Tatizo ni kwamba, muundo wa muungano haujakaa kueleweka na wanamuungano (yaani watanzania), na siri ya muungano kuwa hivyo nadhani wanayo wachache.hili lisipowekwa sawa litaendelea kuzua maswali na watu kuendelea kuuchokonoa mpaka hapo itakavyowekwa hadharani sababu ya kuwa hivyi. na nadhani kuna upande labda unanyonywa na ndiyo sababu ya kutoweka mambo hadharani. lah sivyo wataendelea kutumia ubabe tu kuzuia hoja za watu lkn kelele za muungano hazitaisha. yawezekana nia ni nzuri, lkn kwa nchi yenye wananchi waliopoteza imani kwa viongozi wao kama tanzania, si rahisi watu kumeza bila kutafuna kama inavyolazimishwa kumeza bila kutafuna.kama nia ni nzuri kwa manufaa ya pande zote, sidhani kama kuwa watu wataendelea kuuchokonoa.