thedaydreamer
JF-Expert Member
- Nov 26, 2014
- 372
- 88
Naomba kuuliza wakuu, kwa uelewa wangu ni kwamba plate number za gari hazipaswi kujirudia na ikitokea huwa ni kosa tu la kibinaadam, gari zote na pikipiki nyingi ambazo nimeshaziona mpaka sasa huwa number ni 3 mfano T 111 AGG Namba tatu ina maana ni kuanzia 100 mpaka 999 sasa inakuaje hizo namba tatu za hapo hazijirudii? Sidhani kama number ya kati ya 100 mpaka 999 ndo idadi ya gari zote tz pamoja na pikipiki. Nini huwa kinafanyika kwenye utoaji wa hizo namba naomba kufahamishwa kwa mwenye uelewa.