Kwa nini wanaume hamtukubali na watoto

Kwa nini wanaume hamtukubali na watoto

Anza kumshangaa Diamond kwanza Zari ni sawa na mama yake lakini kila kona wanasifiwa wanapendeza na watu wanajifanya hawajui kama Zari ni mama wa watoto watatu.

Unafki hautakwisha duniani.

hahaha kuna picha nimeiona leo wamefananishwa na janye west na Kim
 
Mmhm! Sijui nianzie wapi kusemea jambo hili
mara nyingi wanaume wengi hawapendi wanawake
waliozalishwa hivyo huwa na msimamo wao
wa kutaka kuoa wasio na watoto
wanaona wale walio na watoto washazeeka
hili ndo tatizo kubwa kwa wanaume
hawajui kuwa hao watoto ni viumbe wa mungu
na wameletwa duniani kwa mlengo wa mungu
mm nashangaa sana ila ni maamuzi ya mtu
kumpenda au kupenda kile apendacho
 
huwa niliamua kusoma u comment kisha na sepa ila kwa hili nimeamua kuliandikia
kwanza kabisa suala hili limefungana na mila na utamaduni katika jamii , na hili swala kwa tanzania limeiathiri sana kamii yetu kwa asilimia 70. namaanisha kuwa ni wanaume wachache mno ambao ni sawa na 30% wataishi na watoto wa mwanamke aliye muoa, na pia wengiwao itakuwa kwa condition flani flani aidha kama huyo mwanamke huyo baba mwenye mtoto alifariki, au yupo mbali mno na mahali wanapo ishi au huruma nyingine au hali ya uchumi ya mwanamke (mwanamke akiwa anauwezo au ana hisa asilimia 70 zaidi ya mumewe pale ndani.

ok niache hayo nije kwenye swali , ni kwanini sisi wanaume tuna kataa hao watoto au hata muda mwingine tuna kataa hata kuwaoa hao wanawake, the main reason ni wivu,na mostly huu wivu unakuwa katika hali ya kujenga tukio la namna huyu mwanamke alivyo ishi ni huyo mwnaume mpaka kuja kuzaa (hapa namaanisha the whole process esp katika mambo ya kindoa). aidha pointi ingine ni uaminifu, huwa sie waume tunatoa imani kwa mwanamke ambaye alikuja na mtoto kwa kujenga shaka kuwa tunaweza pia letewa watoto wngine ambao sio wetu katika familia, kingine ni kwamba jamii inayotuzunga ayo inachangia katika hilo wanajamii wana dertemine style ya maisha yetu, na wao ndio wanatufanya tuwe health so ukienda kinyume nao utaambulia stress daily na lebel mbali mbali.

my point.mimi kama mwanaume , kwanza na kubali kabisa kuwa kumpata mtoto nje ya ndoa ni kosa, na pia ni vizuri kutubu,lakini pia ningependa kuijuza jamii kuwa yule mtoto huwa anabaki kuwa ni mali au thamani ya mama.hivyo basi kama itaotokea ukamposa mwanamke mwenye mtoto uka muoa ni vyema huyo mwanamke ajue kwamba mtoto wake atamlea je,ila kama mimi mposaji nitajawa na huruma tukawachukua hao watoto ni vizuri tukawajuza kwa busara na hekima ya hali ya juu kwamba wao ni watoto wa mama yao, na wa mpende mama yao, na mama yao ndo mwenye haki juu yao kwa kila kitu.

kwenye views za kimila mnaweza endelea.
kueleza kuhusu kurithi na distributions of social need katika family juu yao.
naona wajomba wamekuwa ndo wahangaikaji sana katika hili esp katika malezi

nafikiri nimejaribu kulifungua swali la huyo mdada muulizaji
asante kwa ufumbuzi

je utaweza kumuoa mwenye mtoto?
 
Kiranga nimemuelewa hapa tunaongelea mwanamke mwenye mtoto before marriage na sio kwetu tu hata wao pia wanakuwa na watoto kabla.... Na ndio maana nikasema hapo swala ni upendo na kuchukuliana maisha yataenda...

Hii ya kwamba mwenye mtoto aolewe na mwenye mtoto sio solution masai dada

solution ni ipi
maana mara wanasema ndugu wataingilia,mara sijui nini

nahisi ni muda wa Wanaume kufata mioyo yao
 
Last edited by a moderator:
itara umenena vizuri kabisa.. ndio maana kwenye makabila mengine kama mume umeoa mke ana watoto na unawatunza wewe basi watoto watatambulika kama wako wewe unaewatunza na ikitokea yule mwanaume anataka mtoto wake basi ni lazima akulipe wewe kwanza ndio umpe mtoto yaani kwa maana nyingine analipa mahari kwa ajili ya mtoto(hela uliomtunza toka akiwa kwako). jamani kama nilivyo sema hakuna mwanamke anayependa kubeba mimba na aitunze mwenyewe au asiolewe, basi kama kuna mtu katika ukoo wake au family yake dada yake ajazalisha akaacha au mengineyo basi aanze kutupa maweeeeeeeeeeeeee

hakuna mtu huyo hakika
 
solution ni ipi
maana mara wanasema ndugu wataingilia,mara sijui nini

nahisi ni muda wa Wanaume kufata mioyo yao

Upendo utawale ..... Hatuwezi kuwa na mawazo sawa kuhusu hili ila ni ngumu kulitatua wanaume wameshajenga negative attitude kwetu tukiwa na watoto wanasahau nawao pia inaweza watokea.... Me nadhani tuchukuliane tu haya ni mapito dunia humu si vyema kulaumu sana kilichotokea
 
Mmhm! Sijui nianzie wapi kusemea jambo hili
mara nyingi wanaume wengi hawapendi wanawake
waliozalishwa hivyo huwa na msimamo wao
wa kutaka kuoa wasio na watoto
wanaona wale walio na watoto washazeeka
hili ndo tatizo kubwa kwa wanaume
hawajui kuwa hao watoto ni viumbe wa mungu
na wameletwa duniani kwa mlengo wa mungu
mm nashangaa sana ila ni maamuzi ya mtu
kumpenda au kupenda kile apendacho

umenena jambo
 
Upendo utawale ..... Hatuwezi kuwa na mawazo sawa kuhusu hili ila ni ngumu kulitatua wanaume wameshajenga negative attitude kwetu tukiwa na watoto wanasahau nawao pia inaweza watokea.... Me nadhani tuchukuliane tu haya ni mapito dunia humu si vyema kulaumu sana kilichotokea

yaaa upendo
 
ni ngumu haswa.....ndiyo maana nikashauri ili usiingizwe changa la macho bora utafute bikra....mana kuna case nyingi tu.......kama hiyo yako....na nyingine nyingi.....

bado ni tatizo kuna mkasa mmoja ulitokea wakati nipo Kigoma baba mmoja alitaka kumwacha mke kisa alikuja kugundua ana mtoto baada ya miaka kumi ya ndoa lakin alipohojiwa alidai mkewe alimkuta bikra hata yeye alishangaa kusikia na hatimae kuthibitisha mkewe kuwa na mtoto kabla ya ndoa

LABDA TUFANYE KAMA WAHINDI UNAMUOA AKIWA MDOGO UNAMLEA MWENYEWE
 
itara umenena vizuri kabisa.. Ndio maana kwenye makabila mengine kama mume umeoa mke ana watoto na unawatunza wewe basi watoto watatambulika kama wako wewe unaewatunza na ikitokea yule mwanaume anataka mtoto wake basi ni lazima akulipe wewe kwanza ndio umpe mtoto yaani kwa maana nyingine analipa mahari kwa ajili ya mtoto(hela uliomtunza toka akiwa kwako). Jamani kama nilivyo sema hakuna mwanamke anayependa kubeba mimba na aitunze mwenyewe au asiolewe, basi kama kuna mtu katika ukoo wake au family yake dada yake ajazalisha akaacha au mengineyo basi aanze kutupa maweeeeeeeeeeeeee

kuna walio olewa bahati mbaya kwa kero za wanaume akachika / wajane hao nao pia ni tatizo hapa kinachoonekana tatizo si mama ila ni watoto akizaa mtoto akatupa/au akalelewa na bibi akaficha na kumfundisha amwite majina yote isipokuwa mama huyu hana tatizo ila yule mkweli ndo tatizo hapa tunawafundisha dada zetu tabia za uongo na ukatili ili mradi apate mume basi ajitahidi kuficha maana si wote waliozaa ni wahuni nk
 
Dah sio wote aise ila kwa upande wangu sija bahatika kukutana na mwanamke mwenye watoto wa nje na ikitokea bas nita wa care kama wanangu wa kuwazaa coz mi mwenyew nimelelewa na baba wa kufikia na nimepewa elimu,malezi sawa bila kuonyesha ubaguzi kwa watoto wote japo alisha fariki lakini nilimueshimu kama baba na baba alie nizaa simjui mpaka leo. So mtu kama mimi sioni kama watoto wa mwanamke ni kipingamizi cha yeye kuishi na mimi na hata kama ana watoto wa 3 nitamshauri awa lete tuishi pamoja coz na wenyewe ni members wa familia.

yani ww ndo mwanaume ...am proud of you miaka 80000
 
  • Thanks
Reactions: 7ve
bado ni tatizo kuna mkasa mmoja ulitokea wakati nipo Kigoma baba mmoja alitaka kumwacha mke kisa alikuja kugundua ana mtoto baada ya miaka kumi ya ndoa lakin alipohojiwa alidai mkewe alimkuta bikra hata yeye alishangaa kusikia na hatimae kuthibitisha mkewe kuwa na mtoto kabla ya ndoa

LABDA TUFANYE KAMA WAHINDI UNAMUOA AKIWA MDOGO UNAMLEA MWENYEWE

hahaaa.....akaingizwa mkenge....
 
masai dada na wengine, nawatakieni heri na mafanikio tele katika mwaka huu mpya.

Nafikiri tatizo linaanzia kwenye tamaduni hasa zile zenye mlengo wa kiume (patrilineal) ambazo kwa sehemu kubwa watoto (na mali) ni wa baba(ukoo wa mwanaume). Katika tamaduni za namna hii, ni WAJIBU wa baba au ukoo wa baba kulea "watoto" wao katika ukoo (waliozaliwa ndani ya ndoa na hata wa nje).

Kwa hivyo, ukiona mwanamke kaachiwa kulea watoto, basi ujue huyo mwanaume au ukoo wake umeshindwa kutimiza wajibu wao. Utaratibu huu wa patrilineal (kama ukifanya kazi vizuri) unazo faida zake (kubwa ni uhakika wa malezi ya watoto wa ukoo huo). Infact, kama mwanamke amefiwa na mumewe, basi anaweza patiwa mrithi katika ukoo huo (ndugu wa kiume wa marehemu - hili najua lina magumu yake katika mazingira ya sasa), au kama hataki kurithiwa bado anaweza kubaki katika ukoo husika (provided haulewi na mwanaume wa ukoo mwingine) akisaidiwa na wanaukoo kulea watoto au kama anaamua kuolewa nje ya ukoo, basi hulazimika kuhama katika nyumba na kuachia mali za ukoo (ikiwemo watoto) kwa wanaukoo.

Kwa hivyo unaweza kuona katika utaratibu huu, huwezi kuta mwanamke analea watoto peke yake au mwanaume kulea watoto wa ukoo mwingine(watakushangaa!). Katika utaratibu huu kama mwanaume amezaa na mwanamke na kwa sababu moja ama nyingine hawakuoana basi ukoo wa mwanaume unao wajibu wa kuwakomboa (kuna faini inalipwa kwa "kuingia bila hodi" au "kufanya uharibifu" ) watoto hao (wakifikia umri wa kuweza kutenganishwa na mama-aghalabu miaka 3 hivi). Mkishindwa kuwakomboa mara nyingi watoto hao hubakia katika ukoo wa mwanake (kulelewa na babu au wajomba) na kuchukua majina ya ukoo huo ("ujombani"). Hata ikitokea kuachana bado watoto wanabaki kwa baba au ukoo wa baba (ni "haki" na wajibu wao).

Matatizo yanayotokea sasa (Hilo la mwanamke kuachwa wa watoto, na hivyo kupelekea mwanaume mwingine kumkuta nao) ni matokeo ya tamaduni hizi kupungua (kutozingatiwa, kufuata baadhi ya misingi na kuacha mingine), mchanganyiko katika kuoana watu wa tamaduni tofauti (intermarriages) - matrileneal na patrilineal etc., kuiga tamaduni zingine bila kuwa na mifumo ya kijamii inayo support tamaduni hizo nk. Watoto wa mitaani (na hata hawa "panya road" and the likes) wa ni mojawapo ya viashiria vya kuporomoka kwa tamaduni zetu (ambazo zilikuwa zinaprovide some form of life insurance kwa watoto na hata wajane) na kushindwa kwa tamaduni mpya na kuna masuala ya kiuchumi pia. Bila ya shaka, kuna mengi ya ku debate katika hili.
 
Kinachogomba hapo ni hali ya
1.Uwezekano wakukutana kimwili na huyo mwenye mtoto ni mkubwa sana kwa kisingizio cha mna mawasiliano kwa ajili ya mtoto.
2.Kuwa na share ya kimaongezi kuhusu malezi..yaan huyo jamaa mwenye mtoto atakuwa anahitaji au wewe utakuwa unahitaji kujua maendeleo ya huyo mtoto wakati huo unatakiwa kuwajibika katika majukumu yakulea familia na ya huyu mpya,kwa hiyo hapo inakuwa kama unatumikia mabwana wawili katika mlango wakulea mtoto wa mwanaume mwingine.
3.Kukwepa uwezekano wakugombea mali siku za mbeleni,kwa sababu mtoto atakuzwa katika nyumba nyingine wakati siyo origin yake pale,na atakuwa katika misingi na mtazamo kuwa nae ana haki zote katika mali zile pasipokujua kuwa yeye pale siyo origin yake.
4.Kukwepa kuharibu tabia za watoto wataotokana na damu nyingine,kwa sababu mtoto wako katokana na damu nyingine kwa hiyo atakuwa na tabia za asili za baba ake/kutoka katika ukoo wake,sasa anaweza akawaambukiza hawa wengine(ambapo hapa inazungumziwa tabia mbaya za kishenzishenzi).
5.Kukwepa hali yakuishi kwa wasiwasi wa tabia au mienendo ya mwanamke,kwa sababu ni ngumu sana kujua tabia au sababu haswa iliyofanya kwa nini ulizalishwa ukaachwa,hapa ukiuliza kwa mwanamke atakuambia mwanaume ni tatizo,hakuna mwanamke atayekuambia ukweli hata kama yeye ni chanzo.
Kwa hiyo hizo ndio sababu za msingi kwa uchache kwa nini wanaume hawataki kama siyo kutopenda kuoa wanawake waliokwisha zalishwa.
 
Ni swala la ajabu sana ambalo pengine ukilifukiria unaeza ukasikitika

ni kawaida sana wanaume kutuambiwa wana watoto hata watatu na wenyewe kuona kawaida sana bila hata kutushawishi kwamba utaishi na mwanangu

yaani wao uchukulia kawaida sana sisi kuishi na watoto wao bila kuuliza chochote na wao huona sinkikwazo chochote na pindi utakapokionesha basi unaonekana Mkatili unaonekana wewe sio mke mwema(JAPO KUNA WANAWAKE HUKATAA ) ila sio wengi

SASA IJE SISI NDO TUNA WATOTO
wanaume wengi hukataa kuoa mwanamke mwenye mtoto KWA MSISITIZO na hata kama akikubali husema basi mtoto wako akae kwa bibi au baba ake sijui atawajibika
na mambo mengi hapo katikati

SASA SWALI NI JE KWANINI NYIE MNAONA SISI KUKAA NA WATOTO WENU NI RAHISI LAKINI NYINYI KUKAA NA WETU NI ISSUE tena kubwa sana????

Kama unaona shida kukaa na watoto wa mmewako kataa kuolewa naye kwaniu atakufunga?? Muoaji ndiye anaye panga utaratibu anaoutaka mama
 
ngombezi alafu ukimuoa na akaamua kuzaa njee ya ndoa na yumo ndani ya ndoa ipo inakuwa vipi:wacko::wacko::sleepy:
 
Kiranga nimemuelewa hapa tunaongelea mwanamke mwenye mtoto before marriage na sio kwetu tu hata wao pia wanakuwa na watoto kabla.... Na ndio maana nikasema hapo swala ni upendo na kuchukuliana maisha yataenda...

Hii ya kwamba mwenye mtoto aolewe na mwenye mtoto sio solution masai dada

Kuoa ni suala binafsi.

Pia ni suala la kiutamaduni na kiuchumi.

Tukielimika na kutengeneza uchumi haya mengine yatajitengeneza yenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom