G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,595
- 36,017
Jana nilisikia taarifa kutoka TRA kuhusiana na ongezeko la kodi yaani V.A.T kwenye miamala ya simu na benki pia huduma zote za kifedha nikaanza kujiuliza maswali mengi bila majibu.
Eti TRA wanasema kuwa hiyo nyongeza ya asilimia 18 watakatwa mawakala wao kwamba mwananchi hakitakiwi kuguswa. Hizi ni porojo za aina yake kutolewa na taasisi nyeti ya kiserikali kama TRA.
Mimi moja kwa moja baada ya kusikia taarifa ile mbiombio nikawaza kuwa, ina maana TRA wamemega mapato yao ya mwisho wa mwaka yaani income tax? Kwamba mwisho wa mwaka pale tarehe 30 December wakati wa kulipa kodi ya income tax tayari tutaondoa ongezeko la 18% tulilolipa kama mawakala kwa kila muamala wateja wetu waliofanya? Nikamuuliza kidogo mmoja wa TRA akaniambia lah hasha bali mzigo huo ni wa mawakala bila kugusa makodi ya TRA ya mwisho wa mwaka na makodi mengine ya bodi mbalimbali. Nikastaajabu na kumuuliza, hiyo kodi inayotakiwa kulipwa nje ya utaratibu itatoka wapi?
Bahati mbaya au nzuri hata sheria ya kodi ya fedha "finance act imeeleza bayana kuwa mteja wa wakala ndiye atakayelipia kodi hiyo (Nyongeza) iliyopendekezwa na serikali.
Baada ya kuona jambo dogo kama lile likiwachanganya TRA, sasa nimekata jawabu la yale mapato yanayotangazwa kwa mbwembwe mbona hayaonekani? Na kwa ghafla sana nimeanza kuzipuuza taarifa mbalimbali zinazotolewa na TRA kwani nimegundua kuwa wamekalia tu siasa na porojo ila uhalisia unaonekana waziwazi.