Kwa porojo hizi za TRA ndiyo maana hata mapato ya kila mwezi yamebaki "midomoni" mwao

Umeeleza vizuri mkuu, wanaosema beno nduru yuko sahihi nashindwa kuwaelewa,kila kampuni inayofanya biashara ni lazima ilipe kodi na kodi hiyo inakatwa kwenye mapato ya kampuni husika.Hii ni hesabu rahisi lakn wenye mabenki wanatufanya tuwe kama wajinga wao.

!
!
Unajua maana ya VAT? Rudi Darasani kasome uelewe ndio uchangie, sio kuonesha uJeska wako hapa
 
Umeeleza vizuri mkuu, wanaosema beno nduru yuko sahihi nashindwa kuwaelewa,kila kampuni inayofanya biashara ni lazima ilipe kodi na kodi hiyo inakatwa kwenye mapato ya kampuni husika.Hii ni hesabu rahisi lakn wenye mabenki wanatufanya tuwe kama wajinga wao.
We chalii..................kama taaluma huijui kaa kimya! Unajiabisha jukwaani!
 
....niko upande wa TRA,kwanini mabenki yatulipishe wananchi pesa ambayo wangetakiwa kulipa wao?, wao mabenki si tayari walikuwa wanakata 800/- kwenye ATM, then serikali ilipotangaza kuwadai kodi wakapandisha mpaka 944/-!, ina maana wao wanataka faida yao ibaki palepale ila sisi wananchi ndio tuumie kwa niaba yao? HAIWEZEKANI.
Duuuuu...........soma mchezo kwanza kabla ya kuanza kupiga mashuti uchwara! Hizi ni taaluma za watu...bora ungekaa kimya tu!
 
Jana nilisikia taarifa kutoka TRA kuhusiana na ongezeko la kodi yaani V.A.T kwenye miamala ya simu na benki pia huduma zote za kifedha nikaanza kujiuliza maswali mengi bila majibu.

Eti TRA wanasema kuwa hiyo nyongeza ya asilimia 18 watakatwa mawakala wao kwamba mwananchi hakitakiwi kuguswa. Hizi ni porojo za aina yake kutolewa na taasisi nyeti ya kiserikali kama TRA.

Mimi moja kwa moja baada ya kusikia taarifa ile mbiombio nikawaza kuwa, ina maana TRA wamemega mapato yao ya mwisho wa mwaka yaani income tax? Kwamba mwisho wa mwaka pale tarehe 30 December wakati wa kulipa kodi ya income tax tayari tutaondoa ongezeko la 18% tulilolipa kama mawakala kwa kila muamala wateja wetu waliofanya? Nikamuuliza kidogo mmoja wa TRA akaniambia lah hasha bali mzigo huo ni wa mawakala bila kugusa makodi ya TRA ya mwisho wa mwaka na makodi mengine ya bodi mbalimbali. Nikastaajabu na kumuuliza, hiyo kodi inayotakiwa kulipwa nje ya utaratibu itatoka wapi?

Bahati mbaya au nzuri hata sheria ya kodi ya fedha "finance act imeeleza bayana kuwa mteja wa wakala ndiye atakayelipia kodi hiyo (Nyongeza) iliyopendekezwa na serikali.

Baada ya kuona jambo dogo kama lile likiwachanganya TRA, sasa nimekata jawabu la yale mapato yanayotangazwa kwa mbwembwe mbona hayaonekani? Na kwa ghafla sana nimeanza kuzipuuza taarifa mbalimbali zinazotolewa na TRA kwani nimegundua kuwa wamekalia tu siasa na porojo ila uhalisia unaonekana waziwazi.
Umenena vema
 
Kwakwel this is too much. M2 km ndo una kikampuni chako kuna several taxes unalipa provisional tax, corporate tax, sdl etc. Aya ukija kwa mfanyakaz PAYE hlf hii ndo inaumizs kubabeki hlf wa2 wananeemesha ma2mbo yao. Uje ulipe kodi ya jengo n bidhaa madukan znatakiwa ziwe n VAT so obviously wafanya biashara wataongeza hela 4 profit benefits.
Umeme wameeka VAT.
Jmn mbna tutakoma mwaka huu. Uyu baba haon kua wanancho wake 2naangamia. Kwakwel namba inasomwa na wote japo sikumpigia kura lkn n mm namba naisoma
 
Mimi Nadhani TRA wapo sahihi kusema Kuwa benki ndio wanaotakiwa kulipa kiasi hicho cha kodi ya ongezeko la thamani. Ikumbukwe kwamba pesa iliyopo benki ni tofauti Kabisa na bidhaa iliyopo dukani, nasema hivyo kwa sababu bidhaa iliyopo dukani ni Mali ya mwenye duka hadi pale ajapo mnunuzi wa bidhaa ndio yanafanyika mabadilishano ya umiliki wa hiyo bidhaa kupitia njia za kawaida za kibiashara. Lakini pesa iliyopo benki si Mali ya benki, ni Mali ya mwenye hazina pale benki. Namaanisha kwamba niwekapo pesa yangu benki ile pesa siimilikishi benki na benki hainilipi chochote (kwa hazina ya akiba) badala yake nakuwa Kama nimewakopesha benki kwa riba ya asilimia 0. Kwa Kuwa nakuwa nimewakopesha, benki wanaweza wakaitumia kufanya chochote ila ninapohitaji kiasi chochote cha pesa kisichozidi kiasi nilichowapa wanapaswa kunipa wakati huohuo.
Kazi inaanzia hapa sasa ni Nani anayepata faida Kati ya benki na Mtu mwenye hazina benki, moja kwa moja utagundua Kuwa benki ndio wapatao faida kutokana na gharama za kila muamala niufanyao benki. Kwa Kuwa wao ndio waingizao kipato, imewapasa sasa kulipa kodi ya ongezeko la thamani kutokana na kiasi wanachokiingiza. Ikumbukwe pia ya kwamba benki ni taasisi ya kifedha ipokeayo malighafi (fedha tuziwekazo kwenye hazina zetu) bure kabisa na ikumbukwe pia ya kwamba pesa tuziwekazo benki tayari huwa zimekatwa kodi na kwa Kuwa siingizi kiasi chochote kipya cha pesa Kama faida au ujira katika muamala niufanyao benki, sipaswi kukatwa kodi ya ongezeko la thamani katika muamala huo.

Ni mawazo yangu tu, yanawezwa yakapuuzwa Kama hayana ukweli!
 
Mkuu ww hujui sera za biashara. Kila kampuni ina profit policy yake interms of percentage. Kwamba kwenye kila muamala benki imejiwekea sera ipate faida kiasi gani, sasa unapomwongezea cost nayeye atatafuta namna ya kumaintiain profit yake ileile ambapo kimsingi ni lazima ataongeza bei ya bidhaa husika. Kwahiyo hamna namna ni lazima benki zitaongeza bei zao. Mfano mdogo. Ulikuwa unanunua mzigo wa jumla kwa bei X na ww unsuza kwa bei Z. sasa hivi bei ya mzigo wa jumla imepanda hadi bei Y, je ukienda kuuza kwa reja reja utauza kwa bei ileile uliyokuwa unauza mwanzo au nawewe utaongeza??
Ni jambo la kibiashara wala si wizi.
wewe...! unatakiwa kufahamu kuwa kodi ni elastic kulingana na hali ya soko. Inaweza kubebwa na consumer, service provider/producer au kugawanywa baina ya pande zote mbili.
 
wewe...! unatakiwa kufahamu kuwa kodi ni elastic kulingana na hali ya soko. Inaweza kubebwa na consumer, service provider/producer au kugawanywa baina ya pande zote mbili.
Hujui maana ya VAT ww. Sibishani na asiyejua maana Anaejua na asiejua, hawa wawili hawawi sawa ktk maelezo yao.
 
Umeeleza vizuri mkuu, wanaosema beno nduru yuko sahihi nashindwa kuwaelewa,kila kampuni inayofanya biashara ni lazima ilipe kodi na kodi hiyo inakatwa kwenye mapato ya kampuni husika.Hii ni hesabu rahisi lakn wenye mabenki wanatufanya tuwe kama wajinga wao.
Na wewe haujaelewa kabisa. Bank charges ni sehemu ya mapato kwa benki na tayari wanalipa income tax, katafakari upya bro.
 
Mimi Nadhani TRA wapo sahihi kusema Kuwa benki ndio wanaotakiwa kulipa kiasi hicho cha kodi ya ongezeko la thamani. Ikumbukwe kwamba pesa iliyopo benki ni tofauti Kabisa na bidhaa iliyopo dukani, nasema hivyo kwa sababu bidhaa iliyopo dukani ni Mali ya mwenye duka hadi pale ajapo mnunuzi wa bidhaa ndio yanafanyika mabadilishano ya umiliki wa hiyo bidhaa kupitia njia za kawaida za kibiashara. Lakini pesa iliyopo benki si Mali ya benki, ni Mali ya mwenye hazina pale benki. Namaanisha kwamba niwekapo pesa yangu benki ile pesa siimilikishi benki na benki hainilipi chochote (kwa hazina ya akiba) badala yake nakuwa Kama nimewakopesha benki kwa riba ya asilimia 0. Kwa Kuwa nakuwa nimewakopesha, benki wanaweza wakaitumia kufanya chochote ila ninapohitaji kiasi chochote cha pesa kisichozidi kiasi nilichowapa wanapaswa kunipa wakati huohuo.
Kazi inaanzia hapa sasa ni Nani anayepata faida Kati ya benki na Mtu mwenye hazina benki, moja kwa moja utagundua Kuwa benki ndio wapatao faida kutokana na gharama za kila muamala niufanyao benki. Kwa Kuwa wao ndio waingizao kipato, imewapasa sasa kulipa kodi ya ongezeko la thamani kutokana na kiasi wanachokiingiza. Ikumbukwe pia ya kwamba benki ni taasisi ya kifedha ipokeayo malighafi (fedha tuziwekazo kwenye hazina zetu) bure kabisa na ikumbukwe pia ya kwamba pesa tuziwekazo benki tayari huwa zimekatwa kodi na kwa Kuwa siingizi kiasi chochote kipya cha pesa Kama faida au ujira katika muamala niufanyao benki, sipaswi kukatwa kodi ya ongezeko la thamani katika muamala huo.

Ni mawazo yangu tu, yanawezwa yakapuuzwa Kama hayana ukweli!
boss si kuwa unaipa bank faida ila benki inakuuzia huduma na hiyo huduma ndo unailipia na kama unailipia huduma basi VAT itakatwa kwa kutumia hiyo huduma unayopokea
 
Umeeleza vizuri mkuu, wanaosema beno nduru yuko sahihi nashindwa kuwaelewa,kila kampuni inayofanya biashara ni lazima ilipe kodi na kodi hiyo inakatwa kwenye mapato ya kampuni husika.Hii ni hesabu rahisi lakn wenye mabenki wanatufanya tuwe kama wajinga wao.

Sio lazima uchangie kila kitu mkuu, wenye taaluma yao wakiona huu upuuzi ulioandika, wanasikia kichefuchefu...
Kodi ya ongezeko la thamani (VAT) inalipwa na final consumer na si vinginevyo.
Service provider anatumika kama agent wa serikali katika kukusanya mapato. Yeye analipa corporate tax ambayo ni 30%,ya faida yake kwa mwaka.

Usichangie vitu usivyovijua... Mnakera sana nyie watu.
 
Back
Top Bottom