Naomba kuuliza wakuu, kwa uelewa wangu ni kwamba plate number za gari hazipaswi kujirudia na ikitokea huwa ni kosa tu la kibinaadam, gari zote na pikipiki nyingi ambazo nimeshaziona mpaka sasa huwa number ni 3 mfano T 111 AGG Namba tatu ina maana ni kuanzia 100 mpaka 999 sasa inakuaje hizo namba tatu za hapo hazijirudii? Sidhani kama number ya kati ya 100 mpaka 999 ndo idadi ya gari zote tz pamoja na pikipiki. Nini huwa kinafanyika kwenye utoaji wa hizo namba naomba kufahamishwa kwa mwenye uelewa.
Ni hivi,
Gari za mwanzo kabisa kwenye huu mfumo zitakuwa zilianza na
T 001 AAA hadi T 999 AAA
then
T 001 AAB hadi T 999 AAB
zikaendelea
T 001 AAC hadi T 999 AAC
hizo herufi zikaendelea mpaka zikafika AAZ
zilivyofika AAZ zikaanza tena kama ifuatavyo
T 001 ABA hadi T 999 ABA
T 001 ABB hadi T 999 ABB
T 001 ABC hadi T 999 ABC
.
.
.
T 001 ABZ hadi 999 ABZ
ikaanza tena
T 001 ACA hadi 999 ACA
ukiendelea na huo mtiririko baadae utakuja kufikia mahali ukute namba T 999 AZZ
ambapo itabidi gari linalofuatia lianze na namba zenye herufi zinazoanzia na B yaani
T 001 BAA.
kwa hiyo kwa hii system mpaka magari yajaze hiyo combination ya namba na herufi sio leo wa la kesho ndo maana mpaka leo magari yaliyopo Tanzania yamefikia herufi D tu
huwezi kukuta gari lenye namba kwa mfano
T 345 EAA kwa sasa ila baada ya muda yataanza kuwepo.
Hili swali limesaidia kuona jinsi gani watanzania wengi wanakariri masomo na sio kuelewa, kila mtu kakaa tu kusema mara probability mara permutations alafu kusolve zero, swali rahisi tu hata bila kusoma hizo hesabu unaweza jiongeza tu na kupata majibu.
T 111 AAA
Hapo kwenye namba 111 kuna uwezekano wa kua na namba 0-9 maana yake jumla unaweza kua na namba
sababu namba zinajirudia alafu note nimeanza na 9 kwa assumption kua namba hazianzii zero, kama zinaweza anzia zero itakua 10x10x10, hapo mbele kwenye AAA kwa kua herufi zipo 26, kuna uwezekano wa kuwepo
Jumla ya uwezekano wa namba zote ni
Kwa hiyo kuna uwezekano wa magari milioni 15 kupewa namba unique. Sidhani kama Tanzania kuna magari mengi kiasi hicho.
Sikumbuki kuwahi kuona magari ambayo namba zake zinaanza na tarkimu ya sifuri (0), ila kama yapo basi idadi ya magari yatakayoweza kusajiliwa kwa kufuata mfumo huu tulionao (na unaoendelea kusajili) yatakuwa kama ifuatavyo:
1. Kesi ya kwanza:
Kama kuna namba ambazo zinaanza na herufi ya sifuri (0), yaani T0... mfano T001, T002, ...:, basi idadi ya tarakimu za T(numba ya kwanza) (nama ya pili)(namba ya tatu), mfano T001, T002, .... na kuendelea ( kwa zile zitakazoanza na sifuri peke yake) zitakuwa:
10x10x9=900 (Hapa hatuna T000 kama ilivyo kwa zingine kama T111, T222,... na kuendelea, sifuri haiwezi kuwa mwisho).
Hivyo namba ya
MWISHO ya zile zinazoanza na 0 inabidi iwe kati ya 1 na 9 TU na siyo kati ya 0 na 9 (
SIFURI HAITUMIKI KAMA TARAKIMU YA MWISHO HAPA) na hivyo kupunguza idadi ya uwezekano wa kupata tarakimu ya MWISHO kutoka 10 hadi 9. Kumbuka kuwa tarakimu ya kwanza na ya pili zenyewe zitaendelea kubaki na idadi ile ile ya
"kumi kumi" kwa sababu zenyewe zaweza kuwa yoyote kati ya 0 na 9.
Kufuatia maelezo haya hapa juu hii ina maana kuwa kuna namna 9 TU ambavyo tarakimu ya
MWISHO inaweza kupatikana, kwa zile zenye mfumo wa T0.. , na vile vile namna 10 kwa tarakimu ya
KWANZA na ya
PILI.
Kwa zile zenye mfumo kuanzia T1... mpaka T9..., zina namna 9x10x10 kwa kila mfumo (Hapa tarakimu yoyote inaweza kuwa namba ya kwanza kati ya 1 mpaka 9, na ya pili na ya tatu inaweza kuwa yoyote kati ya 0 na 9)
Kwa hiyo kesi hii, jumla ya namba zote kuanzia T0... mpaka T9.. itakuwa (9x10x10)x10=9000
Lakini pia vile vile kuna herufi 26 kuanzia A mpaka Z. Lakimi ni MUHIMU sana tukakumbuka kuwa katika herufi hizi, mbili hazitumiki ambazo ni O (ambayo inafanana na sifuri) na I (ambayo inafanana na moja). Tunabaki na herufi 24 ambazo kwa mpangilio wa herufi
"tatu tatu", zina namna
24x24x24= 13824. Hapa herufi inaweza kujirudia mfano AAA, BBB, CCC, .... Kwa hali hiyo magari yanayoweza kusajiliwa kwa
mfumo huu wa T0... mapaka T9... na A mpaka Z (bila ya herufi I na O) ni magari
13824x(10x10x10)-1=
13,823,999 (tunatoa moja ile
T000 ambayo haipo)
Kesi ya pili:
Kama hakuna magari yaliyosajiliwa kwa namba zinazoanza na T0... (yaani kwa mfano hakuna T001, T002, ...) basi magari yanayoweza kusajiliwa kwa mfumo huu ni 13824x(9x10x10)-1=
12,441,599
Mbarikiwe wasomaji.