Kwa nini plate number hazijirudii na zipo 3 tu?

Kwa nini plate number hazijirudii na zipo 3 tu?

Asiyelewa hadi haya maelezo basi anahitaji kutumbuliwa jipu na JPM.

Sikumbuki kuwahi kuona magari ambayo namba zake zinaanza na tarkimu ya sifuri (0), ila kama yapo basi idadi ya magari yatakayoweza kusajiliwa kwa kufuata mfumo huu tulionao (na unaoendelea kusajili) yatakuwa kama ifuatavyo:

1. Kesi ya kwanza:
Kama kuna namba ambazo zinaanza na herufi ya sifuri (0), yaani T0... mfano T001, T002, ...:, basi idadi ya tarakimu za T(numba ya kwanza) (nama ya pili)(namba ya tatu), mfano T001, T002, .... na kuendelea ( kwa zile zitakazoanza na sifuri peke yake) zitakuwa:

10x10x9=900 (Hapa hatuna T000 kama ilivyo kwa zingine kama T111, T222,... na kuendelea, sifuri haiwezi kuwa mwisho).

Hivyo namba ya MWISHO ya zile zinazoanza na 0 inabidi iwe kati ya 1 na 9 TU na siyo kati ya 0 na 9 (SIFURI HAITUMIKI KAMA TARAKIMU YA MWISHO HAPA) na hivyo kupunguza idadi ya uwezekano wa kupata tarakimu ya MWISHO kutoka 10 hadi 9. Kumbuka kuwa tarakimu ya kwanza na ya pili zenyewe zitaendelea kubaki na idadi ile ile ya "kumi kumi" kwa sababu zenyewe zaweza kuwa yoyote kati ya 0 na 9.

Kufuatia maelezo haya hapa juu hii ina maana kuwa kuna namna 9 TU ambavyo tarakimu ya MWISHO inaweza kupatikana, kwa zile zenye mfumo wa T0.. , na vile vile namna 10 kwa tarakimu ya KWANZA na ya PILI.

Kwa zile zenye mfumo kuanzia T1... mpaka T9..., zina namna 9x10x10 kwa kila mfumo (Hapa tarakimu yoyote inaweza kuwa namba ya kwanza kati ya 1 mpaka 9, na ya pili na ya tatu inaweza kuwa yoyote kati ya 0 na 9)

Kwa hiyo kesi hii, jumla ya namba zote kuanzia T0... mpaka T9.. itakuwa (9x10x10)x10=9000

Lakini pia vile vile kuna herufi 26 kuanzia A mpaka Z. Lakimi ni MUHIMU sana tukakumbuka kuwa katika herufi hizi, mbili hazitumiki ambazo ni O (ambayo inafanana na sifuri) na I (ambayo inafanana na moja). Tunabaki na herufi 24 ambazo kwa mpangilio wa herufi "tatu tatu", zina namna

24x24x24= 13824. Hapa herufi inaweza kujirudia mfano AAA, BBB, CCC, .... Kwa hali hiyo magari yanayoweza kusajiliwa kwa

mfumo huu wa T0... mapaka T9... na A mpaka Z (bila ya herufi I na O) ni magari

13824x(9x10x10)x10= 124,416,000


Kesi ya pili:

Kama hakuna magari yaliyosajiliwa kwa namba zinazoanza na T0... (yaani kwa mfano hakuna T001, T002, ...) basi magari yanayoweza kusajiliwa kwa mfumo huu ni 13824x(9x10x10)x9=111,974,400


Mbarikiwe wasomaji.
 
Back
Top Bottom