Ushiriki wa Tanzania (Taifa stars) katika michuano ya AFCCON ni faida kwa Simba

Ozone_

Member
Dec 30, 2023
88
106
Habari za muda wadau wote wa michezo.

Baada ya timu ya taifa ya Tanzania maarufu kama taifa stars kutolewa katima michuano ya Afcon inayoendelea kufanyika nchini Ivory Coast mnamo siku ya jana.

Kiufupi michuano hii imekuwa sehemu ya faida kwa kikosi cha simba, hakuna asiejua kuwa kipa Aishi Manula alikaa ne muda mrefu kutokana na majeraha jambo ambalo lilipelekea kushuka kwa kiwango chake, kibaya zaidi mechi yake ya kwanza tu akakutana na zahama ya goli tano toka kwa watani. Kiuhalaisiq kipigo hicho kwanza kilishusha level ya kujiamini kwa kipa huyo pia hata imani ya benchi la ufundi na baadhi ya mashabiki ilipungua kwake.

Kwa upande mwingine kikosi kizima cha simba kilipata taharuki baada ya kipigo kutoka kwa wananchi ingawa hata kabla simba hakuwa na mchezo mzuri ila baada ya kipigo hali ilikuwa mbaya zaidi.

Kitu kilichotokea ni uongozi kuamua kusajili upya katikati ya msimu kitu ambacho sio rahisi kufanikiwa. Bahati nzuri ikatokea fursa ya kombe la mapinduzi ambalo kwa kiasi flani wachezaji walionesha kuongezeka. Sasa upande wa Manula kitendo cha kupewa game time katika mechi zote za Tanzania katika michuano ya afcon kimepelekea kuongezeka kwa hali ya kujiamini na hata ukiangalia game ya mwisho dhidi ya kongo unaweza kukubaliana na mimi.

Mda sio mrefu timu inarudi kambini na nina imani baada ya kurejea kwa ligi wapinzani mtaisoma namba.

Simba
#guvu moyaa

Sent from my SM-A137F using JamiiForums mobile app
 
faida kwa simba au kwa manulla?
simba kwa sasa haina stress za makipa, makipa wote walionesha kiwango kizuri mapinduzi, manulla ndo alikuwa na mtihani kwa benchika mbele ya ayubu. so ni faida tu kwa manula na sio simba maana kibu na mzamiru hawajatumika vya kutosha huko afcon
 
Back
Top Bottom