Kwa staili hii, CHADEMA itavunja muungano

Bora uvunjike hata kesho . Wazanzibari hatuutaki MUUNGANO wa kiini macho. Hongera Kamanda Lissu uzi huo huo mpaka kieleweke.

hotuba Lissu imejaa uchochezi, unafiki na ubaguzi hatuwezi kuacha taifa lisambaratike kwa upuuzi wa mtu mmoja haifai kuungwa mkono. vinginevyo wanaounga mkono wanafikiri kutumia makalio.

hotuba Lissu imejaa uchochezi, unafiki na ubaguzi hatuwezi kuacha taifa lisambaratike kwa upuuzi wa mtu mmoja haifai kuungwa mkono. vinginevyo wanaounga mkono wanafikiri kutumia makalio.

Kaoge kwanza upate nguvu maana bado asubuhi sana,inawezekana pombe za jana bado azijatoka.

Nimemsikiliza kwa makini sana waziri kivuli wa wizara ya katiba na sheria Mh. Tundu Lissu.

Nilisikitishwa sana na kauli ya Lissu kwamba Zanzibar iamue ni aina gani ya muungano wanataka enda

po wataendelea kuwa kwenye muungano. Hii ni kauli hatari kwa maslahi ya taifa letu. Mwalimu alishawahi kusema kwamba viongozi walifilisika hutafuta kujihalalisha kwa makundi.

Chadema inataka kujihalalisha kwa upuuzi wa utanganyika, tuwakatae hao jamani!

Hahahaa, umeandika upupu...magamba bwana kazi kufikilia kwa kutumia masaburiii

Muungano unalalamikiwa sana na wazanzibar kuliko Watanganyika. Kuwauliza wazanzibar na watanganyika kama bado wanaupenda Muungano, tatizo liko wapi?.
Pili, Muungano haukuwashirikisha watanzania(watanganyika na wazanzibar wote) wakati unaundwa. Kuwauliza watanzania wote sasa, tatizo liko wapi?
Tatu, hata kama ungekuwa umewashirikisha vizuri watanzania wakati huo, kama baada ya miaka kadhaa wameuchoka na wanataka kubadili baadhi ya vipengele, tatizo liko wapi?
Mwisho, Turudi kwenye Msingi, kama nchi mbili ziliungana ( Tanganyika na Zanzibar) na kuwa nchi moja (Tanzania), inakuwaje tena kuwe na Zanzibar, bila Tanganyika? Hii fomula ya 1+1 = 2 ktk masuala ya Muungano ni sera ya CCM, siyo Chadema. Tundu Lissu yuko sahihi kwa mujibu wa sera ya Chadema kuhusu Muungano.

Sio dhambi ya Mtanganyika au Mzanzibari yeyote kujadili kujitoa au kuangalia aina ya muungano wetu....Scotland na England waliiungana zaidi ya miaka 150 ilyopita lakini chama cha MSP kinapigania kujitoa na wananchi wamewachagua kuunda serikali kule Scotland. Mtanzania yeyote ana haki ya kusema muungano wetu unafaa au haufai siku zote waamuzi ni wanainchi kwenye kura za maoni au kuchagua wale wanaopigia kampeni ya kujitenga...." Muungano huu ni sawa saw na koti saa yoyote nikichoka nitalivua...Mzee Karume 1971"

Nimemsikiliza kwa makini sana waziri kivuli wa wizara ya katiba na sheria Mh. Tundu Lissu.

Nilisikitishwa sana na kauli ya Lissu kwamba Zanzibar iamue ni aina gani ya muungano wanataka enda

po wataendelea kuwa kwenye muungano. Hii ni kauli hatari kwa maslahi ya taifa letu. Mwalimu alishawahi kusema kwamba viongozi walifilisika hutafuta kujihalalisha kwa makundi.

Chadema inataka kujihalalisha kwa upuuzi wa utanganyika, tuwakatae hao jamani!

kwani we ulitakaje mkuu !

kwahiyo unashauri kidumu chama cha mapinduzi?ama sijakuelewa

Nimemsikiliza kwa makini sana waziri kivuli wa wizara ya katiba na sheria Mh. Tundu Lissu.

Nilisikitishwa sana na kauli ya Lissu kwamba Zanzibar iamue ni aina gani ya muungano wanataka enda

po wataendelea kuwa kwenye muungano. Hii ni kauli hatari kwa maslahi ya taifa letu. Mwalimu alishawahi kusema kwamba viongozi walifilisika hutafuta kujihalalisha kwa makundi.

Chadema inataka kujihalalisha kwa upuuzi wa utanganyika, tuwakatae hao jamani!

Nafikiri hujamuelewa Lissu.

Amesema ni wajibu wa wananchi wa pande zote mbili kuamua kama wanataka muungano na kama wanautaka basi ni wa aina gani. Soma hutuba yake vizuri.

Na alienda mbali zaidi kwa kusema Zanzibar walifanya mabadiliko ya katiba hawakuwashirikisha watu wa Bara. Sasa na vile vile Bara walkifanya marekebisho ya katiba yao hususan kwa mambo yasiyohusu muungano hawataki waZnz wawaingilie. Na wanapojadili mambo ya muungano hapo ndio wote washiriki na lazima kura ipigwe na kila upande 2/3 ya watu wake wayakubali ndio hoja ipite.

Kwa maana hiyo alimaanisha kuwe na Serikali Tatu, yaani Serikali ya TGN, SMZ na TZ. Na hicho ndio wa Znz wanachokitaka sio kama ilivyo sasa. Soma maoni ya WaZNZ hapo chini
Na Mwinyi Sadallah, ZanzibarWakati leo Watanzania wanaadhimisha miaka 45 ya Muungano, Kiongozi Mwandamizi katika Ofisi ya Waziri Kiongozi, Enzi Talib Aboud ameshauri serikali ya Tanganyika irudishwe ili iweze kusimamia mambo yasiyokuwemo katika orodha ya mambo ya Muungano kwa upande wa Tanzania Bara.
Alitoa tamko hilo alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu Zanzibar katika Muungano kwenye kongamano la kitaifa lililofanyika jana mjini hapa.

Akiwasilisha mada hiyo kwa Niaba ya Enzi, mwanasheria maarufu Zanzibar, Ali Omar alisema Serikali ya Tanganyika ina umuhimu wa kurudishwa kwa vile itapata nafasi ya kusimamia mambo yasiyokuwa ya muungano kwa upande wa Tanzania Bara kama ilivyo hivi sasa kwa upande wa Zanzibar.

Aidha alisema wakati umefika Baraza la Wawakilishi Zanzibar lipewe nafasi ya kuridhia mkataba wa Muungano uliofikiwa Aprili 26, 1964 baina ya hayati Baba wa Ttaifa Mwalimu Nyerere na hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Alisema baada ya kufikiwa kwa Muungano mwaka 1964, Baraza la Kutunga Sheria la Zanzibar ambalo lilikuwa ni Baraza la Mapinduzi halikupewa nafasi ya kuridhia Muungano huo.

“Lazima Baraza la kutunga sheria la Zanzibar kwa sasa ambalo ni Baraza la Wawakilishi lipewe nafasi ya kuridhia mkataba huo ili kuupa uhalali wa kisheria kwa upande wa Zanzibar,“ alisema Enzi katika mada yake iliyowasilishwa na mwanasheria Ali Omar.

Alisema katika kutatua kero za Muungano mkataba wa Muungano upitiwe upya na kurekebishwa maeneo ambayo yalikuwa na utatanishi baina ya pande mbili za Muungano.

Enzi ambaye ni mwandishi wa habari mkongwe nchini alisema, ili kuondosha mivutano ndani ya Muungano, Zanzibar inapaswa kuruhusiwa kunufaika na misaada ya kibajeti ya moja kwa moja na iwe na utambulisho wake wa kidola na utambulisho wake katika duru za kimataifa ili iweze kujimudu kiuchumi na kufanikisha mpango wa kuondoa umasikini kwa wananchi wake.

“ Zanzibar ipate haki zake zote za misaada, utambulisho wake wa kidola na uwakilishi wake katika duru za kimataifa,“ alisema.

Alisema orodha ya mambo ya Muungano hivi sasa inaongezeka kutoka mambo 11 yaliyomo katika orodha ya awali ya Muungano hadi 38 na kusababisha kutoka pande mbili za Muungano kwa vile baadhi ya maeneo yaliyoongezeka yamekuwa kikwazo katika nyanja za kiuchumi.

“Muundo wa serikali mbili umepelekea wengi kuamini kwamba kilichofanyika ni kiini macho tu kwani ni Zanzibar iliyokabidhi sehemu muhimu ya mamlaka yake mahusiano ya nchi za nje, ulinzi na usalama, uraia, kodi na sarafu kwa Tanganyika na kisha Tanganyika ikajigeuza jina na kujiita Jamhuri ya Muungano,“ alihoji Enzi katika mada yake.

Hata hivyo, alisema hakuna awezae kubisha kuwa Muungano tangu kuasisiwa kwake umejengeka kutokana na misingi ya hofu, kutiliana shaka na kutoaminiana baina ya pande mbili za Muungano huo.

Wakichangia mada hiyo wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbali mbali vya Zanzibar na viongozi kutoka vyama vya CUF, CCM, NCCR-Mageuzi, UPDP pamoja na watafiti akiwemo Profesa Abdul Sharrif ambao walishauri kero za Muungano zitafutiwe ufumbuzi kwa muda muafaka.

Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini UPDP, Haji Othman Haji alisema kasoro kubwa iliyofanyika katika muungano ni kufikiwa kwa Muungano wenyewe kabla ya kushirikishwa wananchi wa pande mbili za Muungano.

Hata hivyo alisema matatizo ya muungano yataondoka kwa kujadiliwa kwa uwazi na kuwepo kwa nia njema ili kuhakikisha umoja wa kitaifa kuendelea kudumishwa chini ya mfumo wa muungano.

Hata hivyo Ali Mohammed Said alisema wakati umefika kuungalia muungano wenyewe kabla ya kuangalia kero za muungano kwa kile alichodai kuwa Muungnao umechangi kwa kiwango kikubwa kuathiri sekta ya uchumi visiwani.

Naye Profesa Abdul Sharrif ambaye ni mtaalamu wa mambo ya historia alisema hivi sasa wananchi wamegawanyika makundi mawili wapo wanaosema Muungano uvunjwe na uundwe upya na wengine wakiamini ipo nafasi ya kutatua kasoro za Muungano kwa lengo la kuimarisha umoja wa kitaifa.

· SOURCE: Nipashe

Hahaha, tena anatumia kitu cha malawi, rejao usije harisha humu ndani maana hiyo bangi inauwa valvu ya mlango wa masaburii

Hahahahaha!hi kali!Rejao aharishe mara ngapi wakati uharo mpaka kinywani!valvu zote za masaburi tayari zimeshaachia!hahahahaha

Muungano bado ni suala linalohitaji mjadala wa kitaifa kwani si majibu yote yamepatikana...kama pande zote bado zahitaji muungano basi naamini majibu ya kero zilizopo yatapatikana na muungano utazidi kudumu.
binafsi naupenda muungano.

sidhani kama mjadala wa muungano utakuwa na maana kwa vile muungano wengi wanavyouelewa hauko hivyo

umeleta maada bila kufikiri ......wewe unachuki na lisu? matatizo ya muungano huyajui? umesoma katiba ya zanzibar ...aliyechana muswad pale zanzibra mbele ya six alikuwa wa chadema? shame

Muungano unalalamikiwa sana na wazanzibar kuliko Watanganyika. Kuwauliza wazanzibar na watanganyika kama bado wanaupenda Muungano, tatizo liko wapi?.
Pili, Muungano haukuwashirikisha watanzania(watanganyika na wazanzibar wote) wakati unaundwa. Kuwauliza watanzania wote sasa, tatizo liko wapi?
Tatu, hata kama ungekuwa umewashirikisha vizuri watanzania wakati huo, kama baada ya miaka kadhaa wameuchoka na wanataka kubadili baadhi ya vipengele, tatizo liko wapi?
Mwisho, Turudi kwenye Msingi, kama nchi mbili ziliungana ( Tanganyika na Zanzibar) na kuwa nchi moja (Tanzania), inakuwaje tena kuwe na Zanzibar, bila Tanganyika? Hii fomula ya 1+1 = 2 ktk masuala ya Muungano ni sera ya CCM, siyo Chadema. Tundu Lissu yuko sahihi kwa mujibu wa sera ya Chadema kuhusu Muungano.

Serikali ya Tanganyika ina umuhimu wa kurudishwa kwa vile itapata nafasi ya kusimamia mambo yasiyokuwa ya muungano kwa upande wa Tanzania Bara kama ilivyo hivi sasa kwa upande wa Zanzibar.
Aidha wakati umefika Baraza la Wawakilishi Zanzibar lipewe nafasi ya kuridhia mkataba wa Muungano uliofikiwa Aprili 26, 1964 baina ya hayati Baba wa Ttaifa Mwalimu Nyerere na hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Kwani baada ya kufikiwa kwa Muungano mwaka 1964, Baraza la Kutunga Sheria la Zanzibar ambalo lilikuwa ni Baraza la Mapinduzi halikupewa nafasi ya kuridhia Muungano huo.
"Lazima Baraza la kutunga sheria la Zanzibar kwa sasa ambalo ni Baraza la Wawakilishi lipewe nafasi ya kuridhia mkataba huo ili kuupa uhalali wa kisheria kwa upande wa Zanzibar.

Muungano wenu ni batili na Tindu ameliona hilo. Hongera sana Tindu Lissu

Back
Top Bottom