Kwa nini wanawake hufanya hivi???????

mnafiki huyo tena muambie akome na tabia yake mbovu ya kukuambia katongozwa ana mangapi hakuambii ila hilo la kutongozwa tù ndio aje kukuambia?
 
Mi wangu kila wik lazma atongozwe wakimwomba namba anawapa namba yangu, njemba linapiga cm linakutana na sauti ya kiume linaishia kuuma meno!
 
Tunatongozwa na wengi sasa unapoenda kumshtaki mmoja kwa mr anakuwa na wasiwasi mbona hao wengine hujamwambia.
 
The Boss,.personally kuna wale ving'ang'anizi,hao inabidi useme kwasababu wanaeza kufanya mambo ya ajabu balaa..but wengine,UTASEMA WANGAPI!..and kuna wanaume wanaopenda kuambiwa hivyo pia,.
 
Boss saa zingine huwa inakuwa ni kweli na saa zingine inawezakana isiwe kweli, kuna mwanamke mwingine unakuta anakwambia fulani ananitongoza wakati tayari kaishatembea nae na kuna mwingine atakwambia the same story lakini huyu akifanya hivyo ili hata kama ikitokea una suspicions juu ya huyo mtu inakuwa kama vile tayari alikuwa aliisha ku-alert mapema on the situations kwahiyo sometimes inakuwa kama vile kuchukua precautions mapema lakini the situation is still 50/50.
Mimi nilishawahi kuambiwa hivyo na mchumba wangu, nilipotilia shaka akanambia, kama jamaa angekuwa amekula asingenambia. Lakini mwisho wa siku nilikuja kusitukia demu wangu ana mimba ya jamaa. Meaning kwamba alipokuwa ananambia kwamba jamaa anamtongoza, alikuwa anachukua precaution ili nikiona sms ya huyo jamaa au nikiwaona pamoja nisishituke sana. Kwa kuamini kwamba jamaa anapoteza muda wake. Kwangu mimi mke wangu akiniambia anatongozwa na mtu, haraka naanza kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya mke wangu na mtongozaji.
 
The boss yani juzi tu nimekwambia yule jirani ananitaka, ukaniambia niachane nae kumbe nilikushangaza eeh. Minilitaka tu kuonyesha nilivomwaminifu na sitaki mwingine.
 
The boss, unatakiwa kujua kwamba wanawake tunapenda sana kusikilizwa, ndo maana mwanamke anapenda sana amsimulie ampendae kila kitu, na usipo msikiliza ukajidai uko buzy ndo unashangaa anakua mbea anaongea huko mtaani na wadada wengine kwakua hana wa kumuhadithia, wewe uko busy na mambo yako. Anachokwambia mwana mke ni kweli kama akikwambia katongozwa ujue nikweli, Kama ametembea nae hawezi hata kugusia akiogopa utamuhisi.
 
kuna wanaume wanapenda sana kuwabughudhi wake zao kwa swali hili - NANI ANAKUTONGOZA?Ukimwambia kosa! Usipomwambia kosa!

Ushauri kwa akina dada - msilogwe kusema hata siku moja...ukitongozwa fanya ni siri yako.Inaleta amani kwenye mahusiano.Ukisema inakusaidia nini?
Halafu ni utoto kusema vitu kama hivi maana maisha yana mambo mengi na unatakiwa utumie busara kujua lipi la kusema na lipi la kukaa kimya!
 
kuna wanaume wanapenda sana kuwabughudhi wake zao kwa swali hili - NANI ANAKUTONGOZA?Ukimwambia kosa! Usipomwambia kosa!

Ushauri kwa akina dada - msilogwe kusema hata siku moja...ukitongozwa fanya ni siri yako.Inaleta amani kwenye mahusiano.Ukisema inakusaidia nini?
Halafu ni utoto kusema vitu kama hivi maana maisha yana mambo mengi na unatakiwa utumie busara kujua lipi la kusema na lipi la kukaa kimya!

...duhh, ha ha ha...akili kumkichwe kwakweli!...heri ya nusu shari.
Nice topic Boss, haya mambo huletesha mixed emotions.
Binafsi, huonelea bora nidanganywe, ukweli unauma bana
Nice one WoS.
 
Hili huhitaji kulitolea darasa maana kila mtu akili kichwani mwake.Mtu mzima huyo siyo mtoto wa chekechea kumfundisha nini cha kufanya.

Nadhani hilo nalo ni la ushauri tu kama ulivyoshauri (na si fundisho)kufanya siri manake hata mashauri ya kuweka sirini nayo akili kumkichwa!!!!!!
 
Mi wangu kila wik lazma atongozwe wakimwomba namba anawapa namba yangu, njemba linapiga cm linakutana na sauti ya kiume linaishia kuuma meno!

Duuh, kwahiyo mkuu kama kuna wiki hutapigiwa simu na njemba ikimuulizia mkeo ujue keshaliwa, manake kwa mtindo huo wa kutongozwa kila wiki najua kuna mjanja atamchakachua tu siku moja!
 
wakati mwingine sisi wanaume ndio tunaleta balaa.
usione mkeo kasalimiwa/kachekewa na mtu shurti
uulize "nani yule" halafu ukiambiwa "jamaa anaitongoza" unaanza kung'aka!

tuwaache wake/wapenzi wetu wachuje wenyewe mambo ya kutuambia hata
kama umemuona anasalimiana na mtu wewe uchune tu kwani akitaka kukuambia
ni nani atafanya hivyo kama hataki hata ukiuliza utadanganywa au ndio utapata hilo
bomu la kutongozwa.

mkeo akiongea na simu "ulikuwa unaongea na nani?", akisalimiana na mtu "nani yule?"
akipewa lifti "nani yule", sasa utaacha kuambiwa "jamaa ananitongoza"!
 
Ukiona mpenzi wako amekutaarifu ujue hana mpango na huyo mtu na pengine anataka umsaidie kumuondolea usumbufu toka kwa anayemtongoza, sidhani kama mwanamke anania ya kutembea n mtu mwingine atakwambia hakika atanyamza kimya na kuendelea na uchakachuaji bila wewe kufaham
 
Back
Top Bottom