Kwa nini Taifa Stars (Tanzania) haichezi mechi nyingi za kirafiki kama mataifa mengine?

Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,411
11,061
Wanajukwaa natumai nanyi ni mashuhuda timu yetu ya taifa stars haipati mechi nyingi za kirafiki tofauti kabisa na mataifa mengine hata majirani zetu wote wanacheza kwanzia mechi mbili hadi tatu kipindi cha ratiba ya FIFA ya mapumziko ya ligi mbalimbali Duniani.

Taifa hili lina tatizo gani haswaa? Kwa nini sisi Tanzania tupo hivi, seriously kwenye kila sekta tumepoa why?

TFF kazi yao ni ipi bajeti yao kwa kalenda ya FIFA inahusu matumizi ya vitu gani hasa.

Inaudhi na inakera sana Taifa gani hili hovyo kwenye kila kitu.

Wallace Karia anavimbiana tumbo tu.

Karibu kwa maoni
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Umeniwahi..nilikuwa na maswali kama yako..yaani kuna timu za Taifa kwenye hiki kipindi kifupi zimecheza mechi zaidi ya tatu..tena zile ambazo tuko nazo kwenye kundi moja.
 
Hili halijadiliwi sana kwenye platform za media na wadau,kwasababu Taifa stars haina mvuto.
wadau wanajadili kwanini timu ya taifa stars inafichwa wanaacha kujadili kukosekana mechi za kujipima nguvu.

tff wanajua hii timu haitofika mbali kuingia gharama za nini wakati taifa stars ni jamvi la wageni.
hata kufuzu kwake ni kwa mashaka mpaka Uganda wakalalamikia mechi ya mwisho ya kufuzu AFCON taifa stars likua na fixing.
 
Umeniwahi..nilikuwa na maswali kama yako..yaani kuna timu za Taifa kwenye hiki kipindi kifupi zimecheza mechi zaidi ya tatu..tena zile ambazo tuko nazo kwenye kundi moja.
Tena ni miaka yote trend ni hio hio na pia utamaduni umekuwa kucheza mechi nyingi nyumbani
 
Naweza nisiwe sahihi 💯, hz mechi za kimataifa huwa zinapandisha na kushusha madaraja kwenye viwango vya fifa. Sasa timu za madaraja ya chini huwa zinatafuta timu za madaraja ya juu yake au ya kati hili yainuke kwenye madaraja maana ukiwa unacheza na timu za madaraja ya chini zaidi points zako zinakuwa chache sana.

Sasa hapo vita ni kuwahi nani ni cheze nae ukiacha vitu vingine km kumgharamia usafiri na malazi, timu nyingi unakuta zimekuwa booked mapema hivyo basi taifa stars ndio huishia kuoketa timu za kawaida sana au kukosa kabisa.

Nini cha kufanya, stars anatakiwa kujipambanua kwenye michuano mikubwa hili apate mialiko kutoka timu nzuri zaidi
 
Hili halijadiliwi sana kwenye platform za media na wadau,kwasababu Taifa stars haina mvuto.
wadau wanajadili kwanini timu ya taifa stars inafichwa wanaacha kujadili kukosekana mechi za kujipima nguvu.

tff wanajua hii timu haitofika mbali kuingia gharama za nini wakati taifa stars ni jamvi la wageni.
hata kufuzu kwake ni kwa mashaka mpaka Uganda wakalalamikia mechi ya mwisho ya kufuzu AFCON taifa stars likua na fixing.
Wanasimba utawajua tu
 
Back
Top Bottom