Uchaguzi 2020 Kwa Siasa za Rais Magufuli mtu kama Lissu ndio anafaa kupambana naye. Lissu hana cha kupoteza tena hivyo hana hofu ya kumkabili jino kwa jino

Lissu anahitaji support kubwa nyuma yake kutoka kwa wale wanaoangalia safari yetu huko mbele na vizazi vyetu. Ikiwa tunataka kupata mfumo wa viongozi na sio watawala Tanzania.

Tusiangalie itikadi zetu, tujiunge kwa pamoja kumsaidia kamanda Lissu. Tupate nchi yenye mifumo mizuri ya sheria hata ikitokea Kingwendu anakua Rais ataweza kutuongoza.
sikuizi vijana wengi wapuuzi wapo CCM kusaka nyazifa
 
Kabisa, tunataka mifumo ya taasisi imara na sio mtu imara. Tukiwa na taasisi imara mtu yeyote mwenye sifa za kuwa rais ataongoza kwa mafanikio makubwa. Tunahitaji taasisi zenye uwezo wa kutoa dira ya mwelekeo wa nchi, zenye uwezo wa kumwajibisha yeyote hata kama ni rais.

Tunahitaji utawala wa sheria utakaosimamiwa na hizo taasisi imara. Tunahitaji kuishi kwa kuhofia sheria inasemaje na sio hofu ya kumuogopa mtu.
Mnahotaji taasisi imara na yenye kufuata sheria, ni chama gani Cha upinzani Hapa Tanzania ambayo ni taasisi imara, Huwezi kutegemea taasisi imara kwenye vyama ambavyo siyo taasisi imara
 
Magufuli hata kaa akanyage Ulaya na USA..sababu ukifika tu ukimalizana na Rais mwenyeji ni LAZIMA kuna press lazima uzi face utake usitake..

Sasa hayo maswali yanaweza mpeleka mtu mochware.
Umeongea ukweli mtupu, akikanyaga kule lazima abanwe na maswali. Na ndugu paschal Mayala anafahamu vizuri uwezo wa ndugu yetu vizuri ktk hiyo nyanja.
 
Mnahotaji taasisi imara na yenye kufuata sheria, ni chama gani Cha upinzani Hapa Tanzania ambayo ni taasisi imara, Huwezi kutegemea taasisi imara kwenye vyama ambavyo siyo taasisi imara
Umeandika tu ilimradi uonekane umeandika au? Kwa hiyo chama kama sio imara basi nchi haitakiwi kuwa na taasisi imara? Mambo mengine kama ni mazito kwa ubongo wako kuyaelewa ni bora kukaa kimya.
 
Umeandika tu ilimradi uonekane umeandika au? Kwa hiyo chama kama sio imara basi nchi haitakiwi kuwa na taasisi imara? Mambo mengine kama ni mazito kwa ubongo wako kuyaelewa ni bora kukaa kimya.
Kwahiyo tutegeme kuvuna maembe kwenye mchungwa. Toa boriti kwenye jicho lako kwanza
 
Kwahiyo tutegeme kuvuna maembe kwenye mchungwa. Toa boriti kwenye jicho lako kwanza
Wewe jamaa nakupuuza rasmi. Inaonekana unajua kusoma, kuandika na kuhesabu tu. Unachokiandika kinaakisi uelewa wako. Kujibishana na wewe ni sawa na kuongea na mtoto wa miaka 3.
 
Lissu anahitaji support kubwa nyuma yake kutoka kwa wale wanaoangalia safari yetu huko mbele na vizazi vyetu. Ikiwa tunataka kupata mfumo wa viongozi na sio watawala Tanzania.

Tusiangalie itikadi zetu, tujiunge kwa pamoja kumsaidia kamanda Lissu. Tupate nchi yenye mifumo mizuri ya sheria hata ikitokea Kingwendu anakua Rais ataweza kutuongoza.
Hii ni akili kubwa sana,hongera dada yangu,umeniongezea kitu asubuhi hii.
 
Kabisa, tunataka mifumo ya taasisi imara na sio mtu imara. Tukiwa na taasisi imara mtu yeyote mwenye sifa za kuwa rais ataongoza kwa mafanikio makubwa. Tunahitaji taasisi zenye uwezo wa kutoa dira ya mwelekeo wa nchi, zenye uwezo wa kumwajibisha yeyote hata kama ni rais.

Tunahitaji utawala wa sheria utakaosimamiwa na hizo taasisi imara. Tunahitaji kuishi kwa kuhofia sheria inasemaje na sio hofu ya kumuogopa mtu.
Wakufanya hivi?!
 
Lissu ndio hasa kisiki cha mpingo cha kupambana na Jiwe. Hata wapiga kura watakuwa majasiri wa kudai haki yao endapo wataporwa ushindi wao.

Wakina Membe na wengineo wampishe Lissu kwa huu Uchaguzi maana hawana uwezo wa kupambana na Siasa za kibabe za jiwe. Lissu hasa ndio pekee anayeweza kwenda sambamba na midundo ya Jiwe.
Kwa ulichokiandika unamaanisha kuwa Tundu Lissu anauwezo wa kupambana na JPM kwenye ukumbi wa ngumi au wa siasa.
Tuache utani JPM kwanza afanye siasa vipi wakati tayari yeye pekee ni political brand na siasa zake ni nimefanya A,B,C na naenda kumalizia D,E,F,G, n.k kwasababu tayari Mazingira ya kukamilisha niliyoyaahidi tayari nimeyatengeneza Mfano
1. Watumishi hewa Kwisha habari yake.
2. Vyeti Feki kwisha habari yake.
3. Siasa za uongo na ulaghai kwisha habari yake.
4. Watumishi kudharau Wananchi kwisha habari yake.
5. Mihimili kuheshikiana imeimarika.
6. Uharifu umepungua
7. Uropokaji na upotoshaji kwa kisingizio cha haki kwisha habari yake, ukipotosha lazima uthibitishe kwa mujibu wa sheria.
8. Wizi wa Madini na Maliasili ikiwemo Ardhi zilipendwa n.k.
Njoo kwa Tundu Lissu
Hoja 1. Nilipigwa Risasi na Watu wasiojulikana. ( Anasahau kama alipigwa na wanaojiita Kamati ya uhamasishaji/Redbrigade wanaolinda nafasi ya Mwenyekiti).
Hoja 2. Nitavunja Muungano kwa Maslahi ya Wazanzibar ( Anasahau zaidi ya anaowaita Wazanzibar wote tumekuwa koo moja na tunafamilia kubwa kwasababu sote ni Watanzania).
Hoja 3. Nitapandisha Mishahara: Wakati Watumishi wanapata nyongeza ya mshahara ambayo ni Siri ya Mtumishi ili kulinda uwezo wa kununua bidhaa mshara wa Mtumishi (Purchasing power).
Hoja 4. Kuminya Demokrasia: Wakati hata Mwenyewe kutwa anafanya siasa na anataka kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Urais, Ubunge na Udiwani. Hoja yake ni ya kulialia wakati ni uongo.
Hoja 5. Uminywaji wa haki ya habari: Wakati hata yeye hiyo habari anaifikisha kutwa kwa Wananchi kutumia Vyombo vya habari.
Kwa ujumla hoja za kulaumu na kulialia , Atasahau kama Mbowe alibadili katiba na kuwa Mwenyekiti wa kudumu wa Chadema, Mwenyekiti ameshawishi waliokuwa wanampinga wafukuzwe uanachama na kuwaita wasaliti, Ili uwe Mbunge Chadema lazima ukubali kukatwa mshahara na posho na Mwenyekiti n.k.
Matumizi ya Ruzuku ya Chadema haieleweki.
Mwenyekiti kila siku eti amekikuposha Chama. ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€ duuuuuu lazima Mtu ajikojoleeeee na kutonesha kidonda alichoshughulikiwa na kikosi Maalum cha Mbw.
 
Lissu ndio hasa kisiki cha mpingo cha kupambana na Jiwe. Hata wapiga kura watakuwa majasiri wa kudai haki yao endapo wataporwa ushindi wao.

Wakina Membe na wengineo wampishe Lissu kwa huu Uchaguzi maana hawana uwezo wa kupambana na Siasa za kibabe za jiwe. Lissu hasa ndio pekee anayeweza kwenda sambamba na midundo ya Jiwe.
Wapinzani mnapoteza muda tu. Magufuli ni mshnd tayari
 
Kwahiyo hoja ni kupambana na Magufuli na siyo Kuweza kutatua changamoto za wananchi
Million 50 kila KIJIJI Ahadi haijatimia hadi sasa

Ajira hakuna ukilinganisha na IDADI ya WAHITIMU kila mwaka

BUNGE halipo LIVE mwaka wa 5 sasa hatuna UELEWA wa KUTOSHA kuhusu MIRADI WANAYOISIFIA kila KUKICHA

TUWE SERIOUSLY Tz NI YETU SOTE
 
Lissu ndio hasa kisiki cha mpingo cha kupambana na Jiwe. Hata wapiga kura watakuwa majasiri wa kudai haki yao endapo wataporwa ushindi wao.

Wakina Membe na wengineo wampishe Lissu kwa huu Uchaguzi maana hawana uwezo wa kupambana na Siasa za kibabe za jiwe. Lissu hasa ndio pekee anayeweza kwenda sambamba na midundo ya Jiwe.
hqdefault-1.jpg

Jr
 
wanaweka jiwe tunaweka chuma aiseeeee tutaelewana tu.....Naskia lumumba hapakaliki now days
 
Back
Top Bottom