mhWanasayansi wengi wamekuwa wakielezea ulimwengu wetu kuwa ni dude kubwa mno lisilo kuwa na mwisho(means the universe size is almost infinity)
Leo hebu tuchambue na kuangalia ukubwa wa dunia yetu
Kabla ya kuendelea naomba kuelezea kidogo kuhusu Galaxy, huu ni mkusanyiko wa nyota,sayari na vyote vilivyoko katika ukanda husika,Galaxy hutofautiana sana kwa ukubwa ila ya kati inakadiriwa kuwa na nyota bilioni 400 na mabilioni ya sayari,Galaxy yetu inaitwa milky way ambayo ina mabilioni ya sayari na na nyota,hebu sasa twende kwa picha
1.Hii ni dunia yetu,sehemu tunamoishi
2:Huu ni mfumo wetu wa jua,solar system
3.Huu ni umbali kutoka duniani mpaka mwezini
katika umbali Huu wa mwezini mpaka duniani waweza Panga sayari Tisa na zikaenea!
4.Hii ni sayari ya Jupiter ni kubwa sana
Hicho kidoti kidogo amerika kaskazini
5.Huu ni mwonekano wa Saturn ukiweka dunia katika ringi zake,mwonekano wa dunia sita katika ringi zake
6.Hebu tulinganishe Jua na dunia,
Jua 1=dunia milioni 1!!!,yaani dunia kwenye jua inaingia mara milioni 1
7.Hii ni picha maarufu ya dunia iliyochukuliwa kutoka maili bilioni 4 ,hicho kidoti kidogo ni dunia
8.Tuliangalia kuwa katika jua dunia huingia Mara milioni moja
Hebu tulinganishe jua na nyota zingine
9.Kuna nyota inaitwa Articus ni Mara 16,000 ya jua,hicho kidoti kidogo ni jua
10:Kuna nyota inaitwa Alpha scropti ni kubwa Mara 690 milioni kuliko jua,hicho kidoti kidogo ni jua
11.Kuna nyota inaitwa VY Canis major ni kubwa Mara bilioni 2.9
Kuliko jua,hapo usisahau kulinganisha jua na dunia!
Hicho kidoti kidogo cha mwisho ni jua
12.Hebu tuangalia galaxy yetu,ni ukanda wenye nyota zaidi ya bilioni 400 pamoja na sayari zake
Ndani ya sekunde moja mwanga huzunguka dunia Mara saba na nusu,ukienda kwa speed hiyo ulitakuchukua miaka 100,000 kutoka katika ukanda wetu(milky way Galaxy)
13:milky way Galaxy ni kubwa sana,na hyo doti ya njano ni nyota tyu ambazo unauwezo wa kuziona kati ya mabilioni ya nyota
Najua umeshawishika kuona milky way Galaxy(ukanda wetu wa nyota ni mkubwa sana lakini nikuambia kuwa ni kidude kidogo sana ukilinganishwa na dubwasha kubwa la Galaxy liitwalo 1C1011,galaxy Hii ukienda na speed ya mwanga ambayo nilikueleza kuwa itakuchukua miaka 6,000,000
Milky way ni hicho kidoti kidogo kulinganisha na 1C1011 Galaxy
14.Hebu tuchukue Hubble telescope, picha Hii ina mabilioni ya Galaxy na kila Galaxy ina mabilioni ya nyota na sayari mabilioni pia na kila doti unayoona hapo ni galaxy nzima
Oooh umechoka ,subiri
Hii ni dunia
Tukizoom zaidi Hii ni solar system
Tukizoom tena tunaona majirani katika solar system katika picha nzima ya galaxy
Tukizoom tunaona milky way galaxy ni hicho kidoti!
Local galactic Group
Ni mkusanyiko wa galaxy zaidi ya 54 ikikadiriwa kuwa na gravitational force centre kati ya milky way galaxy na andromeda
Virgo Supercluster
Huu ni mkusanyiko wa galaxy zaidi ya 100 uliogunduliwa mwaka 2014,group hii ni moja tu kati ya milioni kumi ya namna hii!
Ulimwengu unaoonekana!
hapa tunaongelea pale ambapo darubini zetu na telescope zimeishia,kuna umbali wa 93 billions light years kwa diameter, kwahyo ulimwengu wote tunaoongelea tunaishia hapo kwenye huo mduara kinachoendelea baada ya hapo ni space na anga kwahyo anga halina mwisho,kwhy kwenye hyo mduara ndipo wanasayansi wanapoishia haimaanishi kuwa ndo mwisho wa ulimwengu la hasha,ila mpaka huo mpaka kuna galaxy billioni 400 kila galaxy moja ina mabilioni ya sayari na nyota,inakadiriwa kuwa kuna nyota nyingi katika anga kuliko vipunje vya mchanga dunia nzima
Kwenye huo mduara ndipo tulipoishia ila ulimwengu unapanuka kuliko speed ya mwanga unavosafiri,hebu fikiria mwanga ndani ya sekunde moja unazunguka dunia Mara 7.5 halafu ulimwengu unajitengeneza zaidi ya speed ya mwanga its really amaizing
Yaani ukitoka nje ya huo mduara tunaenda kugusa ulimwengu tusiojua,yaani sehemu ambazo telescope zetu hazijafika kuzichunguza,inamaana porojo zote hizi za mabilioni ya galaxy ni ndani ni mduara huo,
Kwahyo ukitaka kujua ulimwengu mzimaa
Unachukua ulimwengu tuuonao
Observable universe+unknown universe=Total universe
Nini maana ya ulimwengu tusiojua?(unknown universe?)
hii ni sehemu inayoendelea baada ya mduara huo ni sehemu hii ina nishati iitwayo dark energy ambayo inawezesha Galaxy mpya kuundwa kila siku, nyota,sayari na galaxy zinaendelea kujitengeneza kwa speed zaidi ya light na ukumbuke speed ya light unazunguka dunia Mara 7 ndani ya sekunde moja,kwahy kutokana na hali hii ulimwengu utakuwa mkubwa sana na binadamu hatutaweza kuuona mwisho wake
Je ulimwengu mzimaa kuna galaxy ngapi ?
Jibu ni zaidi ya trilioni mbili,ulimwengu huu ni mkubwa mno mno mno mno
Universe is really big
Paulo illakwahhi Jf member!
Very Interesting
...Maji huwa hayapindi?? Hebu chukua Moira halafu jaza kikombe maji na uyamwage pale juu ya ule Moira uone maji yatafanya nini.....!elimu ya science ya ulimwengu ni elimu ya kusadikika haina ukweli wowote wala haiingii akilini kama tutakuwa na uwezo wa kufikiri,binadamu hatuwezi kuishi kwenye dunia yenye shepu ya chungwa,na kama ingekuwa kweli tungekuwa tunaweza kuishi kwenye milima mikubwa kwa kuganda pembezoni mwa milima bila ya kuanguka.
dunia haiwezi kuwa duara na maji kuganda nje ya dongo la dunia na kisha iwe inaruka angani kwa speed na masafa tunayoambiwa hii haiwezekani kabisa,katika uhalisi wa maji hayawezi kupinda kufata umbo la nje la kitu chochote,maji popote yalipo ni lazima yawe level hio ndio sifa kuu ya maji,na ndio mana tunatumia lever za maji kujengea majumba ili kupata usawa wa nyumba
jua na mwezi ni vitu vipo sawa sawa na umbali wake kutoka ardhini ni sawa sawa kama tunavyoviona,pia kama utaangalia jua na mwezi utakuta vipo ndani ya wingu la blue havipo umbali wanaosema,pia mwezi hauna ardhi ya watu kwenda kutua,tukiwa hapa tunauona kuwa mwezi ni kitu kinapitisha mwangaza(transparent),utazame mwezi mchana utaliona wingu la buluu kwenye mwezi na usiku utaona wingu jeusi kupitia kwenye mwezi.
tumefundishwa gravity ndio inayotuzuia tusipeperushwe na speed ya dunia hiki ni kichekesho kikubwa,kwanini gravity haiwezi kuzuia mabofu na mifuko ya plastic na ni vyepesi sana, kwa ufupi hakuna gravity ni vitu vizito vinabaki ardhini na vyepesi vinakwenda angani
hatuwezi kufahamu kila kitu lakini upo uwezekano kuwa ukubwa wa dunia ndio hauna mwisho(infinity) wala sio duara na haizunguki wala kuruka,uhalisi ni kama tunavyoona kila siku dunia ipo tuli imetulia.
Kwanza hujajibu vyema swali nililokuliza.swala hili limejitokeza kwa wachangiaji wengi natarajia wanaweza kulisoma hapa
jua halizami wala haliendi chini ya dunia,linazunguka juu ya uso wa dunia, mzunguko mmoja unachukua masaa 24,ki ilivyo hasa kila kitu kipo kama tunavyokiona na tunavyokihisi, hatuhisi dunia kuzunguka hivyo ndio ilivyo haizunguki,jua lipo juu ya utosi hivyo ndio ilivyo jua haliko 93 mil miles,lipo juu ya utosi.
ngoja nitoe mfano mmoja hapa wa kuchemsha bongo,wengi wetu tunaweza tusifahamu lakini tujaribu
umbali wa jua kutoka duniani ni 93mil miles
mwangaza wa jua kufika duniani unachukua 8 mitutes, kwa hio umbali wa jua ni 8 light minute
tuchukulie kama jua lina umbali wa mara mbili zaidi 93x2=186mil mile, hapa tutaliona jua nusu ya lilivyokuwa kabla,ambapo umbali wake utakuwa 8x2=16 light minutes away
tukifanya umbali wa mara tano ya hio hesabu jua hatutaliona kabisa 93x5=465 mil miles away, sawa sawa na 8x5=40 light minutes away
swali linakuja hapa
katika nyota zote zilizo angani ambazo tunaziona,iliyo karibu sana ni 4.2 light years away
ikiwa tungeshindwa kuliona jua kwa umbali wa 40 lights minutes away, tunaziona vipi vyota zilizo na umbali wa 4.2 light years away