Wanasayansi wengi wamekuwa wakielezea ulimwengu wetu kuwa ni dude kubwa mno lisilo kuwa na mwisho(means the universe size is almost infinity)
Leo hebu tuchambue na kuangalia ukubwa wa dunia yetu
Kabla ya kuendelea naomba kuelezea kidogo kuhusu Galaxy, huu ni mkusanyiko wa nyota,sayari na vyote vilivyoko katika ukanda husika,Galaxy hutofautiana sana kwa ukubwa ila ya kati inakadiriwa kuwa na nyota bilioni 400 na mabilioni ya sayari,Galaxy yetu inaitwa milky way ambayo ina mabilioni ya sayari na na nyota,hebu sasa twende kwa picha
1.Hii ni dunia yetu,sehemu tunamoishi
2:Huu ni mfumo wetu wa jua,solar system
3.Huu ni umbali kutoka duniani mpaka mwezini
katika umbali Huu wa mwezini mpaka duniani waweza Panga sayari Tisa na zikaenea!
4.Hii ni sayari ya Jupiter ni kubwa sana
Hicho kidoti kidogo amerika kaskazini
5.Huu ni mwonekano wa Saturn ukiweka dunia katika ringi zake,mwonekano wa dunia sita katika ringi zake
6.Hebu tulinganishe Jua na dunia,
Jua 1=dunia milioni 1!!!,yaani dunia kwenye jua inaingia mara milioni 1
7.Hii ni picha maarufu ya dunia iliyochukuliwa kutoka maili bilioni 4 ,hicho kidoti kidogo ni dunia
8.Tuliangalia kuwa katika jua dunia huingia Mara milioni moja
Hebu tulinganishe jua na nyota zingine
9.Kuna nyota inaitwa Articus ni Mara 16,000 ya jua,hicho kidoti kidogo ni jua
10:Kuna nyota inaitwa Alpha scropti ni kubwa Mara 690 milioni kuliko jua,hicho kidoti kidogo ni jua
11.Kuna nyota inaitwa VY Canis major ni kubwa Mara bilioni 2.9
Kuliko jua,hapo usisahau kulinganisha jua na dunia!
Hicho kidoti kidogo cha mwisho ni jua
12.Hebu tuangalia galaxy yetu,ni ukanda wenye nyota zaidi ya bilioni 400 pamoja na sayari zake
Ndani ya sekunde moja mwanga huzunguka dunia Mara saba na nusu,ukienda kwa speed hiyo ulitakuchukua miaka 100,000 kutoka katika ukanda wetu(milky way Galaxy)
13:milky way Galaxy ni kubwa sana,na hyo doti ya njano ni nyota tyu ambazo unauwezo wa kuziona kati ya mabilioni ya nyota
Najua umeshawishika kuona milky way Galaxy(ukanda wetu wa nyota ni mkubwa sana lakini nikuambia kuwa ni kidude kidogo sana ukilinganishwa na dubwasha kubwa la Galaxy liitwalo 1C1011,galaxy Hii ukienda na speed ya mwanga ambayo nilikueleza kuwa itakuchukua miaka 6,000,000
Milky way ni hicho kidoti kidogo kulinganisha na 1C1011 Galaxy
14.Hebu tuchukue Hubble telescope, picha Hii ina mabilioni ya Galaxy na kila Galaxy ina mabilioni ya nyota na sayari mabilioni pia na kila doti unayoona hapo ni galaxy nzima
Oooh umechoka[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2],subiri
Hii ni dunia
Tukizoom zaidi Hii ni solar system
Tukizoom tena tunaona majirani katika solar system katika picha nzima ya galaxy
Tukizoom tunaona milky way galaxy ni hicho kidoti!
Itaendelea...