Sababu plate number za 3D kupigwa marufuku

Kaparare

Member
Apr 19, 2021
93
230
Sijui ni nani alianzisha Plate Number za 3D lakini ukweli ni Kwamba Ubunifu huu Ulipokelewa vizuri mtaani kiasi Cha Wabunifu Kuanza kuneemeka utundu wao.

Lakini Kabla Asali hiyo haijakolea mdomoni Utamu umeingia mdudu Serikali Kupitia Jeshi la Polisi wamepiga Marufuku matumizi ya Plate Number za 3D huku ikitoa sababu kadhaa ikiwepo kutokidhi viwango kisheria.

Lakini naomba nikuibie Siri Sababu kuu ni Moja tu 3D hazisomi kwenye Camera zinazowekwa Barabarani na Polisi kwa Lengo la Ku detect Madeni yaani gari ikipigwa faini na Polisi na ikawa Deni basi zile Kamera zinazowekwa Barabarani ili kunasa Magari yanayodaiwa gari zenye 3D hazionekani Kamera inashindwa kutambua kutoka na Ukubwa wa hizo Namba.

Poleni sana Wabunifu wa 3D Ubunifu wenu umegusa Mapato ya Serikali Kupitia Jeshi la Polisi.
 
Ni fursa nyingine inatakiwa izaliwe.

Machine za kudetect 3D number zitengenezwe.

Habari hii waipate huko Abroad!!
 
Wabunifu tumekosa ulaji huku mitaani, tulihisi wenyn tenda ya kutengeneza plate number wamesaga kunguni serikalini. Basi hayo makampuni wabuni 3d zinazosomwa na camera za polisi na sie wengine tubaki na ufundi wetu wa kuzikarabati kama kawaida. inakuaje unapewa tenda na serikali halafu unakosa ubunifu na wengine wakibuni kitu bora unakimbilia kusaga kunguni? Daima tutaendelea kubuni vitu bora bila kujali washindani wasaga kunguni
 
Back
Top Bottom