Kwa sasa mbali na kwamba ninakipato, lakini kipato changu kinaishia kwenye kula tena kwa kukatisha milo, Je,lipi bora, nilipe ada tufe au tule tuish

Paulsylvester

JF-Expert Member
Oct 15, 2021
1,467
3,381
Kwa jinsi ilivyo kwa sasa, huwenda nawakilisha wananchi wengi mamilioni kwa mamilioni wenye swali kama hili

Maisha yamekuwa ghali sana kushinda vipato vyetu,

Wengi wetu, vipato vyetu haviruhusu kucheza mbali na kula tuu, na hapo ni kwa kukatisha Milo, kama mtu kwa kipato hikihiki ambacho tulikitumia miaka michache iliyopita kwa kula na kulipia ada za watoto na mambo mbalimbali ya kifamilia, Leo kipato hikihiki, kinatulazimisha kufuta karibu mambo mengi ya mhimu na ya lazima

Kipato hiki kwa sasa, kinakulazimisha ukitumie kula tuu, usilipe ada na wala kufanya vitu vingine,

Swali najiuliza, mambo yanapokuwa hivi, ni kipi bora cha kufanya kuzingatia na mahitaji ya mhimu

Ulipie ada watoto ili ikiwezekana mfee, au bora mtumie kwa kula na watoto wasiende shule?

Je, serikali watatuelewa?

Na Je sasa, Serikali wanalifahamu hili kwamba wazazi wengi sana wanadaiwa huko mashuleni na uwezo wa kulipia ada watoto umeshuka na hswajui ni lini watalipa madeni yao?

Inapokuwa hivyo, serikali huyatafakari mambo hayo kwa mtazamo gani?

Ni rasimi sasa, ama sio Leo, au kesho ikiwa mambo yataendelea kuwa magumu kiasi hiki, shule binafsi zitafungwa, na au watumishi wa shule za binafsi watakuwa wahanga wa kukopesha fani zao kwa sababu wazazi hawana uwezo wa kulipia ada ili wao walipwe!
 
Watanzania, ki ukweli tumetofautiana sana kikipato, nimeleta hoja hii nikiamini kabisaa na nikiwa na ushahidi kabisaa kuwa, swala la maisha limekuwa tatizo, na ni janga kubwa

Bahati mbaya kabisa, wachangiaji tumekuwa tukiwakandamiza watanzania wenzetu kwa kuwaona ni kama hawafanyi kazi n.k

Embu tuzungumze kwa mtazamo wa uhalisia wa mambo yalivyo sasa
 
Hapo Ni kununua Dumu na fagio Mkuu huko private Ni pamoto Sana mkuu
 
Elimu ni bure kuanzia nursery hadi university,huko unakolipia umejitakia kwa hiyo kufa tuu itakuwa vizuri.
 
Usiyoyapenda kuyasikia ni haya hapa

Huko mashuleni kulikolipiwa na serikali kuna haya yafuatayo

Kuna kulipia mlinzi 10000 kwa mwaka, kuna test za kila siku sh 1000, kuna kulipia mitihani ya moko sh 12000 kila wakifanya!

Kuna pesa ya kula tsh 32000 kwa mwezi

Unayajua hayo mkuu!

Je, kuna ubule hapo?
 
Ulipie ada watoto ili ikiwezekana mfee, au bora mtumie kwa kula na watoto wasiende shule?
Chukua orodha ya mawaziri wa JMT jumlisha na orodha ya wakurugenzi wa makampuni 500 bora nchini Tanzania, jumlisha orodha ya wabunge. Ukipata hata 10% ya wao 'waliosoma St marry's', uje nikulipie ada ya watoto wako kwa miaka 10!
Nimesoma Mzumbe sec shule ya watoto wenye vipaji maalumu. Lakini kati ya hao wote, 80% hawajatoboa kimaisha.
Elimu sio msingi wa mafanikio. Invest on academic excellence at your on peril!
 
Usiyoyapenda kuyasikia ni haya hapa

Huko mashuleni kulikolipiwa na serikali kuna haya yafuatayo

Kuna kulipia mlinzi 10000 kwa mwaka, kuna test za kila siku sh 1000, kuna kulipia mitihani ya moko sh 12000 kila wakifanya!

Kuna pesa ya kula tsh 32000 kwa mwezi

Unayajua hayo mkuu!

Je, kuna ubule hapo?
Hayo uliyoyataja sio uniform bali huwa wazazi husika katika eneo tofauti wanaamua wanachotaka..

Kwa hiyo kwetu hakuna cha Mlinzi Wala kuchangia test au Moko kwa sababu hiyo mitihani huratibiwa na Wizara kwa std 7 na std 4.
 
Kwa jinsi ilivyo kwa sasa, huwenda nawakilisha wananchi wengi mamilioni kwa mamilioni wenye swali kama hili

Maisha yamekuwa ghali sana kushinda vipato vyetu,

Wengi wetu, vipato vyetu haviruhusu kucheza mbali na kula tuu, na hapo ni kwa kukatisha Milo, kama mtu kwa kipato hikihiki ambacho tulikitumia miaka michache iliyopita kwa kula na kulipia ada za watoto na mambo mbalimbali ya kifamilia, Leo kipato hikihiki, kinatulazimisha kufuta karibu mambo mengi ya mhimu na ya lazima

Kipato hiki kwa sasa, kinakulazimisha ukitumie kula tuu, usilipe ada na wala kufanya vitu vingine,

Swali najiuliza, mambo yanapokuwa hivi, ni kipi bora cha kufanya kuzingatia na mahitaji ya mhimu

Ulipie ada watoto ili ikiwezekana mfee, au bora mtumie kwa kula na watoto wasiende shule?

Je, serikali watatuelewa?

Na Je sasa, Serikali wanalifahamu hili kwamba wazazi wengi sana wanadaiwa huko mashuleni na uwezo wa kulipia ada watoto umeshuka na hswajui ni lini watalipa madeni yao?

Inapokuwa hivyo, serikali huyatafakari mambo hayo kwa mtazamo gani?

Ni rasimi sasa, ama sio Leo, au kesho ikiwa mambo yataendelea kuwa magumu kiasi hiki, shule binafsi zitafungwa, na au watumishi wa shule za binafsi watakuwa wahanga wa kukopesha fani zao kwa sababu wazazi hawana uwezo wa kulipia ada ili wao walipwe!
Kwani shule za government zinalipiwa ada sikuizi?

Kweli maisha Sasa Ni magumu, ila hali ikiwa ngumu mtoto bora umpeleke shule za serikali tu kuliko kudhalilika na kuwaua njaa watoto
 
Watanzania, ki ukweli tumetofautiana sana kikipato, nimeleta hoja hii nikiamini kabisaa na nikiwa na ushahidi kabisaa kuwa, swala la maisha limekuwa tatizo, na ni janga kubwa

Bahati mbaya kabisa, wachangiaji tumekuwa tukiwakandamiza watanzania wenzetu kwa kuwaona ni kama hawafanyi kazi n.k

Embu tuzungumze kwa mtazamo wa uhalisia wa mambo yalivyo sasa
Mkuu, hili uliloleta ni la msingi sana na ndo uhalisia jinsi ulivyo kwa sasa, hata kwa watumishi waandamizi na watu wengine wenye vipato vya kati ambao ndo tunatarajia wawe na uwezo wa kumudu maisha kwa kiwango kikubwa nao hali ni tete, pesa inaishia kwenye kununua chakula na kwenyewe ni kwa kupiga mahesabu makali, vipi watu wa hali ya chini. Hawa watu wanapokuwa wame relax kwenye ma viiieite ya mil 500 sidhani wanapata hata akili ya kufikiria ugumu walio nao wananchi.​
 
Kwani shule za government zinalipiwa ada sikuizi?

Kweli maisha Sasa Ni magumu, ila hali ikiwa ngumu mtoto bora umpeleke shule za serikali tu kuliko kudhalilika na kuwaua njaa watoto
Shule za serikali zina michango had I vichwa vinauma

Tatizo lililopo ni kuwa, eti hizo michango ni makubaliano ya wazazi, lakini ukweli ni kuwa, kamati zibazoundwa huko mashuleni Kwa kushirikiana na walimu, zinakuwa na mjadara wa pamoja kuhakikisha mambo ya michango yanapitishwa Kwa manufaa yao

Wazazi wakija kwenye vikao, nguvu kubwa ya kupitisha mambo hayo yanakuwa chini ya uongozi wa shule na kamati ya wazazi

Lakini ndani yake ni maumivu makali Kwa wazazi wengi,

Wazazi wamekumbwa tu kwenye mkumbo, lkn maisha yao ni magumu kinoma na cha moto wanakioba

Wakikosa kupeleka michango, wanaambiwa, si mlikubalina wazazi kuwa na hiyo michango.?

Kwa hiyo, ili iwe bure, serikali iingilie kati kukataza kila kitu Kutoka Kwa wazazi
 
Watanzania, ki ukweli tumetofautiana sana kikipato, nimeleta hoja hii nikiamini kabisaa na nikiwa na ushahidi kabisaa kuwa, swala la maisha limekuwa tatizo, na ni janga kubwa

Bahati mbaya kabisa, wachangiaji tumekuwa tukiwakandamiza watanzania wenzetu kwa kuwaona ni kama hawafanyi kazi n.k

Embu tuzungumze kwa mtazamo wa uhalisia wa mambo yalivyo sasa
Mkuu, kwani una watoto wangapi?
 
Mkuu, kwani una watoto wangapi?
Hahaaa!

Mkuu, Nina familia ya watu wanne, baba,mama na watoto wawili,

Mkuu, kwani vipi, Mimi ni baba wa kazi haswaa, lakini sasa kipato changu chote kinaishia kwenye msosi na kisitoshe,

Hapo ni Mimi, na nikijipina ninaunafuu Mkubwa saana kikipato ukilinganisha na ambao kiukweli wako chini, je wao wanaishije yaani
 
Kuna mtu humu alisema kuna wakati ukiangalia net income yako unabaki kushangaa namna unavyosavaivu 😂
 
Watanzania, ki ukweli tumetofautiana sana kikipato, nimeleta hoja hii nikiamini kabisaa na nikiwa na ushahidi kabisaa kuwa, swala la maisha limekuwa tatizo, na ni janga kubwa

Bahati mbaya kabisa, wachangiaji tumekuwa tukiwakandamiza watanzania wenzetu kwa kuwaona ni kama hawafanyi kazi n.k

Embu tuzungumze kwa mtazamo wa uhalisia wa mambo yalivyo sasa
Hakika umesema kweli, sasa hvi unashika pesa unaangalia niende sokoni au bank kulipa ada tena ukiwa na watoto zaidi ya wawili ndo wazimu hupanda kabisa
 
Back
Top Bottom