Kwa nini wanaume hamtukubali na watoto

Kwa nini wanaume hamtukubali na watoto

Ni swala la ajabu sana ambalo pengine ukilifukiria unaeza ukasikitika

ni kawaida sana wanaume kutuambiwa wana watoto hata watatu na wenyewe kuona kawaida sana bila hata kutushawishi kwamba utaishi na mwanangu

yaani wao uchukulia kawaida sana sisi kuishi na watoto wao bila kuuliza chochote na wao huona sinkikwazo chochote na pindi utakapokionesha basi unaonekana Mkatili unaonekana wewe sio mke mwema(JAPO KUNA WANAWAKE HUKATAA ) ila sio wengi

SASA IJE SISI NDO TUNA WATOTO
wanaume wengi hukataa kuoa mwanamke mwenye mtoto KWA MSISITIZO na hata kama akikubali husema basi mtoto wako akae kwa bibi au baba ake sijui atawajibika
na mambo mengi hapo katikati

SASA SWALI NI JE KWANINI NYIE MNAONA SISI KUKAA NA WATOTO WENU NI RAHISI LAKINI NYINYI KUKAA NA WETU NI ISSUE tena kubwa sana????
Lakini nyie wanawake ni kikwazo pia mfano mama mkwe, mawifi na mashangazi ndio wa kwanza kupinga kaka kuoa mke aliyezaa kabla
 
Kwa kuwa dada yangu umesema WANAUME,bhasi naomba nijibu swali kwa swali kama mwanaume ambae niko included humo...
Kwann mwanamke anaongezeka thamani na kuonekana wa maana sana endapo atajitunza mpaka wakati wa kuolewa????

Vp kama ndoa ya kwanza ilivunjika au mume kafariki???
 
Mmhm! Sijui nianzie wapi kusemea jambo hili
mara nyingi wanaume wengi hawapendi wanawake
waliozalishwa hivyo huwa na msimamo wao
wa kutaka kuoa wasio na watoto
wanaona wale walio na watoto washazeeka
hili ndo tatizo kubwa kwa wanaume
hawajui kuwa hao watoto ni viumbe wa mungu
na wameletwa duniani kwa mlengo wa mungu
mm nashangaa sana ila ni maamuzi ya mtu
kumpenda au kupenda kile apendacho

Wengine sio mpango wa MUNGU aisee yaani mtu arukeruke afanye umalaya ajazwe mimba halafu useme mpango wa MUNGU.
Mpango wa MUNGU ni mtu ajitulize mpaka wakati wa kuoa/kuolewa na haya matatizo ya kuzalia nyumbani na kuzalishwa kabla ya kuolewa yasingekiwepo.
 
ni ngumu haswa.....ndiyo maana nikashauri ili usiingizwe changa la macho bora utafute bikra....mana kuna case nyingi tu.......kama hiyo yako....na nyingine nyingi.....

Kuna wengine wanabikira za kichina, suala la kukubaliana tu....
 
Wengine sio mpango wa MUNGU aisee yaani mtu arukeruke afanye umalaya ajazwe mimba halafu useme mpango wa MUNGU.
Mpango wa MUNGU ni mtu ajitulize mpaka wakati wa kuoa/kuolewa na haya matatizo ya kuzalia nyumbani na kuzalishwa kabla ya kuolewa yasingekiwepo.

kuna wengine ni malaya na wakipata mimba wanatoa......ili akufurahishe wew umuone siyo malaya mana hana mtoto....na wala hajazaa wala kuzalishwa nyumbani........
 
Kuna wengine wanabikira za kichina, suala la kukubaliana tu....

makubaliano hapa umenena......

sasa kila mtu aheshimu makubaliano ya watu wengine na siyo kuponda.....ukiona mwanamme mwenzio ameamua kutunza na kulea bao la mwanaume mwenzake.....usimponde na kumshangaa na kumvunja moyo.....bali uheshimu yale makubaliano yake na mwenzake......basi.......

kabanga.....nashukuru kwa hili neno.....MAKUBALIANO
 
Last edited by a moderator:
masai dada na wengine, nawatakieni heri na mafanikio tele katika mwaka huu mpya.

Nafikiri tatizo linaanzia kwenye tamaduni hasa zile zenye mlengo wa kiume (patrilineal) ambazo kwa sehemu kubwa watoto (na mali) ni wa baba(ukoo wa mwanaume). Katika tamaduni za namna hii, ni WAJIBU wa baba au ukoo wa baba kulea "watoto" wao katika ukoo (waliozaliwa ndani ya ndoa na hata wa nje).

Kwa hivyo, ukiona mwanamke kaachiwa kulea watoto, basi ujue huyo mwanaume au ukoo wake umeshindwa kutimiza wajibu wao. Utaratibu huu wa patrilineal (kama ukifanya kazi vizuri) unazo faida zake (kubwa ni uhakika wa malezi ya watoto wa ukoo huo). Infact, kama mwanamke amefiwa na mumewe, basi anaweza patiwa mrithi katika ukoo huo (ndugu wa kiume wa marehemu - hili najua lina magumu yake katika mazingira ya sasa), au kama hataki kurithiwa bado anaweza kubaki katika ukoo husika (provided haulewi na mwanaume wa ukoo mwingine) akisaidiwa na wanaukoo kulea watoto au kama anaamua kuolewa nje ya ukoo, basi hulazimika kuhama katika nyumba na kuachia mali za ukoo (ikiwemo watoto) kwa wanaukoo.

Kwa hivyo unaweza kuona katika utaratibu huu, huwezi kuta mwanamke analea watoto peke yake au mwanaume kulea watoto wa ukoo mwingine(watakushangaa!). Katika utaratibu huu kama mwanaume amezaa na mwanamke na kwa sababu moja ama nyingine hawakuoana basi ukoo wa mwanaume unao wajibu wa kuwakomboa (kuna faini inalipwa kwa "kuingia bila hodi" au "kufanya uharibifu" ) watoto hao (wakifikia umri wa kuweza kutenganishwa na mama-aghalabu miaka 3 hivi). Mkishindwa kuwakomboa mara nyingi watoto hao hubakia katika ukoo wa mwanake (kulelewa na babu au wajomba) na kuchukua majina ya ukoo huo ("ujombani"). Hata ikitokea kuachana bado watoto wanabaki kwa baba au ukoo wa baba (ni "haki" na wajibu wao).

Matatizo yanayotokea sasa (Hilo la mwanamke kuachwa wa watoto, na hivyo kupelekea mwanaume mwingine kumkuta nao) ni matokeo ya tamaduni hizi kupungua (kutozingatiwa, kufuata baadhi ya misingi na kuacha mingine), mchanganyiko katika kuoana watu wa tamaduni tofauti (intermarriages) - matrileneal na patrilineal etc., kuiga tamaduni zingine bila kuwa na mifumo ya kijamii inayo support tamaduni hizo nk. Watoto wa mitaani (na hata hawa "panya road" and the likes) wa ni mojawapo ya viashiria vya kuporomoka kwa tamaduni zetu (ambazo zilikuwa zinaprovide some form of life insurance kwa watoto na hata wajane) na kushindwa kwa tamaduni mpya na kuna masuala ya kiuchumi pia. Bila ya shaka, kuna mengi ya ku debate katika hili.
heri ya mwaka mpya mkuu
nadhani tamaduni zetu na mazingira
 
Kinachogomba hapo ni hali ya
1.Uwezekano wakukutana kimwili na huyo mwenye mtoto ni mkubwa sana kwa kisingizio cha mna mawasiliano kwa ajili ya mtoto.
2.Kuwa na share ya kimaongezi kuhusu malezi..yaan huyo jamaa mwenye mtoto atakuwa anahitaji au wewe utakuwa unahitaji kujua maendeleo ya huyo mtoto wakati huo unatakiwa kuwajibika katika majukumu yakulea familia na ya huyu mpya,kwa hiyo hapo inakuwa kama unatumikia mabwana wawili katika mlango wakulea mtoto wa mwanaume mwingine.
3.Kukwepa uwezekano wakugombea mali siku za mbeleni,kwa sababu mtoto atakuzwa katika nyumba nyingine wakati siyo origin yake pale,na atakuwa katika misingi na mtazamo kuwa nae ana haki zote katika mali zile pasipokujua kuwa yeye pale siyo origin yake.
4.Kukwepa kuharibu tabia za watoto wataotokana na damu nyingine,kwa sababu mtoto wako katokana na damu nyingine kwa hiyo atakuwa na tabia za asili za baba ake/kutoka katika ukoo wake,sasa anaweza akawaambukiza hawa wengine(ambapo hapa inazungumziwa tabia mbaya za kishenzishenzi).
5.Kukwepa hali yakuishi kwa wasiwasi wa tabia au mienendo ya mwanamke,kwa sababu ni ngumu sana kujua tabia au sababu haswa iliyofanya kwa nini ulizalishwa ukaachwa,hapa ukiuliza kwa mwanamke atakuambia mwanaume ni tatizo,hakuna mwanamke atayekuambia ukweli hata kama yeye ni chanzo.
Kwa hiyo hizo ndio sababu za msingi kwa uchache kwa nini wanaume hawataki kama siyo kutopenda kuoa wanawake waliokwisha zalishwa.

umechanganua vyema sana

je hilo haliwezi kuaa kwa mwanaume pia endapo atakua ana mtoto na mwingine?
 

Attachments

  • 1420319207826.jpg
    1420319207826.jpg
    29.7 KB · Views: 128
Mi bado nakula sikukuu tu.....maana tunavunja kamati ya krikimas na new year hapa kuna kreti 12 zikipita kesho SAA nne zinarudishwa kwa muuzaji...
 
Mwanamke mwenye mtoto ni rahisi sana kurudiana na mwenye mtoto kuliko mwanaume mwenye mtoto hiyo ndo hofu yetu kubwa
 
Back
Top Bottom