anaitwa fundi umeme na kweli anatoa huduma hizo. Hivyo wengine watasema ni huyu wengine ni yule. Back to the point nami pia ni mdau wa maeneo hayo tangia miaka ya 88.

Kuna siku "Chai maharage" ilichinja watu kibao baada ya kuingia kwenye mtaro, palikuwa hapatamaniki. Baada ya watu kuwa wameondolewa kija mmoja alisisitiza kuwa girlfriend wake bado yupo kule chini ya ile gari ambayo ilikuwa nyanganyanga. Na kweli baada ya kuinua kwa msaada wa gari nyingine binti yule alioneka. Watu wengi walisema ndo maana paitwa bucha - maana watu wananchinjwa.

Pia ikumbukwe kuwa kulikuwa na madai kuwa ajali hizo zilisababiswa na yeye ktk kutafuta / kulinda mali zake, ingawa mimi najua ni kutokana na mteremko ukitokea pande zote mbili kwani madereva wanajisahau. Hivyo yawezekana scenario zote mbili zinachangia ama jamaa baada ya kusikia panaitwa bucha huku kukiwa na tuhuma dhidi yake basi akaanzisha bucha ili kiuzipotezea tuhuma hizo.
 
Pdidy;

Story yako iko very interesting, ila nimetumia nguvu sana kuisoma, maana kuna maneno duh! Ukipata muda jaribu kui-edit kaka.

Duh! Biashara si mchezo.
 
Last edited by a moderator:
we mgeni dar? Inasemekana Ni kweli alihusishwa sababu alichonga kasha(bila kujua!)lililobeba bomu. Lakini pia inasemekana swalatano walikataa pale kuitwa bucha sababu bucha inayoitwa/tamkwa pale ni bucha kubwa na maarufu ya kitimoto. Ni bora akumbukwe Thomas Lyimo kuliko kitimoto!
....Hivi na ule mjengo uliopo pale kimara sijui ndio wanaita korogwe uande wa kushoto kuelkea Moro unaodaiwa kuwa ndio ilikuwa garage yenyewe bado analimiliki au FBI walipiga stop kutumika tena?
 
Mkuu hakuna kinachonisikitisha kama kile kituo cha Tip Top kilipobadilishwa jina na kuitwa Bakharesa yaani ni ujinga usio na maana kabisa isitoshe huyo Bakharesa amepakuta pale pakiwa na jina hilo hilo,na nashindwa kuelewa walitumia vigezo gani kubadili majina ya hivi vituo ambavyo vinabeba kumbukumbu na maana kubwa sana kwa Wakazi wa Manzese na Dar nzima,au ndio mambo ya mlungura yametembea.
...Pale kulikuwa na ice cream parlour ya Bakharesa na kwa wakati ule wa Enzi za giza ilikuwa rahisi mtu kuelekezwa kwa jina la Bakharesa. Ingawa pia kulikuwa na hata bucha za "Noah" miaka ile kabla ya mtifuano wa wanaharakati pangeweza pia kuitwa kituo cha "Noah"..
 
Umenena vema mkuu. Sasa utamsaidiaje kuhusu hilo toto ili lijirekebeshe ili liweze ku run miradi ya baba yake isife kama ikitokea baba "akapumzika" maana si familia tu inayonufaika na miradi ya mzee Thomas maana ametoa ajira kwa watu wengi ambao maisha yao yanategemea kuwepo kwa miradi yake. Miradi ikifa maana yake ni kuwa ajira zinapotea
The chances are, mzee akiondoka basi he will go with a big chunk of his projects.

Lijamaa linasema likifa, ile garage itajaa watoto wake wa nje........lakini halijawahi kutambulisha watoto wa nje ndani ya familia yake. Linasema limemalizana nao juu kwa juu, kwa maana ya kwamba watoto na amam zao wanajitegemea huko walipo.

Huyo ndo Thomas...ana Mercedes Benz 5 amepark nyumbani na garage zimeshajifia +other cars like 20, zote ame-park na zimeshakufa kwasababu hataki mtu aguse wala hataki kuuza.
 
Pale pia kulikuwa na Baa maarufu ya John Ngogo (Marhum) RUAHA GALLAXY!
Hahahahahaaaaa!!..........Ewaaaaa.

Sasa pale, wale wahudumu wote wanawake wameshakufa isipokuwa moja tu - anaitwa mama Sadiki kama sikosei, hakuwahi kujua kusoma wala kuandika mpaka leo hii. Dogo amecukua ile bar, ameamua kumstaafisha bibi, amemfungulia genge. na amemwambia awe anakuja kunywa bia mbili kila jumapili. Huyo maza hawezi hata kurudisha chenchi lakini amekuwa mhudumu wa Ruaha Galaxy kwa maisha yake yote...tangu usichana wake mpaka amekuwa bibi.

Namkumbuka sana......akiniona ananiita .......mwanangu siku hizi umeacha kunywa Kilimanjaro..duh....hahahahahaaa!!
 
The chances are, mzee akiondoka basi he will go with a big chunk of his projects.

Lijamaa linasema likifa, ile garage itajaa watoto wake wa nje........lakini halijawahi kutambulisha watoto wa nje ndani ya familia yake. Linasema limemalizana nao juu kwa juu, kwa maana ya kwamba watoto na amam zao wanajitegemea huko walipo.

Huyo ndo Thomas...ana Mercedes Benz 5 amepark nyumbani na garage zimeshajifia +other cars like 20, zote ame-park na zimeshakufa kwasababu hataki mtu aguse wala hataki kuuza.

Sijui kwanini wengine huwa wanabarikiwa zaidi ya mahitaji yao wakati wengine hawapati hata robo ya mahitaji yao?
 
Back
Top Bottom