Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,488
- 13,608
Kuna watu hapa JF wanakariri habari za miaka ya nyuma halafu wanazileta sasa bila ya kujua nini haswa wanachokiandika.
Ni hawa wanaopenda kuandika habari za nchi kuibiwa, na habari za ndege kuonekana huko maporini. Hawa kuna mahali hawaelewi labda hawafahamu kuwa TZ ya sasa imenunua rada nne zinazotumika kuilinda nchi nzima kwa ujumla wake.
Bilioni takriban 67 zilitengwa na serikali ya awamu ya tano ya hayati JPM na zikanunuliwa rada nne kutoka kampuni moja ya Ufaransa, zikafungwa na zinafanya kazi ya kuilinda nchi.
Hakuna kinachoingia ndani ya anga la TZ kisionwe na rada hizo, hakipo kwa sasa na siku zijazo. Faida nyingine ya rada hizo ni kuongeza pato la taifa. Kila ndege inayokatiza katika anga letu inatazamwa moja kwa moja na mamlaka ya anga halafu invoice inatumwa kwa mamlaka ya anga ya nchi ambayo ndege inatoka.
Anga letu ni mali yetu kwa asilimia mia moja tofauti na miaka ile ambayo Paul Kagame alidhani anatuzidi akili alipo hodhi sehemu ya magharibi ya anga wakati sisi tupo tu.
Wanaoleta nyuzi za kichonganishi kwa kusema ndege zinatua huko porini waje na taarifa sahihi na zilizokamilika waachane na hizi kasumba za kufanya siasa nyepesi za kichonganishi.
Kwa sasa hakuna ndege inayoweza kutua ndani ya JMT bila ya kuonwa na mamlaka ya anga, hakipo kitu hicho. Hizi sio nyakati za zile ndege za kwenda mgodini kuchukua dhahabu kila alhamisi, zama hizo zimebakia historia.
JPM anaweza kuonekana hakufanya la maana, lakini ametuachia msingi mzuri wa kuipeleka nchi hii katika uchumi wa kati na ule wa juu zaidi. Aendelee kupumzika kwa amani.